Zaidi ya KM 2000 za barabara kuanza kujengwa kwa mtindo wa EPC +F. Serikali yasema hazitalipiwa Tozo

Zaidi ya KM 2000 za barabara kuanza kujengwa kwa mtindo wa EPC +F. Serikali yasema hazitalipiwa Tozo

Haijawahi nunuliwa hiyo bei zaidi ya maigizo ya kuficha aibu,ndio tulisikia kwamba watu wakaoneshe mashamba walipolima korosho, mwisho wa siku iliozea kwenye Maghala ya serikali ikamwagwa maana wanunuzi waligoma [emoji23][emoji23]
Wedo unanikumbusha mbali sana,mtaji wangu wa kangomba umefia mikononi mwa magu nilipo pokonywa korosho zangu heti sina shamba lakini magu simtomsahau ila na msamehe bule
 
Kama kawaida, tu-sifa twa kuokoteza. Sasa hapo historia ni gani? Barabara au EPC+F?

Sikilizeni nyie chawa. Huyo mama yenu hamna kitu anafanya. Anarukaruka tuu hatumwelewi huku. Barabara nayo ni kitu cha kumsifia? Hamna jipya.
Utajuaje umuhimu wa barabara hali yakuwa hapo ulipo utoki uko kama bikoni ya mjerumani mpaka sasa bikoni hizo zinadhani bado mtawala ni mjerumani [emoji14][emoji14][emoji14][emoji14][emoji14]
 
Hi nimeilewa sana, sana hizo barabara nimezipita kwakweli kimapinduzi makubwa sana, hongera mama Samia, najua enzi za mwenda zake huu mzigo ungepelekwa Chato huko
 
Hatupaswi kuwafurahia sana wachina..
Tuweke taratibu Za wazi zaidi ili kuvutia wakandarasi bora toka ktk mataifa mengine makubwa Japan,Korea na Kwingineko..

Zipo tuhuma nyingi juu ya Sifa za makampuni ya kichina kwenye Utoaji Rushwa ili kupata miradi (They are very aggressive ktk hili) hili si la kubezwa..Na wanapotoa rushwa hufanya madudu ktk quality delivery..
Wachina ndio Wakandarasi Bora Kwa Sasa Duniani
 
Kwa mara ya Kwanza baada ya Uhuru Tanzania imepata Rais Samia apewe maua yake.

Serikali ya Rais Samia imeandika Historia nyingine ya ubunifu kwa kusaini kuanza ujenzi wa barabara za kuu za lami kwenye mikoa 13 kwa pamoja zenye jumla ya urefu wa KM 2035 kwa mtindo wa EPC+ F (Engineering, Procurement, Construction and Finance) kwa gharama ya Tsh.Tilioni 3.8 ambapo miradi inatarajiwa Kukamilika ndani ya miaka 4 (2023-2027).

Akizungumza wakati wa kushuhudia kutiwa saini kwa mikataba hiyo Jijini Dodoma, Waziri wa Ujenzi Prof. Mbarawa amesema kwamba, barabara hizo hazitokuwa za kulipia tozo kama wapotoshaji wanavyosema. Ikumbukwe hii haijawahi tokea toka Uhuru, walinda legacy mnafundishwa kazi.

My Take
Samia anawaonesha kwamba Private Sector inalipa kuliko Ujamaa mbuzi ambao baadhi ya watu wasiojielewa wanakumbatia.

Ndio maana hata kwenye Bandari anataka awafundishe namna ya kutumia rasilimali kwa manufaa ya watu badala ya kuhubiri propaganda za Uzalendo mbuzi na umaskini over years.

Hongera sana Mh. Rais, na Waziri wa Mbarawa Kwa Ubunifu,Historia itaandika jina lako kwa wino Mwekundu.

=====

MIRADI YA BARABARA ILIYOSAINIWA KWA UTARATIBU WA EPC + F

i) Barabara ya Kidatu – Ifakara – Lupiro – Malinyi – Kilosa Kwa Mpepo – Londo – Lumecha/Songea (km 435.8) inapita katika mikoa ya Morogoro na Ruvuma na inapita pia katika Majimbo ya Kilombelo, Ulanga, Malinyi na Namtumbo;

ii) Barabara ya Arusha – Kibaya – Kongwa (km 453.42) inapita katika Mikoa ya Arusha, Manyara na Dodoma na inapita katika Majimbo ya Arusha Mjini, Arumeru Magharibi, Simanjiro, Kiteto na Kongwa;

iii) Barabara ya Handeni – Kiberashi – Kijungu – Kibaya – Njoro – Olboroti – Mrijo Chini – Dalai – Bicha – Chambolo – Chemba – Kwa Mtoro – Singida (km 384.33) inapita katika Mikoa ya Tanga, Manyara, Dodoma na Singida na inapita katika Majimbo ya Kilindi, Chemba, Kiteto, Singida Mashariki na Iramba Mashariki;

iv) Barabara ya Igawa – Songwe – Tunduma (njia nne) (km 237.9) inapita katika Mikoa ya Mbeya na Songwe na inapita katika Majimbo ya Mbarali, Mbeya Vijijini, Mbeya Mjini, Mbozi, Vwawa na Tunduma;

v) Barabara ya Masasi – Nachingwea – Liwale (km 175) inapita katika Mikoa ya Lindi na Mtwara na inapita katika Majimbo ya Masasi, Nachingwea na Liwale;

vi) Barabara ya Karatu – Mbulu – Haydom – Sibiti River – Lalago – Maswa (km 339) inapita katika Mikoa ya Manyara, Simiyu, Singida na Arusha na inapita katika Majimbo ya Mbulu Mjini, Mbulu Vijijini, Karatu, Iramba Mashariki, Meatu, Maswa Mashariki na Kisesa; na

vii) Barabara ya Mafinga – Mtwango – Mgololo (km 81) inapita katika Mkoa wa Iringa na inapita katika Majimbo ya Mufindi Kusini na Mafinga.
Barabara ya Pugu, Majohe, Viwege, Njia nne, Mbondole hadi Mwembeni ipo? Kama haipo huo mradi kwangu hauna maana
 
Siyo kweli.
1992 ilijengwa na Patzansik Put
2002 ilivunjwa na kujengwa sikumbuki ni kampuni gani ile possibly ilikuwa ukarabati fulani mkubwa
2012 ilijengwa kuanzia Iringa kama sijakosea sana
 
Utajuaje umuhimu wa barabara hali yakuwa hapo ulipo utoki uko kama bikoni ya mjerumani mpaka sasa bikoni hizo zinadhani bado mtawala ni mjerumani [emoji14][emoji14][emoji14][emoji14][emoji14]
Yaa, uko sahihi. Ntajuaje umhimu wa barabara ikiwa kila nikitoka nakutana na maelfu ya km za barabara zilishajengwa huko. Huyo mama yenu anakipi kipya katika barabara kianchowafanya muje kutuimbia mapambio hapa. Ni hicho kigezo cha barabara hazijengwi kwa tozo?! Rubish🚮
 
Huyu mama hesabu na yeye ni mbingu na ardhi 1km 2b
Sasa limekuja suala la ujenzi wa barabara kwa kutumia utaratibu wa EPC + F. Wanavyousifia utaratibu huo ni kama nchi imevumbua muujiza mkubwa utakaomaliza matatizo yote ya ujenzi wa barabara, na kama vile tawala nyingine zote zilizotangulia zilikosa ubunifu.

Ukweli ni kwamba EPC + F, hakuna utawala ambao ungeshindwa kujenga barabara kwa kufuata utaratibu huo kama ungeonekana ni rahisi na wenye tija.

Kwa mchumi mzuri, siyo mchumi wa makaratasi, ujenzi wa barabara kwa utaratibu huu, ndiyo aghali kuliko utaratibu mwingine wowote ambao nchi imewahi kutumia.

Kwa wasioelewa, utaratibu huu wa EPC + F, mjenzi anajenga barabara kwa kutumua pesa yake, halafu Serikali itakuwa inamlipa yule mjenzi taratibu kwa kiwango kilichokubaliwa.

Mjenzi wa barabara anapata wapi pesa?
Mjenzi wa barabara anachukua pesa toka kwenye mabenki na taasisi mbalimbali za fedha.

Mjenzi wa barabara anazichukua pesa toka benki kwa utaratibu gani?
Mjenzi anachukua pesa benki kwa njia ya mkopo. Mkopo ni lazima uwe na riba maana mkopeshaji naye anatafuta faida.

Mjenzi kwa nini akubali kutujengea barabara halafu alipwe taratibu?
Mjenzi ni mfanyabiashara. Anatafuta faida. Hivyo nchi italazimika kumlipa mjenzi kwa kiwango ambacho mjenzi lazima apate faida.

Mjenzi atapataje faida?
Lazima atahakikisha nchi inalipa kufidia riba ya benki alikochujua pesa, plus faida ya kwake yeye mjenzi. Na tukichelewesha, tutalipa na penalty.

Kwa hiyo utaratibu huu wa EPC + F, utatufanya tujenge barabara zetu kwa gharama kubwa kuliko kipindi chochote kile. Kwa wasioupendelea utaratibu huu wangeweza kuuliza, kwa nini ukalipe riba kwa taasisi mbili, yaani kwa benki na mjenzi, wakati kuna uwezekano wa kukopa benki moja kwa moja, ukaokoa riba ambayo ungemlipa mjenzi?

Wakati Waziri Mbarawa akiusifia utaratibu huu kama vile amegundua sayari mpya, hakutoa mchanganuo wowote. Kwa mfano alitakiwa kusema:
1) kwa wakati huu ambao barabara zimekuwa zinajengwa kwa taratibu tofauti na EPC + F, kilometer 1 ya barabara ya lami, gharama ya ujenzi ni sh. ngapi?
2) Kwenye utaratibu huu wa EPC +F, kilometer 1 ya barabara ya lami, itagharimu kiasi gani?

Mkopo siyo pesa ya bure. Na wala huwezi kujisifia kuwa umegundua mbinu mpya ya kukopa. Mateso ya mkopo utayajua wakati wa ulipaji. Uganda wanalalamika sasa hivi, maana kwa mara ya kwanza mwaka huu wa fedha, karibia 40% ya bajeti yao yote itakuwa inagharamia kulipa madeni. Na sisi kwa sababu ni watu ambao uwezo wetu unaishia kushangilia na kupongeza, tunaelekea huko huko. Ifahamike tuna mikopo ya kugharamia miradi kama SGR, bwawa la Mwalimu Nyerere, daraja la Busisi, mikopo ya miaka mingi ya huko nyuma, sasa inakuja na hii ya EPC + F, na kutakuwa na mikopo kuziba pengo la bajeti kila mwaka. Hatuwezi kukwepa kukopa, lakini mwenye weledi anakopa kwa umakini, na siyo kurundika mikopo mingi kwa wakati mmoja kwa sababu tu amepatikana wa kukukopesha.

Nchi nyingi zinazotumia utaratibu wa EPC + F, zinatumia wakandarasi wa ndani. Kwao, hata kama barabara zitajengwa kwa gharama kubwa, mabenki yanayokuwa yamenufaika kutokana na riba ni ya nchini mwao. Wajenzi walionufaika kutokana na riba ni wa nchini mwao. Kwa hiyo hela inakuwa imetoka Serikalini imeenda kwa watu wao. Sisi hela itatoka Serikalini kwenda kwenye mabenki ya nje, pesa itatoka Serikalini kwenda kwa makampuni ya ujenzi ya nje.
 
Ujinga
 
Back
Top Bottom