Zaidi ya KM 2000 za barabara kuanza kujengwa kwa mtindo wa EPC +F. Serikali yasema hazitalipiwa Tozo

Zaidi ya KM 2000 za barabara kuanza kujengwa kwa mtindo wa EPC +F. Serikali yasema hazitalipiwa Tozo

Pia nashauri waikumbuke barabara ya Makambako Songea. Imesha chakaa sana kwasababu ya Magari yanayochukua Makaa ya mawe.....na pia ni ya zamani mno
Iko kwenye manunuzi,baadae mwaka ujao ujenzi unaanza kuanzia Songea km 100 Kuna pesa za IMF pale.
 
Dar-Moro-Dom itakuwa express way njia 6 na kati ya hizo kutakuwa n dedicated lanes za Malori..

Morogoro Hadi Igawa njia ilishajengwa ni pana ya kutosha japo sio njia 4.

Kwa nini section ya Igawa ni Kwa sababu kule mwishoni Malori yanakuwa mengi maana ndiko destination na pia ndiko yanakoingilia kama tuu kipande Cha Dar-Moro..

On top of that Kuanzia Njombe Hadi Tunduma Kuna Miji Mingi sana hapo na hivyo traffic ya magari ya Kawaida ni kubwa sana on top of Malori.eg Mbeya Tunduma Costa zile zinaachiana dk 5 tuu kati ya gari na gari kutoka Stand ,hakuna section yenye minbus nyingi za Abiria kama hiyo ,labda ya Moshi Arusha inaweza fuata maana napo wanataka kuweka njia 4 pia..
Lost Time kubwa ipo recorded kati ya DSM, Bandarini na Morogoro, fikiria hadi busses zinatumia masaa manne km 191 average traveling time 47.75 km per hour, this is too much, Je Kwa malori si ndio 30!?
 
Wewe kajinga kweli,alijenga Nchi nzima km ngapi Kwa mda gani?
Soma haya maelekezo hapa utoe ujinga kichwani

Mkjuu kweli ni jambo jema, lakini kwa upande wa pili kwa hali ilivyo, watoto wetu wa kike wanaojiunga na shule za secondary wengi wapangisha kwenye nyumba za mitaani; yaani ni kama wale waliohitimu elimu yao na kuajiriwa. Wengi wa watoto hawa wa secondary ni watoto wa watanzania maskini sana ambao nadhani hata kuwahudumia hao watoto ni kwa shida sana na kupelekea hata vijana wetu wa daladala wanachukuwa jukumu la kuwalipia pango hizo na hatimaye wengi kupata mimba na hivyo kukatishwa ndoto zao.
Aidha huduma ya maji kwa wa TZ wengi huko vijijini inatosha, mbona hamweki mikakati yenye nguvu kama hii? Magonjwa mengi ya wa-TZ yanatokana na matumizi ya maji machafu yasio salama na hivyo kupelekea kujenga mazahanati meengi na bajeti kubwa za madawa, kisa ni
 
Huwezi jua shida unashinda kwenye umbea mda mwingi..

EPC+F maana yake Engineering (detailed design),Procurement, Construction and Financing..

Kiufupi Serikali inaalika mkandarasi anaeweza kufanya hizo kazi na aoneshe financing model kabisa harafu wnakubaliana gharama Kwa mda mrefu yaani concessional agreement,risks zote atabeba contractors hivyo itamlazimu kuwa makini na kujenga Kwa Ubora na atakuwa analiowa mdogo mdogo ndani ya mda wa consessional agreements inaweza fika miaka 30 na mda wote huo ni wajibu wa contractor ku maintain Barabara kabl ya kuja kukabidhi.
Kitefu chake nilishakuona, ila huo ufafanuzi ndio nilitaka.

Anyway, tunaomba hiyo financing model isihusishe tozo ya barabara
 
Kitefu chake nilishakuona, ila huo ufafanuzi ndio nilitaka.

Anyway, tunaomba hiyo financing model isihusishe tozo ya barabara
Hakuna tozo mbona hamuelewi? Tozo zipo kwenye Barabara za Expressway zinazojengwa Kwa Model ya PPP na inakuja kati ya Kibaha Moro Dom
 
Mkjuu kweli ni jambo jema, lakini kwa upande wa pili kwa hali ilivyo, watoto wetu wa kike wanaojiunga na shule za secondary wengi wapangisha kwenye nyumba za mitaani; yaani ni kama wale waliohitimu elimu yao na kuajiriwa. Wengi wa watoto hawa wa secondary ni watoto wa watanzania maskini sana ambao nadhani hata kuwahudumia hao watoto ni kwa shida sana na kupelekea hata vijana wetu wa daladala wanachukuwa jukumu la kuwalipia pango hizo na hatimaye wengi kupata mimba na hivyo kukatishwa ndoto zao.
Aidha huduma ya maji kwa wa TZ wengi huko vijijini inatosha, mbona hamweki mikakati yenye nguvu kama hii? Magonjwa mengi ya wa-TZ yanatokana na matumizi ya maji machafu yasio salama na hivyo kupelekea kujenga mazahanati meengi na bajeti kubwa za madawa, kisa ni
Huko kwenye Elimu usiseme,hakuna sekta ambayo Rais kaipa msukumo mkubwa kama hiyo,shida yenu hamfuatilii Bajeti za serikali..
 
Lost Time kubwa ipo recorded kati ya DSM, Bandarini na Morogoro, fikiria hadi busses zinatumia masaa manne km 191 average traveling time 47.75 km per hour, this is too much, Je Kwa malori si ndio 30!?
Umeshaambiwa hapo Kuna expressway inakuja iko.kwenye manunuzi huelewi nini?

Swala la kupotea Kwa mda ni kote kote mda unapotea,on top of that Ile section imechakaa sana,Barabara nyembamba,na Ina casualties sana Kwa sababu hizo na nature ya terrain ,so Serikali Iko sahihi kabisa kuanza na Ile section.
 
Kwa mara ya Kwanza baada ya Uhuru Tanzania imepata Rais Samia apewe maua yake.

Serikali ya Rais Samia imeandika Historia nyingine ya ubunifu kwa kusaini kuanza ujenzi wa barabara za kuu za lami kwenye mikoa 13 kwa pamoja zenye jumla ya urefu wa KM 2035 kwa mtindo wa EPC+ F (Engineering, Procurement, Construction and Finance) kwa gharama ya Tsh.Tilioni 3.8 ambapo miradi inatarajiwa Kukamilika ndani ya miaka 4 (2023-2027).

Akizungumza wakati wa kushuhudia kutiwa saini kwa mikataba hiyo Jijini Dodoma, Waziri wa Ujenzi Prof. Mbarawa amesema kwamba, barabara hizo hazitokuwa za kulipia tozo kama wapotoshaji wanavyosema. Ikumbukwe hii haijawahi tokea toka Uhuru, walinda legacy mnafundishwa kazi.

My Take
Samia anawaonesha kwamba Private Sector inalipa kuliko Ujamaa mbuzi ambao baadhi ya watu wasiojielewa wanakumbatia.

Ndio maana hata kwenye Bandari anataka awafundishe namna ya kutumia rasilimali kwa manufaa ya watu badala ya kuhubiri propaganda za Uzalendo mbuzi na umaskini over years.

Hongera sana Mh. Rais, na Waziri wa Mbarawa Kwa Ubunifu,Historia itaandika jina lako kwa wino Mwekundu.

=====

MIRADI YA BARABARA ILIYOSAINIWA KWA UTARATIBU WA EPC + F

i) Barabara ya Kidatu – Ifakara – Lupiro – Malinyi – Kilosa Kwa Mpepo – Londo – Lumecha/Songea (km 435.8) inapita katika mikoa ya Morogoro na Ruvuma na inapita pia katika Majimbo ya Kilombelo, Ulanga, Malinyi na Namtumbo;

ii) Barabara ya Arusha – Kibaya – Kongwa (km 453.42) inapita katika Mikoa ya Arusha, Manyara na Dodoma na inapita katika Majimbo ya Arusha Mjini, Arumeru Magharibi, Simanjiro, Kiteto na Kongwa;

iii) Barabara ya Handeni – Kiberashi – Kijungu – Kibaya – Njoro – Olboroti – Mrijo Chini – Dalai – Bicha – Chambolo – Chemba – Kwa Mtoro – Singida (km 384.33) inapita katika Mikoa ya Tanga, Manyara, Dodoma na Singida na inapita katika Majimbo ya Kilindi, Chemba, Kiteto, Singida Mashariki na Iramba Mashariki;

iv) Barabara ya Igawa – Songwe – Tunduma (njia nne) (km 237.9) inapita katika Mikoa ya Mbeya na Songwe na inapita katika Majimbo ya Mbarali, Mbeya Vijijini, Mbeya Mjini, Mbozi, Vwawa na Tunduma;

v) Barabara ya Masasi – Nachingwea – Liwale (km 175) inapita katika Mikoa ya Lindi na Mtwara na inapita katika Majimbo ya Masasi, Nachingwea na Liwale;

vi) Barabara ya Karatu – Mbulu – Haydom – Sibiti River – Lalago – Maswa (km 339) inapita katika Mikoa ya Manyara, Simiyu, Singida na Arusha na inapita katika Majimbo ya Mbulu Mjini, Mbulu Vijijini, Karatu, Iramba Mashariki, Meatu, Maswa Mashariki na Kisesa; na

vii) Barabara ya Mafinga – Mtwango – Mgololo (km 81) inapita katika Mkoa wa Iringa na inapita katika Majimbo ya Mufindi Kusini na Mafinga.
Hii ni zaidi ya maendeleo kwa nyakati hizi. Maelezo yote ya kimkakati. Bado tu morogoro mvuha dutumi kisaki
 
Back
Top Bottom