Yutong na Scania

Yutong na Scania

sasa mbona matajiri hao hao wa mascania mbona wanaoleta yutong saizi. Sawa scania inadumu lkn ili upate faida inabidi ukae nayo miaka 6 wkt yutong miaka 2 tu imeleta faida. Kumbuka biashara ni faida

Scania zinalipa. Umeona Marcopolo Andare Class za Hood na Abood?? Zina zaidi ya miaka kumi na bado hazikamatiki. Tafuta Yutong au Shuchi yenye umri huo uone kituko.
 
mkuu kwa kusini wahdas si lolote si chochote mbele ya yutong, zhongtong na higer za machinga, buti la zungu, najma, maning nice au hamanju. labda ulisinzia ukadhani mabas mengine yako nyuma ilihali nyie ndio mnaburuza mkia



Nilisafiri na scania toka Ubungo kwenda mby, na basi la nganga scania lilikuwa la nne kutoka terminal na yalitangulia Newforce,nakuhakikishia kabla ya mlandizi tuliwapita na tuka ingia Mbeya Wa kwanza.Achana na scania.juzijuzi nilikuwa lindi scania za wahidas zilikuwa za kwanza kuingia pale wakati hao Wa China waliingia baada ya nusu Saa,ujue wahida mabus yao ni ya zamani sana ukilinganisha na yutong
 
zhongtong atasubiri sanaaaaaa nyuma ya yutong. hapana chezea yutong wewe labda higer ndo anaweza chuana na yutong


Malizeni mjadala then tupambanishe Zhongtong na Yutong...The crash of brothers

Yutong kwa zhongtong anakaa vizuri yutong ameachwa nyuma sana
 
mkuu kwa kusini wahdas si lolote si chochote mbele ya yutong, zhongtong na higer za machinga, buti la zungu, najma, maning nice au hamanju. labda ulisinzia ukadhani mabas mengine yako nyuma ilihali nyie ndio mnaburuza mkia

Mkuu kwa barabara ya Dar-Mbeya ni Yutong tu wengine wanafuta...
kuna new fors na super feo, Scania wanalia tu hapo.!!
 
princeses muro ni scania au ni yutong. kuna sikui ilinipita nilikuwa naendesha langu cruiser niko speed mia hamsin ila alinipita kama nimesimama
 
princeses muro ni scania au ni yutong. kuna sikui ilinipita nilikuwa naendesha langu cruiser niko speed mia hamsin ila alinipita kama nimesimama

Anazo zote Scania na Yutong.!!
 
Nimekubali Yutong za GREEN STAR ni bomun kwani kunasiku niliipanda kwenda Mbeya ilikuwa inachemsha vibaya sana,kili km kumi lilikuwa linasimama na kutiwa maji hadi abiria walipokuja juu ndio tulipofika morogoro wakatufaulishia ktk basi la Abood,scania
 
Yutong hazidumu. Ila nakuhakikishia ukikutana na madereva watundu utaipenda. Nakumbuka mwaka jana nilitoka Dodoma asubuhi saa12 na cresta Gx100.Da Yutong za Dodoma Arusha usipime.Gx100 dashbody inasoma140km unaona mko sambamba hadi kufika 150-160km/h ndo tukamwacha.
 
we vipi?mbona sikusomi?kwani marcopolo ni nissan?marcopolo ni haina mojawapo ya scania buses!
marcopolo ni mabodi na wala si mashine, hataTATA wanatumia mabodi ya marcopolo. Kwa kifupi ni kampuni ya kutengeneza bodi za mabasi.
 
Kwa route ya kusini hata iweje zile engine za lorry za wahidas awapite Buti la Zungu, Machinga, Najma,Hamanju hawa jamaa wanamagar ya kichina yanatembea hatari. Ila kulikuwa na Scania moja likiitwa Mtwara raha, nakuhakikishia hawa wote na Yutong zao wangesoma plate number. Mtwara raha ilikuwa ni subscania inatembea ajabu. Kwa wakazi wa Mtwara na wenyeji wa njia ya kusini kwa ujumla wanalifahamu hili basi, wanaweza kuhadithia vizuri(the big show,sizinga) watusaidie. Hivyo kiuimara scania ni the best
 
Da tena umenikumbusha Princess Muro: Dar Mwanza aisee ni hatari
Yaani wanatembea hatari. Yutong kwa zinatembea aisee, kwa vyovyote uimara haiwez kufikia scania. Yutong za mwanzo zilikuwa nyanya na nyingi za engine nyuma ziliwapa hasara sana kwanza zilikuwa zinachemsha
 
mnazisema yutong nyanya lakini mibasi ile inaitwa sks bus ( sumry na mbeya express) migari minyanya ile sijawahi ona ukiliona jipya kwa nje utatamani lakini halina mwendo ht kidogo injini nyuma
 
bado zipo, angalia spider,kimotco e.t.c
 
Back
Top Bottom