MastaKiraka
JF-Expert Member
- Jan 10, 2015
- 5,736
- 18,648
Aliyefariki hakuwa na familia inayomtegemea???!!! huu ndio ubinafsi wa watu weusi unaotukwamisha kuendelea, kila mtu anawaza tumbo lake kuneemeka kupitia ofisi za umma.Amedai kuwa ulitokea mgogoro kati ya wakulima na wafugaji akiwa mkuu wa mkoa na katika tukio Hilo, alifariki mtu Mmoja, alipoitwa IKULU, Mzee Mwinyi alimtaka ajiuzulu Ili kuonyesha uwajibikaji.
Mzee Makamba akamwomba msamaha Rais Mwinyi na kumwambia amsamehe Kwa kuwa ana familia inayomtegemea, baada ya kusema hayo, Mzee Mwinyi alitabasamu na kumwambia nimekusamehe,usirudie tena.
Hawa wazee wawe wanapimwa akili kabla ya kufanyiwa mahojiano ama wasiwe wanahojiwa kabisa. Mada zote ni maslahi binafsi tu.Amesema HAYATI Mwinyi amemfaa sana Kwa kumteua Ukuu wa wilaya, Kisha baada ya miezi SITA akamteua ukuu wa Mkoa, na baadaye Mh KIKWETE akaendelea kumwamini.
Akibubujikwa na machozi Kwa Huzuni kubwa, amesema kuwa Ili Nchi iwe salama, inahitaji kuwa mikononi mwa mtu aina ya Mzee Mwinyi, na mtu hiyo wa aina ya Mzee Mwinyi, ni Mh Samia Suluhu Hassan.