Zaidi ya KM 2000 za barabara kuanza kujengwa kwa mtindo wa EPC +F. Serikali yasema hazitalipiwa Tozo

Kwahiyo Kanda ya Ziwa baada ya JPM Kufa tuna adhibiwa eti?
Nyie wakati mnaadhibu wenzenu mlijua ni raha si ndio?

Pili huko Kanda ya Ziwa Kuna miradi kibao tuu inaendelea ya Barabara ila wewe Kwa kuwa umezoea umbea huwezi jua.
 
Tatizo hujishughulishi na takwimu, unaongozwa na mihemuko kuliko weledi.

Nenda TANROADS wakupe takwimu.

Kama huwezi, chukua haya yakusaidie:

Wakati wa utawala wa Kikwete zilijengwa kilometa 12,000 barabara za lami. Barabara ndefu kabisa wakati wa utawala wake:
1) Dodoma-Tinde-Kahama-mpakani na Rwanda (zaidi ya kilometa 700)
2) Dodoma -Iringa (kilometer 264)
3) Tunduma-Sumbawanga-Mpanda (zaidi ya kilometa 400)
4) Songea=Tunduru-Masasi (zaidi ya kilometa 400)
5) Tinde = Mwanza (zaidi ya kilometa 200)
6) Mwanza = Geita - Bukoba- mpakani na Uganda (zaidi ya kilometa 400)
7) Dar - Iringa - Mafinga upgrade (zaidi ya 600km)
8) Chalinze -Korogwe-Moshi-Arusha upgrade (zaidi ya 500km)
9) Manyoni -Itigi-Tabora-Urambo (zaidi ya 300km)
10) Bwanga-Ngara-Kabanga-mpakani na Burundi (zaidi ya 300km)
Na nyingine nyingi za kilometa chini ya 300.

Nimekuwekea hizo chache ndefu ili ikusaidie isiye na kumbukumbu.

Tatizo mnaweka mihemko mbele, weledi mnaweka makabatini.

Wakati wa awamu ya Magufuli barabara za lami zimejengwa 2,800km.

Katika tawala zote, kilometer nyingi za barabara za lami zimejengwa wakati wa Kikwete.

Ungekuwa mtu wa kutafakari, ungejiuliza, hayo matengenezo ya kilometa zaidi ya 23,000 ya barabara kuu yalikuwa yanafanyika wapi kama hizo barabara hazikuwa tayari zimejengwa?

Kwanza ufahamu kuwa hakuna mkoa mpaka sasa hivi ambao haufikiki kwa barabara ya lami. Lakini kuna mikoa michache ambayo hazina barabara za kukatisha kuufikia mkoa jirani, mpaka upitie mkoa mwingine. Kwa mfano, una uwezo wa kutoka Dar mpaka Songea kwa barabara za lami 2, yaani Dar-Masasi-Songea; na Dar-Iringa-Songea. Lakini hakuna barabara ya lami ya kukatisha kutoka Mikumi direct to Songea. Vivyo hivyo kwa mikoa kama Tanga to Dodoma. Lakini una uwezo wa kufika Dodoma toka Tanga kwa barabara ya lami. Kabla ya utawala wa Kikwete kuna mikoa ambayo ilikuwa hakuna hata barabara moja ya lami ya kufikia makao makuu ya mkoa, hata kwa kuzunguka.
 
Wewe kweli ni mzalendo uchwara.
Mbona mleta Mada ameweka na kirefu chake .
Soma ujumbe uumalize ndiyo uanze kucoment.
 
Matusi hayatawasaidia ,mtu wenu si aliwajengea airport ya Chato nenda mkaduke ndio kulikuwa kipaombele 😁😁

Ndio maana Huwa nasema hakuna kitu Cha maana aliwasaidia ni alikuwa mjinga,pesa bil.725 za daraja zingetosha kujenga Barabara zalami Lake zone yote na Jiji la Mwanza lote ila ndio hivyo tatizo ni kichwa kikubwa akili kisoda..

Sasa Iko hivi mama ni Muingwana wala usijari amewafikia hata huko..

Hapo Mwanza Jiji na Kahama Kuna tactic zaidi ya km 27 za lami mtaani mtapata na Kahama ni zaidi ya km 20..

Kuhusu Barabara Kubwa za Mikoa Kagera pekee Kuna miradi 4 inaendelea,Mara Kuna miradi 3 na Mwanza Kuna mradi 1..

Harafu usikariri sio lazima Kila Barabara ijengwe Kwa EPC+F,hii model ni Kwa Barabara za kiuchumi tuu,nyie mnajengewa Kwa utaratibu wa kawaida 👇
 
Tena dhahabu Nyekundu,wakati Jiwe anatumia mtutu kuongoza na visingizio kibao Samia anakimbiza mwizi kimya kimya..

Toka Nchi Imepata Uhuru Sasa ndio tumepata Rais .

Ngoja ndugu zake nyerere wa jamiiforum wakuijie na hilo jibu la kupata uhuru 😁 yani huwaambii kitu kuhusu nyerere

Niseme tu, mama anaupiga sana, na tumtakie kila la heri

Mwisho kabisa,SSH is the best president ever

ALEYOMBA GEKKE NKOI CHOICE VARIABLE, SSH is the best president ever ever...wanaomchukia wana lao jambo
 
Mbona hayo ma fly-over Dar nzima, na Mogororo Road...ni JPM
Sasa flyover 2 ndio zinakuchanganya? Acha ushamba flyover ni daraja tuu na Kuna Madaraja Yana gharama kubwa kuliko huyo tu flyover..JK mwenyewe alijenga kule kurasini punguza ujinga.
 
Waulize CCM wenzako iliwezekana vipi wakampa umakamu then urais
 
Hawawezi kukubari hili ila nawaambia Tanzania itakuwa Mpya chini ya Samia Kwa sababu ni Rais mwenye akili bahati n Nyota kali sana.
 

Kuwa chawa ni Mzigo wa dhambi na kuwa mwanakijani aina yako tayari unatokuwa unatoka Ukoo mmoja wa kishetani. Haya kachukue UDASI wa Mchamba wima
 
Huwezi kumpinga Kikwete Kwenye Ujenzi Wewe Mbulula.
Kama Unamsifia Samia Msifiye Lkn Usimfananishe Na Kikwete.
Bado Hajamfikia.
 
Ningependa na barabara za Shinyanga to Mwanza, especially ya Mwanza sehemu kubwa imeoza, watuwekee lami iliyo enda shule mkuu, asilimia kubwa ya barabara hiyo imejaa viraka, lami isiyo na kiwango, marais waliopita sijaona wa kushughulikia, kutwa kuziba mashimo/viraka. In short barabara ya mwanza to shinyanga imechoka, waibomoe yote na waanze upya
 
Kuna maeneo kweli serikali ipewe maua yake
 
Mpuuzi wewe umevimbiwa maharage unatoa mashuzi tu hapa barabara zilishajengwa hizo unazo pigia debe wewe ni marudio kwani watu wanapita kwenye vumbi hivi sasa!
Kipara kipya una matatizo.
Hakuna barabara Ata Moja Iliyotajwa Hapo Ambayo Imejengwa kwa Kiwango cha Lami
 
Hapa Bado Kuna tatizo la priorities, malori yote yanatoka Bandarini kuelekea nchi jirani za Burundi, Uganda na Rwanda huwa malori yanagawanyikia Morogoro uelekeo WA Dodoma, na pia uelekeo wa Malawi, Zambia. Na Congo DRC malori huendelea uelekeo WA mbeya, Sasa priority ya kuweka njia za malori ni kati ya DSM na Morogoro, Iweje Igawa na Tunduma!? Muda mwingi unapotezewa DSM na Morogoro, issue ya ajali tuweke kando kwanza
 
Ni mimi tu ndio sijaona maana ya EPFC, ni nini hasa?
Huwezi jua shida unashinda kwenye umbea mda mwingi..

EPC+F maana yake Engineering (detailed design),Procurement, Construction and Financing..

Kiufupi Serikali inaalika mkandarasi anaeweza kufanya hizo kazi na aoneshe financing model kabisa harafu wnakubaliana gharama Kwa mda mrefu yaani concessional agreement,risks zote atabeba contractors hivyo itamlazimu kuwa makini na kujenga Kwa Ubora na atakuwa analiowa mdogo mdogo ndani ya mda wa consessional agreements inaweza fika miaka 30 na mda wote huo ni wajibu wa contractor ku maintain Barabara kabl ya kuja kukabidhi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…