Zaidi ya KM 2000 za barabara kuanza kujengwa kwa mtindo wa EPC +F. Serikali yasema hazitalipiwa Tozo

Zaidi ya KM 2000 za barabara kuanza kujengwa kwa mtindo wa EPC +F. Serikali yasema hazitalipiwa Tozo

Kazi inaendelea 👇

Akili yetu ni bandari tu!!!!
Hata iwekwe lami barabara xote huko uliko hatutatoka kwenye reli , reli ni bandari tu.

EPC + F watanganyika watakuja kulipa kupitia wapi kama mbarawa anauza bandari?
 

Attachments

  • 5718FE6E-7162-4EC7-B180-968B72207A6B.jpeg
    5718FE6E-7162-4EC7-B180-968B72207A6B.jpeg
    23.3 KB · Views: 5
Kwa mara ya Kwanza baada ya Uhuru Tanzania imepata Rais Samia apewe maua yake.


Serikali ya Rais Samia imeandika Historia nyingine ya ubunifu kwa kusaini kuanza ujenzi wa barabara za kuu za lami kwenye mikoa 13 kwa pamoja zenye jumla ya urefu wa KM 2035 kwa mtindo wa EPC+ F (Engineering, Procurement, Construction and Finance) kwa gharama ya Tsh.Tilioni 3.8 ambapo miradi inatarajiwa Kukamilika ndani ya miaka 4 (2023-2027).


Akizungumza wakati wa kushuhudia kutiwa saini kwa mikataba hiyo Jijini Dodoma, Waziri wa Ujenzi Prof. Mbarawa amesema kwamba, barabara hizo hazitokuwa za kulipia tozo kama wapotoshaji wanavyosema. Ikumbukwe hii haijawahi tokea toka Uhuru, walinda legacy mnafundishwa kazi.

My Take
Samia anawaonesha kwamba Private Sector inalipa kuliko Ujamaa mbuzi ambao baadhi ya watu wasiojielewa wanakumbatia.

Ndio maana hata kwenye Bandari anataka awafundishe namna ya kutumia rasilimali kwa manufaa ya watu badala ya kuhubiri propaganda za Uzalendo mbuzi na umaskini over years.

Hongera sana Mh. Rais, na Waziri wa Mbarawa Kwa Ubunifu,Historia itaandika jina lako kwa wino Mwekundu.

=====

MIRADI YA BARABARA ILIYOSAINIWA KWA UTARATIBU WA EPC + F

i) Barabara ya Kidatu – Ifakara – Lupiro – Malinyi – Kilosa Kwa Mpepo – Londo – Lumecha/Songea (km 435.8) inapita katika mikoa ya Morogoro na Ruvuma na inapita pia katika Majimbo ya Kilombelo, Ulanga, Malinyi na Namtumbo;

ii) Barabara ya Arusha – Kibaya – Kongwa (km 453.42) inapita katika Mikoa ya Arusha, Manyara na Dodoma na inapita katika Majimbo ya Arusha Mjini, Arumeru Magharibi, Simanjiro, Kiteto na Kongwa;

iii) Barabara ya Handeni – Kiberashi – Kijungu – Kibaya – Njoro – Olboroti – Mrijo Chini – Dalai – Bicha – Chambolo – Chemba – Kwa Mtoro – Singida (km 384.33) inapita katika Mikoa ya Tanga, Manyara, Dodoma na Singida na inapita katika Majimbo ya Kilindi, Chemba, Kiteto, Singida Mashariki na Iramba Mashariki;

iv) Barabara ya Igawa – Songwe – Tunduma (njia nne) (km 237.9) inapita katika Mikoa ya Mbeya na Songwe na inapita katika Majimbo ya Mbarali, Mbeya Vijijini, Mbeya Mjini, Mbozi, Vwawa na Tunduma;

v) Barabara ya Masasi – Nachingwea – Liwale (km 175) inapita katika Mikoa ya Lindi na Mtwara na inapita katika Majimbo ya Masasi, Nachingwea na Liwale;

vi) Barabara ya Karatu – Mbulu – Haydom – Sibiti River – Lalago – Maswa (km 339) inapita katika Mikoa ya Manyara, Simiyu, Singida na Arusha na inapita katika Majimbo ya Mbulu Mjini, Mbulu Vijijini, Karatu, Iramba Mashariki, Meatu, Maswa Mashariki na Kisesa; na

vii) Barabara ya Mafinga – Mtwango – Mgololo (km 81) inapita katika Mkoa wa Iringa na inapita katika Majimbo ya Mufindi Kusini na Mafinga.

Vizuri
 

Attachments

  • 7297341B-1120-4DAE-847B-B57FF5A6E85F.jpeg
    7297341B-1120-4DAE-847B-B57FF5A6E85F.jpeg
    49 KB · Views: 3
  • 118E587B-C1B2-452E-9897-CBA02A5865D2.jpeg
    118E587B-C1B2-452E-9897-CBA02A5865D2.jpeg
    64.1 KB · Views: 3
  • 802A7FB9-6D74-4B1B-BD69-1BB77E8DF0C3.jpeg
    802A7FB9-6D74-4B1B-BD69-1BB77E8DF0C3.jpeg
    51.7 KB · Views: 3
  • 3191375D-1A46-494A-BC97-5C722FEBBA97.jpeg
    3191375D-1A46-494A-BC97-5C722FEBBA97.jpeg
    63 KB · Views: 3
  • 9A1AA1BB-9A55-4CDA-901A-731E3D0B07B8.jpeg
    9A1AA1BB-9A55-4CDA-901A-731E3D0B07B8.jpeg
    44.1 KB · Views: 3
Back
Top Bottom