Zaidi ya Degree 100 zimefutwa baada ya vyuo 15 kufanya kazi kinyume na Sheria Kenya

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
378
Reaction score
766
Nimewaza tu kwa sauti kwamba mtu umepigika zako miaka mitatu ya kutafuta digrii alafu unakuja kufutiwa kwamba ni feki.​

===================================
Tume ya Elimu ya Vyuo Vikuu imetaja vyuo 15 vinavyofanya kazi kinyume cha sheria nchini Kenya na kuwaonya Wakenya kwamba vyeti vya kimasomo vinavyotolewa na vyuo hivyo vitachukuliwa kuwa vya uongo 'fake'.​

Zaidi ya hayo, Tume hiyo imetaja ni vyuo 79 tu vilivyothibitishwa kufanya kazi nchini Kenya, vikijumuisha vyuo vikuu vya umma na binafsi, vyuo vya vyuo vikuu vya binafsi, na taasisi zilizo na barua za Mamlaka ya Mpito.

Hivyo basi, digrii 100 zilifutwa na maafisa wa vyuo vikuu walikamatwa. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na tume hiyo imesema "Ili kuepuka mkanganyiko, taasisi yoyote inayofanya kazi kama chuo kikuu au kutoa digrii na ambayo haionekani kwenye orodha ya taasisi zilizothibitishwa na Tume haitambuliki kisheria na sifa zake za digrii hazitakubalika nchini Kenya,"

Vyuo vilivyofungiwa ni; Eldoret Bible College, Al-Munawwarah College, Grace Life Bible College, Africa Theological Seminary, Kenya Anglican University, The East African University Bradgate International University, Eldoret Bible College, Regions Beyond Ministry Bible College, Baraton College, The Africa Talent University, Breakthrough Bible College, Theophilus Theological College, Northwestern Christian University, Logos University, Harvest Land University na Word of Faith Bible College.
 
Karibu 90% ya vyuo hapo naona ni vyuo vya kanisa.

My take.
Matapeli wengi wamejificha kanisani kwa mgongo wa kujifanya wanaumtangaza Yesu. Kuwa makini sana na fursa yoyote inayeletwa mbele yako kwa kivuli cha kanisa.
 
Back
Top Bottom