TANZIA Zahara wa Afrika Kusini afariki Dunia. Imedaiwa aliwekewa Sumu na Ndugu yake katika Sherehe ya Baada ya Mahari

TANZIA Zahara wa Afrika Kusini afariki Dunia. Imedaiwa aliwekewa Sumu na Ndugu yake katika Sherehe ya Baada ya Mahari

Sasa kwanini useme wapiganiji wa uchawi ndo wachawi ?
Hapa pia usiponielewa basi kila Mtu aamini anavyoamini [emoji116]

2 WAKORINTHO 11:14-15.

Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.

Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Zahara alilishwa sumu ya kichawi
Ma-dr Hawa ni wa pekee,wameona uchawi kwa vipimo vya kisayansi,. Mungu amrehemu dada huyu,sauti yake nzuri as if ana miaka 17,



Naendelea kuamini south Africa Wana roho mbaya, ni baada ya kusoma nyuzi mbili za Hawa jamaa ndani ya wiki Moja,,,

Ntawahusia wanangu hata maisha yakiwagonga wasiende south
 
Nimesoma kwny mwananchi online..kwamba alikua mlevi mnooo..na alishapewa onyo kuhusu pombe..maybe alipitia depression akaamua kuwa mlevi..ila wasanii wana maisha ya stress sana behind the camera...alijisemea Vanessa Mdee kuliko kuja kujiingiza kwny pombe na madawa kupoteza mawazo bora a quit the game....
 
Habari ya kwanza niliyokutana nayo leo kwenye mitandao ya kijamii inahusu kifo cha mwanadada Mwimbaji Bulelwa Makutukana ( Zahara) kilicho tokea jana huko Johanesburg baada ya kuugua ini kwa muda mfupi.

Zahara amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 35.

Binafsi nitamkumbuka sana Zahara kwa wimbo wake "Loliwe".

Wimbo huu uliwahi kunisaidia katika nyakati ngumu.

To be honest with you. Taarifa ya kifo cha Zahara imefanya nafsi yangu iwe troubled kama nafsi ya Yesu ilivyokuwa troubled alipopewa taarifa za kifo cha rafiki yake Lazaro.

Asante Mungu kwa kuipa dunia zawadi ya kipaji kikubwa kama Zahara.


LALA NGOXOLO ZAHARA.

Update: Inadaiwa chanzo cha kifo chake ni multiple organ failure iliyo sababishwa na yeye kulishwa sumu na mmoja kati ya wanafamilia mara baada ya Zahara kutolewa mahari..

Taarifa nyingine inadai kwamba Zahara alilishwa sumu ya kichawi " muthi" kwenye chakula wakati ya sherehe ya kulipa mahari yake.

Duh kwamba kuna mwanafamilia alichukia kuona Zahara katolewa mahari? Just like that? Ooh please God protect your children from evil.
---

View attachment 2839995
Tasnia ya Burudani nchini humo imepata pigo lingine kutokana taarifa za kifo cha Mwimbaji Bulelwa Mkutukana maarufu Zahara (35) baada ya vifo vya AKA Februari 10, na CostaTitch, Machi 11, 2023.

Taarifa zimeeleza kuwa Kifo cha Zahara aliyetamba na nyimbo mbalimbali zikiwemo Loliwe' na Phendula kimetokea katika Hospitalini Jijini Johannesburg alikokuwa akipatiwa matibabu kutokana na kuugua maradhi ya ini kwa takriban Wiki 2. Pia kuna taarifa kuwa maradhi hayo yalisababishwa na sumu aliyowekewa na mmoja wa Mwanafamilia katika Sherehe ya baada ya kutolewa Mahari.

Vyombo vya Habari nchi humo vimeripoti kuwa siku chache kabla ya Kifo cha Zahara, Dada zake walichukua Kadi zake za Benki na kwenda 'Shopping' huku ndugu yao akipigania uhai wake Hospitali.

Enzi za Uhai wake Zahara aliwahi kuja Tanzania Oktoba 2018 ambapo alitoa burudani Jukwaa moja na Juliana Kanyomozi wa Uganda, na LadyJayDee katika Tamasha la Vocals Night liliondaliwa na Lady JayDee.
Kunywa kangweso kupita kiasi ndio imechukua maisha yake na ini kufeli hakuna kurogwa
 
Mwezi wa Desemba ni mwezi wa mbaya sana kuliko miezi yote. Sifahamu kwa nini, yaani ni vifo na ajali, Tuwe makini .
Hii habari imenisikitisha.RIP.
 
Back
Top Bottom