Zaidi ya %80 ya watanzania hawajafika chuo kikuu?

Swahili_Patriot

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2018
Posts
358
Reaction score
831
Tukitumia evidence ya maoni ya WATANZANIA kwenye threads za Jamii forums na social platforms nyingine kama Facebook, IG nk, ni dhahiri kuwa Tanzania kama taifa, inabidi tubadilishiwe mfumo wetu wa elimu na tununue nguvu kazi kutoka nchi zilizopiga hatua kielimu waje kufundisha kwenye shule zetu. Kama mtamzania, inanouma kuona jinsi tunavyoongozwa alafu tunachukulia poa tu. Hivi kweli uwezo wetu wa kuchagua viongozi upo dhofulhali namna hii??

Cha ajabu ukijaribu kufuatilia maoni yetu kwenye pg za mitandao ya jamii ndio shiiidaaaah. Kwanini tunachukulia mzaha kuandika uharo kwenye vitu serious?? Kweli uwezo wetu wa kufikiria umeishia hivyo kirahisi rasihi namna hii?? Hivi hatuoni kwenye nchi jirani walivyo serious kwenye vitu serious??? Tutaendelea kupigwa hadi lini??

Alafu kipindi cha uchaguzi tunapewa f5 tano zilizotolana n ufisadi na tunaziuza kura zetu kirahiiisi?? Tukipigwa tunaishia kuandika pumba n jambo linapita!! Kama nchi tunahitaji wasomi, maana wasomi wetu mwenyewe vilaza. Ilimradi mtu anajua kuona n kuandika kwetu bomba tu. Taifa litauzwa hili. We zetu Kenya zaidi ya %80 za kodi zinaenda ulipa deni la taifa, na bado sisi vilaza fc. Dah, kweli ngombe waaskini hazai😭😭😭
 
Harafu Mama anapojenga vyuo Vikuu Mikoa ambayo hakuna na kufungua matawi Kuna wapumbavu wanadai Vyuo vimetosha.

Kwa jinsi walivyobobea kwenye upumbavu wanaahindwa kujua kwamba Tanznaia inazidiwa na Nchi jirani zote kasoro Burundi tuu kwenye mambo ya Elimu ya Juu.

Hongera Serikali ya Mama Kwa kuamua kujenga Vyuo Vikuu na matawi kwenye Mikoa 17 ambayo haikuwahi kuwa na Chuo Kikuu.
 
Watanzania wachache wanatumia mitandao ya kijamii.
Hiyo unayosema tuangalie wenzetu wanavyojibu nchi jirani. Jibu lako ni elimu yetu ni duni saaaaaana
 
Sio tuu duni Bali waliofikiwa ni wachache sana kama alivyosema mtoa mada.

Mama anajenga Vyuo Vikuu 17 vipya Kila Mkoa Tanzania.
 
Watanzania mind zao zipo kwa Nyerere labda tusubiri kizazi Cha Nyerere kipotee, hapo tutapata wapinzani wa kweli wa kuitoa CCm madarakani
 
Tukitumia evidence ya maoni ya WATANZANIA kwenye threads za Jamii forums na social platforms nyingine kama Facebook, IG nk, ni dhahiri kuwa Tanzania kama taifa, inabidi tubadilishiwe mfumo wetu wa elimu na tununue nguvu kazi kutoka nchi zilizopiga hatua kielimu waje kufundisha kwenye shule zetu. Kama mtamzania, inanouma kuona jinsi tunavyoongozwa alafu tunachukulia poa tu. Hivi kweli uwezo wetu wa kuchagua viongozi upo dhofulhali namna hii??
Hoja yako ni nini? kufika chuo kikuu kwa maana ya hata kupa tembelea tu au kufikia elimu ya chuo kikuu?
 
Tukitumia evidence ya maoni ya WATANZANIA kwenye threads za Jamii forums na social platforms nyingine kama Facebook, IG nk, ni dhahiri kuwa Tanzania kama taifa, inabidi tubadilishiwe mfumo wetu wa elimu na tununue nguvu kazi kutoka nchi zilizopiga hatua kielimu waje kufundisha kwenye shule zetu. Kama mtamzania, inanouma kuona jinsi tunavyoongozwa alafu tunachukulia poa tu. Hivi kweli uwezo wetu wa kuchagua viongozi upo dhofulhali namna hii??

Cha ajabu ukijaribu kufuatilia maoni yetu kwenye pg za mitandao ya jamii ndio shiiidaaaah. Kwanini tunachukulia mzaha kuandika uharo kwenye vitu serious?? Kweli uwezo wetu wa kufikiria umeishia hivyo kirahisi rasihi namna hii?? Hivi hatuoni kwenye nchi jirani walivyo serious kwenye vitu serious??? Tutaendelea kupigwa hadi lini??

Alafu kipindi cha uchaguzi tunapewa f5 tano zilizotolana n ufisadi na tunaziuza kura zetu kirahiiisi?? Tukipigwa tunaishia kuandika pumba n jambo linapita!! Kama nchi tunahitaji wasomi, maana wasomi wetu mwenyewe vilaza. Ilimradi mtu anajua kuona n kuandika kwetu bomba tu. Taifa litauzwa hili. We zetu Kenya zaidi ya %80 za kodi zinaenda ulipa deni la taifa, na bado sisi vilaza fc. Dah, kweli ngombe waaskini hazai😭😭😭
F.A.C.T
 
Harafu Mama anapojenga vyuo Vikuu Mikoa ambayo hakuna na kufungua matawi Kuna wapumbavu wanadai Vyuo vimetosha.

Kwa jinsi walivyobobea kwenye upumbavu wanaahindwa kujua kwamba Tanznaia inazidiwa na Nchi jirani zote kasoro Burundi tuu kwenye mambo ya Elimu ya Juu.

Hongera Serikali ya Mama Kwa kuamua kujenga Vyuo Vikuu na matawi kwenye Mikoa 17 ambayo haikuwahi kuwa na Chuo Kikuu.
Elimu haianzii chuo kikuu, lazima ujenge misingi imara kwenye elimu ya msingi kama inavyoitwa. Bahati mbaya tumejijengea dhana kuwa shule za msingi ni sehemu ya kucheza juhudi tunatakiwa tuzifanye kuanzia sekondari, mtindo huu ndio umedhoofisha elimu yetu.
 
Toa ufala wako hapa,kama Elimu ya shule ya msingi inatosheleza kelele za nini? Literacy ya Nchi Kwa Elimu ya msingi ni zaidi ya 80% Kwa nini haiwaletei Mabadiliko stahili?
 
Watafikaje wakati kuna kikwazo cha mitihani ya form four na six? Hii mitihani ni noma sana, ukichujwa hapo elimu ya chuo kikuu utaisikia kwa wengine
 
Kwa asiekuelewa hapo kwenye heading yako anaweza kufikiri umekosea,ila kiuhalisia hiyo %80 ni kiswahili na kizungu ni 80%,hongera mkuu....
 
Elimu yetu inatia mashaka kila kukicha, mfano ni kwa huyu aliyeanzisha mada bila shaka na mhitimu wa chuo kikuu.
 
Haiwezekani. Mbona heading ya uzi wake na content ya uzi wake haviendani. Hawezi kuwa University graduate.
Kila hoja ni sahihi kulingana n mawazo ya mtoa hoja. Ila uhalinisia nibkwamba, kuanzia darasa la4 hadi chuo ckusomea tz. So uwezo wangu wa kuconverse in swahili ni duni kuliko English. Japo ninaijua lugha yetu, ila mawazo ya mpangilio wa maneno cku zote huniangusha. Kama utanielewa, haya ni madhara ya direct translation of ideas from English to swahili
 
Back
Top Bottom