Yupo wapi Spika Mstaafu, Job Ndugai?

Yupo wapi Spika Mstaafu, Job Ndugai?

Alfred Daud Pigangoma

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2009
Posts
1,833
Reaction score
972
Katika hali ya kushangaza ambayo si utamaduni wa Watanzania pale inapotokea tendo la kuapishwa kwa mtu anayechukua nafasi katika uongozi wa Umma, mtangulizi / watangulizi wake kama wapo hai uhudhuria na hata kupiga nae picha ya pamoja!

Katika hali ya sintofahamu ambayo imezua taharuki mitaani ni kutoonekana kwenye viwanja vya Bunge siku ya leo kwa Ndugu Job Ndugai. Wanaharakati wa haki za binadamu tunahoji wapi mmemficha Job Augustino Ndugai? Na kwa nini asitokelezee kwenye picha ya ukumbusho?

Tunamtaka Job!

1643801483832.png

Yawezekana hakuwepo, kuna utaratibu wa kupiga kura by "proxy" yaani unaandaa barua ya kuomba udhuru wa kutohudhuria kikao Ila unatamka kura yako ni ndio hau hapana Ile itasehebiwa pamoja haupo in person.

Hata hivyo hajafanya sawa Kama hakuwepo.
 
Akizingua atastuka tayari Katibu wa Bunge anaitaarifu Tume ya Uchaguzi kuwa jimbo la Kongwa lipo wazi baada ya Mbunge wake kwa hiyari bila ya kushinikizwa kajiuzulu kwa maslahi ya nchi na chama
Nchi hii ukiwaza tofauti tu na Rais wake. Umekwisha.

Katiba hii ya Tanganyika siyo kabisa.

Nawaza wenzetu Kenya [emoji1139] Rais anawaza kivyake na makamu kivyake. Lakini hata mende hawafi !!
 
Aliemruhusu Msekwa akatoka kwake na hiyo suti aliyovaa,Mungu anamuona.
Wala sio mara ya kwanza ,hivi huyu so mine was Anna Abdala?

Hao wajukuu wanafanya kazi gani, wanamwqcha Babu na suti kiubwa za kichina...kwa mwili ule wangeenda kwa Msambaa mmoja wamshonee Kaunda Suti saafi
 
Katika hali ya kushangaza ambayo si utamaduni wa Watanzania pale inapotokea tendo la kuapishwa kwa mtu anayechukua nafasi katika uomgozi wa Umma, mtamgulizi / watangulizi wake kama wapo hai uhudhuria na hata kupiga nae picha ya pamoja!

Katika hali ya sintofahamu ambayo imezua taharuki mitaani ni kutoonekana kwenye viwanja vya Bunge siku ya leo kwa Ndugu Job Ndugai. Wanaharakati wa haki za binadamu tunahoji wapi mmemficha Job Augustino Ndugai? Na kwa nini asitokelezee kwenye picha ya ukumbusho?

Tunamtaka Job!
View attachment 2104427
Anakula pension yake, huku akitembelea shamba lake la mikorosho mara Kwa mara.
 
Akizingua atastuka tayari Katibu wa Bunge anaitaarifu Tume ya Uchaguzi kuwa jimbo la Kongwa lipo wazi baada ya Mbunge wake kwa hiyari bila ya kushinikizwa kajiuzulu kwa maslahi ya nchi na chama
Kama na yeye alivyopata habari mpasuko na kuona barua kuwa kajiuzuru [emoji119][emoji38][emoji38]
 
Nimekumbuka alichoongea Josephat Gwajima mwanzoni kabisa mwa hili sakata kabla Ndugai hajaomba msamaha.

"Si mmeona mimi...Kuna mmoja alikuwa ananifuatiliafuatilia,juzi karopoka vitu vya ajabu,Mmemsikia ee.

Na bado Mwaka 2022,Utawatafuta waliokuwa wanafanya uadui juu yako na hautawaona,Asema Bwana wa Majeshi".

Naona mmeanza kumtafuta jamaa na haonekani tayari.😁.
 
Wewe upo nje ya ukumbi wa bunge, utaoneshwa unachotakiwa kukiona...
 
Back
Top Bottom