Zaa kwa mahesabu, sio uzae watoto waje kufanywa Watumwa huku Duniani

Zaa kwa mahesabu, sio uzae watoto waje kufanywa Watumwa huku Duniani

Tatizo linakuja kwa hao hao wawili, je akitokea mmoja akawa shoga? Wewe hauoni tatizo lake litakuwa limesababishwa na ujinga wangu?
Ni pia nina imani hata nikizaa mmoja sitakuwa na plan ya kumfanya huyo huyo mmoja kuja kuwa simba atakayeongoza kundi la ng'ombe msituni.
Bado atakuwa maskini na mwenye magonjwa kibao
Kwamba wewe ni mgonjwa na unaogopa utamuambukiza?
 
Sio tu kuzaa watoto wengi mimi kwangu hata kuzaa kwenyewe tu sitamani,.
Dunia na ulimwengu wa sasa sio salama tena kwa binadamu sanasana watoto sanasana watoto wa kike na wakiume,.
Mimi kwa upande wangu ni bora ni teseke kwa hali yeyote ile nipambane kwa namna yeyote na ikitokea nikafa basi nife mwenyewe kuliko kufa na kukiacha kizazi changu kiendelee na mambo kama haya ya kwangu,.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Mkuu ujumbe umeuweka kihisia sana
 
Wewe Robert achana na sisi.
Fahari ya maskini ni watoto.
Utajiri wa maskini ni watoto.

😊😊😊
Kama mnafurahia wakitumikishwa na kufanywa misukule kwenye maviwanda, mashamba boy, wavuja jasho, na aina zote za udhalili Sawa. Mimi sina neno.

Ila ukishakuwa Mzee alafu ukaona Kwa watoto wako 10 wote wanateswa utakumbuka hii post
 
Kwenye hao kumi.
Lazima watatokea wakubutua kombolela.
Si wote watakuwa hivyo.
 
Nisaidie hapo taycon ,si wanasemaga ukiua mtu ni dhambi? Pia jua tu mamaye akijua huna bahati she'll kill yoh

Kuna watu ukiwaua sio dhambi.
Ila kwa serikali ni kosa kisheria.

Mama yake kabla sijamuoa anajua mumewe ni mtu wa namna gani.

Mimi sio Wale wakuvumilia mambo ya kipuuzi hasa yaliyo ndani ya uwezo wangu na ndani ya familia yangu
 
Nchi zetu hizi za kifala, kuzaa zaa tu bila kuwa na mikakati juu ya unaowaleta duniani ni ufala...

Ndio unaona sasa vilio vimetawala kama vya bima za afya, ada za shule(ingawaje kiasi zimeondolewa) n.k
 
Nitazalisha hadi mbegu zikauke..kila mtoto na mama yake, mama zao watajua wenyewe huko, nitazaa na wanawake wanaoweza kulea wenyewe, sitaki stress hata kidogo....

...alisikika jamaa wa hovyo hovyo akinena!!
 
🤣🤣

Watu wa hivi ni wabinafsi alafu hawana Upendo WA dhati.
Ni hatari kwenye jamii.
 
Katika kitu nimekataa kukubaliana nacho ni hichi, uzae mtoto bila kuwa na mipango thabiti ya kumlea, uje ujipe moyo kila mtoto anakuja na sahani yake, hapana kwa kweli..!

😊😊
Sahani zipo nyingi Sana.
Tatizo nyingi Kati ya hizo sahani zipo kwenye Meza ya usukule na utumwa
 
Mimi hawa wawili wanatosha ,Kuna jamaa mmoja hivi anao wanne, hana shamba , kapanga nyumba, mke wake ni house wife, unene sio afya lakini jamaa hata kamwili kuja hakuna na yuko kazini tena serikalini zaidi ya miaka kumi , ameajiriwa ndio lakini ajira mbuzi ndio maana ana mahasira muda wote na anahangaika na maushirikina ili apate ubosi wakati Hana connection
Atatoa mtoto wake kafara maana ndo za wabongo wengi siku hizi[emoji848]
 
Kuna watu ukiwaua sio dhambi.
Ila kwa serikali ni kosa kisheria.

Mama yake kabla sijamuoa anajua mumewe ni mtu wa namna gani.

Mimi sio Wale wakuvumilia mambo ya kipuuzi hasa yaliyo ndani ya uwezo wangu na ndani ya familia yangu
"Kuna watu ukiwaua sio dhambi.
Ila kwa serikali ni kosa kisheria" ila Mungu huyo huyo anatuhimiza tuitii mamlaka tycoon. Pia Mungu si anasema hutakiwi kuua, jukumu la kuua ni la serikali/mamlaka pekee au?kaufafanuzi hapa
 
Mimi hawa wawili wanatosha ,Kuna jamaa mmoja hivi anao wanne, hana shamba , kapanga nyumba, mke wake ni house wife, unene sio afya lakini jamaa hata kamwili kuja hakuna na yuko kazini tena serikalini zaidi ya miaka kumi , ameajiriwa ndio lakini ajira mbuzi ndio maana ana mahasira muda wote na anahangaika na maushirikina ili apate ubosi wakati Hana connection
Baadae aje kujisifu kweny vibanda vya kahawa " watoto wangu nimewalelea kwa tabu" kumbe tabu kazitafuta mwenyewe
 
"Kuna watu ukiwaua sio dhambi.
Ila kwa serikali ni kosa kisheria" ila Mungu huyo huyo anatuhimiza tuitii mamlaka tycoon. Pia Mungu si anasema hutakiwi kuua, jukumu la kuua ni la serikali/mamlaka pekee au?kaufafanuzi hapa

Mungu anatutaka tuitii mamlaka inayotoka kwake(Kwa Mungu) na Dalili moja wapo ya mamlaka inayotoka Kwa Mungu ni kutenda haki na kufuata sheria za Mungu.

Zaidi ya hapo sina nyongeza
 
Mungu anatutaka tuitii mamlaka inayotoka kwake(Kwa Mungu) na Dalili moja wapo ya mamlaka inayotoka Kwa Mungu ni kutenda haki na kufuata sheria za Mungu.

Zaidi ya hapo sina nyongeza
Nimekuelewa tycoon!asante sana kuhani wa hekalu jeusi,kitukuu cha kuhani Melkizedeki
 
Back
Top Bottom