Intro: Let me talk to this girl meeen....
....aaahhaaa, yeeaah
Naamini unanipenda sio kwa vile mi rapper, ni jinsi navyokupa vitu roho inataka/
Una kila nachohitaji, una kila nachotaka wengi wamehustle juu yako wamevapa/
You know what, baby girl you are so lucky/
Jinsi navyowakwepa wanashikana mashati/
Mipango ishakaa sawa, usipoteze wakati/
Usicheze na midoli hao midoli hawang'ati/
Njoo ucheze nami sema nami kila wakati/
Mi nna future yako, we una future yangu/
Mi nina siri zako na we unatunza zangu/
Basi mshumaa kwenye upepo usiweke makusudi/
Baki innocent usijivike ugaidi, nitasema kwa upole sitosema kiukaidi/
Mpakaa nimefika level hizi baby ujue hii ni serious/
Hatuwezi kutengana kama bob na the wailors/
Kuwa maadui kama pac na notorious/
Siwezi kusema najua kila kitu , Wala huwezi kusema unajua kila kitu/
Kama kupenda ni kasoro sitaki kukamilika tena/
Wanafki wakileta ikibidi ntakua mkatili sana/
Siku hizi ni ngumu kila mtu kuaminika so sikuuzii maneno mi ni mtu wa vitendo/
Rapper wa mwisho wa ukweli, mkali asiye na skendo/
Pingu zitafungwa baby haitakua tena magendo/
Ikiwa hard time au good time zote kubali/
Madogy style, wima mikunjo na chali nipo tayari/
Makini Kama style uandishi na vocal zangu/
Napigana kuhakikishaa milele unabaki wangu/