Pre GE2025 Za ndani kabisa 2025, Fomu ya urais ndani ya CCM ni zaidi ya moja

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
SAFI sana 2025 RAIS MWANAUME TOKA BARA πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸ‡ΉπŸ‡Ώ KWAHERI YA KUONANA 🐸🐸 KIZIWI 🀣🀣🀣
 
Nakubaliana na wewe moja kwa moja.
 
Inatakiwa ifanyike mbinu asichukue fomu kabisa.Akichukua tu,hao wengine waliochukua fomu kuchuana naye watapotea mmoja baada ya mwingine au watashawishiwa ili wajitoe.
 
Hakuna jambo kama hilo hii sio tetesi umejitungia baada ya kupata picha za hizo pikipiki!
Kama mie ningekuwa ndani ya CCM ningekubaliana na hili kwani 2015 JPM wa awamu ya 5 alishindanishwa na wenzake ndani ya chama na akapita hiyu wa sasa hakuwa chaguo la chama bali aliteuliwa na Magufuli amsaidie na alipokufa Katiba ya nchi ikampa ridhaa kushika hatamu.
Kwa hiyo huyu hajawahi kushindanishwa na wengine ndani ya chama bali lilikuwa chaguo la Magufuli kuwa makamu wake tu.
Sasa lazima arudi ashindanishwe na wenzake sio kupenda mtelemko wa dezo kwa kifo cha aliye mteua awali.
After all anaogopa nini wakati yeye ameshapata nafasi ya kuonyesha uwezo wake? Anaweza kujinadi na Royotuwa (stelingi yeye na mzungu) akawaombea kura kwa umahiri wa kucheza filamu (kwi kwi kwi) na kwa ninavyo wajua ccm atapewa kura
 
Kinachonitisha Mimi ni kama vile alivyowahi kunena Jenerali Ulimwengu kuwa alimuogopa mno Mrema kama angefanikiwa kuwa Rais mwaka 1995.Ni kwa sababu akili yake ilikuwa na utata mkubwa sana.
Nami namuogapa sana Mama Samia kwani mengi mabaya yanayotokea hayafuatilii na yale anayoyapata hajali.
Hiyo tabia kwa Kiongozi wa nchi ni hatari kabisa.
 
Kipindi cha pili cha Magufuli hakukuwa na mshindani nafikiri ni Membe aliye tishia tishia akaishia kukimbia sasa huyu naye ni kama yupo second term yake kama ilivyo mazoea sio kanuni wala sheria hana budi kuachiwa amalize bila upinzani wala pingamizi!
 
Kama kila Mtu mtanzania ana haki ya kugombea nafasi yoyote ya kuwaongoza watanzania wenzake ilimradi ana sifa stahiki, haipendezi vyama vya siasa kuweka utaratibu ambao unawanyima wengine fursa ilihali mmoja keshafanya...iwe kwamba mtu akishafanya 5 yrs akitaka tena mingine 5 awe challenged kuanzia kwenye chama chake maana tukitegemea kule apate mserereko kisha awe challenged na vyama pinzani..watanzania hatuwezi pata mtu sahihi sana kwakuwa huyo aliyepo madarakani anakuwa na nafasi kubwa zaidi ya kuamua au kuamuliwa matokeo yawe upande wake...na inaweza kuwa kinyume only if opposition is strong enough au wananchi wakafanya maamuzi ya uhakika..naamini mda wa huyu unamtosha tunamshukuru..ila akitaka kuendelea kikatiba basi hicho kipengele kwenye ccm kitoke ili atleast tuone kama kuna anayeweza kuwa zaidi ya huyu kuliko kusubiri tena hadi 2030.
Ni kwa wema tu sio ubaya.
 
Tatizo ni internal systems za udhibiti pale CDM hazipo vizuri.
Ukiwasikiliza wengi wakiongea it's like wao wanatosha kuchukua utawala wa nchi... Na ikiwa hivyo watawashughulikia vilivyo waliopo upande wa pili! Wrong messaging!
Badala ya kuwasaka viongozi wenye ushawishi wanaokerwa na uwepo wao ndani ya defunct system ya ccm... Wao utaona wanapambana bila malengo wakati huo hata kusimamisha wagombea kwenye nafasi zote nchi nzima hawawezi!

Washaurini wajisogeze chini zaidi kwa wananchi. Nchi hii wale tunaowaona "wajinga" ndo wapiga kura! Ndo maana ccm wapo nao bega kwa bega!
 
Kikulacho ki nguoni kwako. Ukisikia fitina, basi huku Tanganyika ndiyo chuo cha fitina. Watu wanacheka na mtu mchana lkn usiku wanamuua.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ imebidi nicheke aiseee, ila kwa Watanzania izo mambo ya unafiki na kugeukana ni dakika 1 tu.
 

Kama ishu iko ivyo et Jk awe mwenyekiti wa Muda hahaha ngoma imeishia hapo, ila kama iko ivyo basi B Mkubwa atafosi fomu iwe moja, ili kuepuka kumpa JK uenyekiti wa muda.
 
Sasa naanza kukuelewa unapo simamia.
Ni hivi mkuu 'Mfikirishi': kila mara tumewashauri sana hao CHADEMA wafanye kazi na wananchi tokea mashinani/mitaani/vitongojini, n.k., hili siyo jambo geni unalo libuni wewe hapa. Hii tumewashauri sana tokea 2020; maandishi hayo yamo humu humu JF.
Sisi pia tunasikitika ushauri huo haukuzingatiwa kwa kiasi kikubwa; kwa sababu wange fanya hivyo, hali sasa hivi ingekuwa ni tofauti sana na ilivyo.
Lakini sote tunaelewa, pamoja na udhaifu wa uongozi katika maswala kama hayo, tunajuwa jinsi walivyo rubuniwa na kupoteza muda kwenye kiini macho cha "mazungumzo ya maridhiano". Sasa sijui kama wewe hujawahi kuona au kusikia ulaghai huo.
Washaurini wajisogeze chini zaidi kwa wananchi. Nchi hii wale tunaowaona "wajinga" ndo wapiga kura! Ndo maana ccm wapo nao bega kwa bega!
Wewe umeona "CCM wapo bega kwa bega" na wananchi? Wapi huko ulipo wewe na kuona hali hiyo?
Ukiwasikiliza wengi wakiongea it's like wao wanatosha kuchukua utawala wa nchi... Na ikiwa hivyo watawashughulikia vilivyo waliopo upande wa pili! Wrong messaging!
Wewe unavyo vigezo vipi ambavyo unaona CHADEMA hawana kuwawezesha "kuchukuwa utawala wa nchi"? Ni viongozi gani ambao unafikiria wewe wapo nje ya CHADEMA ambao endapo chama hicho kitaachana na uoga wa wageni watawasaidia kuwa na sifa za kuchukuwa nchi?

Hao viongozi ulio nao akilini mwako na kutaka wakubaliwe kuingia CHADEMA, wao hawana uwezo wa kuimarisha au kuunda chama wakatumia uwezo wao huo na kuchukua nchi? Kwa nini wasubiri kukaribishwa ndani ya chama kingine?

Nataka unielewe vizuri. Sipo hapa kuwatetea CHADEMA. Ndani ya chama hicho, kama ilivyo ndani ya vyama vingine vyote, na hasa hasa ndani ya CCM, kote huko kumejaa viongozi 'opportunists' tele. Lakini hasa hasa kinacho kosekana ndani ya CHADEMA ni viongozi wa juu walio na 'commitment' ya dhati kwa maslahi ya nchi hii na wananch wake. Kiongozi anaye weza kuaminiwa kuongoza viongozi wengine, hata hao ma-opprtunists' na kuwapanga vizuri kufanya kazi za wananchi. Kiongozi anaye aminiwa na wananchi.

Lakini, hata tukiacha yote haya, CHADEMA wanatakiwa tu sasa hivi kujenga uwezo wa kuwaondoa CCM madarakani kwa kuwashawishi wananchi kuhusu kutekeleza mambo muhimu machache sana; kama Kupatikana kwa Katiba Mpya. Wakifanikiwa kuwasihi wananchi kuiondoa CCM ambayo inatumia nguvu kubaki na mfumo mbovu. Kazi hiyo inatosha kabisa kwa sasa CHADEMA kuifanya.

Mwisho, nawe nikusihi, uwahimize hao viongozi unao fikiri kuna umuhimu wao kukaribishwa CHADEMA ndipo waweze kuonekana umuhimu walio nao, wajibidishe kufanya shughuli zao huko huko walipo, wasisubiri kukaribishwa kwenye chama kingine.
 
Sasa huyu ni lini aliwahi kushindanishwa na mwenzake?
Au kwa vile mwanamke ndio maana mnataka asishindanishwe?
Kwani urais ni Ndoa bana?
 
Na huo ndio ukweli
 
Duh Kina nani tena hao wanasema ivo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…