Yusuph Makamba: Hayati Mwinyi ni hazina ya Mwenyezi Mungu kwa nchi yetu

Yusuph Makamba: Hayati Mwinyi ni hazina ya Mwenyezi Mungu kwa nchi yetu

Halafu anasema Rais Mwinyi akatabasamu!

Mtu kafa wao wanatabasamu! Wanapeana mistari ya maandiko halafu "akatabasamu."

Vichwa vibovu, uko sahihi kabisa.
Wewe ndio hujaelewa, Mzee Makamba alikuwa anamuelezea JINSI Mwinyi alivyomsamehe kumfuta ukuu wa Mkoa baada ya Kutokea KIFO katika Mkoa wake kilichotokana na ugomvi wa wakulima na wafugaji.
 
Wewe ndio hujaelewa, Mzee Makamba alikuwa anamuelezea JINSI Mwinyi alivyomsamehe kumfuta ukuu wa Mkoa baada ya Kutokea KIFO katika Mkoa wake kilichotokana na ugomvi wa wakulima na wafugaji.
Sijaelewa nini ????

Mzee Makamba kaongea pumba msibani!

Kasema alimwambia Mwinyi amsamehe kwa vile ana familia ya kutunza, akanukuu maandiko. Mwinyi akatabasamu, akamsamehe.

Uhoro mtupu. Familia ya marehemu imetunzwa na nani ? Mwinyi anatabasamu, raia kufa ni jambo la kutabasamu ? Wote wawili walikuwa tone deaf and out of touch, hawaelewi uzito wa dhamana za uongozi. Makamba anadhani tunafurahi kusikia tabasamu zao na kusameheana kwao kwa saab wana familia za kutunza? Pumba tupu.
 
Hapo Mwinyi alikengeuka, alipasa kufukuza Makamba Kwa kuwa alitoa sababu za kibinafsi.

Kumbe umeelewa vizuri🙏
 
Salaam, shalom!!!

Akizungumza Kwa uchungu mkubwa na majonzi alipokuwa akimuelezea HAYATI Mwinyi, amesema kuwa Mzee Mwinyi alikuwa mtu mwenye kheri, mpole na mstaarabu na muwajibikaji.

Amedai kuwa ulitokea mgogoro kati ya wakulima na wafugaji akiwa mkuu wa mkoa na katika tukio Hilo, alifariki mtu Mmoja, alipoitwa IKULU, Mzee Mwinyi alimtaka ajiuzulu Ili kuonyesha uwajibikaji.

Mzee Makamba akamwomba msamaha Rais Mwinyi na kumwambia amsamehe Kwa kuwa ana familia inayomtegemea, akanukuu maandiko yasemayo, baba hatahukumiwa Kwa dhambi alizofanya mtoto,baada ya kusema hayo, Mzee Mwinyi alitabasamu na kumwambia nimekusamehe,usirudie tena.

Amesema HAYATI Mwinyi amemfaa sana Kwa kumteua Ukuu wa wilaya, Kisha baada ya miezi SITA akamteua ukuu wa Mkoa, na baadaye Mh KIKWETE akaendelea kumwamini.

Akibubujikwa na machozi Kwa Huzuni kubwa, amesema kuwa Ili Nchi iwe salama, inahitaji kuwa mikononi mwa mtu aina ya Mzee Mwinyi, na mtu hiyo wa aina ya Mzee Mwinyi, ni Mh Samia Suluhu Hassan.

Mzee Makamba ameendelea kusema Mzee Mwinyi apumzike Kwa Amani na huko aendako awasalimu waliotangulia HAYATI Mzee Nyerere, HAYATI Mzee Mkapa na HAYATI Magufuli.

Source: Tanzania Broadcasting Corporation ( T. B. C).

Maombolezo yaendelee😪🙏
Wazuri hawafi bali wabayo ndo wanaokufa, hiyo ndo kauli tunaishi nayo
 
Hamna lolote,,,Mwinyi aliaandaa viongozi wezi kama akina jakaya ambao mpaka Leo Taifa hili linaliwa na familia zisizozidi 10. Wakiwepo watoto wa Masuria wao kina mwigulu. Afe kabisa asitudanganye hapa
 
Back
Top Bottom