Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 28,297
- 68,017
ZAA KWA MAHESABU, SIO UZAE WATOTO WAJE KUFANYWA WATUMWA HUKU DUNIANI!
Anaandika, Robert Heriel
Shahidi!
UTUMWA!
Usukule!
Kutumwa tumwa! Kuvujishwa jasho pasipo malipo, Kulambishwa mavumbi ya viatu pasipo utu. Kuimba pambio katika wimbo wa walao nchi.
Manamba na vibarua wa mashamba, HAO ndio utakaowazaa waje kujambishwa na watoto wa wenzako? Sitaki majibu Yako hapa! Baki nayo.
Zaa Kwa Hesabu zenye jawabu. Sio uzae kama panya, kuzaa watoto wengi Kwa Zama hizi bila Hesabu sio tuu kukosa upendo Bali ni ukatili Kwa watoto wako.
Katika ulimwengu WA teknolojia na Ujuzi na maarifa wingi sio hoja Bali vioja.
Unakuwa na watoto wengi ambao wanatumikishwa kwenye viwanda Kama randa la mbao ndivyo wanavyoranda Randa wakinuka jasho.
Nazaa watoto Saba, najiita kidume kwenye mfumo dume.
Taikon sina shamba wala kiwanja, lakini ninawatoto Saba.
Haipendezi kuzaa watoto waje watumikishwe na kuteswa alafu mzazi bila aibu nawe Kwa ukatili mtoto unamnyonya zaidi mwanao licha yakuwa kipato chake ni duni.
Huo ni ukatili, unyanyasaji na ukosefu wa utu.
Tuzae Kwa Hesabu.
Watoto ambao tunauwezo wa Kuwatunza na kuwaandalia maisha MAZURI na Urithi ili wasiwe Watumwa.
Sio unazaa wapiga Kura wa watoto wa wenzako waluoandaliwa.
Sio anazaa watoto ambao watakuja kuwa vibarua.
Sisemi Kwa ubaya, au kupangia mtu Maisha.
Ila Kwa kweli hakuna kitu kibaya Kwa mzazi mwenye upendo kuona umezaa watoto ambao umewaleta kuja kuteseka na kuteswa na wanadamu wengine.
Mzazi asiye na upendo WA dhati hawezi ona uchungu Kwa mwanaye.
Kwani wengi huzaa Kwa ubinafsi wao tuu. Wakitaka watoto wao waje wawasaidie baadaye lakini hawataki kuwaandaa watoto hao kuishi maisha MAZURI.
Huo ni Ubinafsi na ukatili.
Kama huna uwezo wa kuandaa watoto waishi maisha mazuri, zaa Kwa hesabu. Watoto wachache wanaokutosha.
Jitahidi uangalie Quality zaidi kuliko Quantity.
Sio mtu unajivunia unawatoto wengi lakini watoto uliozaa ni Watumwa, misukule, na watu wanaoteswa na watu wengine.
Zamani watu walizaa watoto wengi Kwa sababu walikuwa wanauwezo wa kuwarithisha mashamba, maboma, na Urithi mwingine.
Lengo jingine na kuleta nguvu kazi katika jamii.
Lakini vipi Zama za leo?
Je tutazaa Kondoo wengi ambao wataongozwa na Simba mmoja?
Au tutazaa Simba mmoja kuongozwa Kondoo wengi?
Au tutazaa Simba wengi kutawala Mbuga?
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam