Acha porojo Mzee,Zingejengwa Km 12,000 kama unavyosema wewe Mikoa yote Tanzania ingekuwa imeunganishwa na lami..
Kikwete alijitahidi kujenga ndio ila sio zaidi ya km 8,000 tena Kwa miaka 10,Sasa hizi tunazozungumzia Sasa ni sehemu tuu ya maelfu ya Barabara zingine ambazo zikianza ujenzi 2021/22 na 2022/23,Bado za Bajeti Mpya ya 2023/24 hazijasainiwa elewa Hilo..
Ndio.kusema Kwa mwaka 2022/23 Kuna hizi km 2,000 plus plus hizi hapa zingine [emoji116]
View attachment 2660092
Tatizo hujishughulishi na takwimu, unaongozwa na mihemuko kuliko weledi.
Nenda TANROADS wakupe takwimu.
Kama huwezi, chukua haya yakusaidie:
Wakati wa utawala wa Kikwete zilijengwa kilometa 12,000 barabara za lami. Barabara ndefu kabisa wakati wa utawala wake:
1) Dodoma-Tinde-Kahama-mpakani na Rwanda (zaidi ya kilometa 700)
2) Dodoma -Iringa (kilometer 264)
3) Tunduma-Sumbawanga-Mpanda (zaidi ya kilometa 400)
4) Songea=Tunduru-Masasi (zaidi ya kilometa 400)
5) Tinde = Mwanza (zaidi ya kilometa 200)
6) Mwanza = Geita - Bukoba- mpakani na Uganda (zaidi ya kilometa 400)
7) Dar - Iringa - Mafinga upgrade (zaidi ya 600km)
8) Chalinze -Korogwe-Moshi-Arusha upgrade (zaidi ya 500km)
9) Manyoni -Itigi-Tabora-Urambo (zaidi ya 300km)
10) Bwanga-Ngara-Kabanga-mpakani na Burundi (zaidi ya 300km)
Na nyingine nyingi za kilometa chini ya 300.
Nimekuwekea hizo chache ndefu ili ikusaidie isiye na kumbukumbu.
Tatizo mnaweka mihemko mbele, weledi mnaweka makabatini.
Wakati wa awamu ya Magufuli barabara za lami zimejengwa 2,800km.
Katika tawala zote, kilometer nyingi za barabara za lami zimejengwa wakati wa Kikwete.
Ungekuwa mtu wa kutafakari, ungejiuliza, hayo matengenezo ya kilometa zaidi ya 23,000 ya barabara kuu yalikuwa yanafanyika wapi kama hizo barabara hazikuwa tayari zimejengwa?
Kwanza ufahamu kuwa hakuna mkoa mpaka sasa hivi ambao haufikiki kwa barabara ya lami. Lakini kuna mikoa michache ambayo hazina barabara za kukatisha kuufikia mkoa jirani, mpaka upitie mkoa mwingine. Kwa mfano, una uwezo wa kutoka Dar mpaka Songea kwa barabara za lami 2, yaani Dar-Masasi-Songea; na Dar-Iringa-Songea. Lakini hakuna barabara ya lami ya kukatisha kutoka Mikumi direct to Songea. Vivyo hivyo kwa mikoa kama Tanga to Dodoma. Lakini una uwezo wa kufika Dodoma toka Tanga kwa barabara ya lami. Kabla ya utawala wa Kikwete kuna mikoa ambayo ilikuwa hakuna hata barabara moja ya lami ya kufikia makao makuu ya mkoa, hata kwa kuzunguka.