Zaidi ya TZS Bilioni 70 zatengwa Ujenzi wa mradi wa maji Biharamulo

Zaidi ya TZS Bilioni 70 zatengwa Ujenzi wa mradi wa maji Biharamulo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Kufatia kuwepo kwa kero ya muda mrefu ya maji katika wilaya ya Biharamulo moani Kagera, serikali imetenga Zaidi ya shilingi Bilioni 70 kwaajili ya kuanza ujenzi wa maji kutok ziwa Victoria.

Kauli hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Mhandisi Ezra Chiwelesa wakati alipokuwa akiongea na wanachama wa ccm wilaya ya Biharamulo ambapo amewasihi wananchi kumshukuru na mkumpongeza Rais Samia kwa kuamu kuwatua wakina mama ndoo kichwani.

Ezra Chiwelesa Amesema kuwa viongozi wengi wamepita katika nchi hii lakini hakuna mradi mkubwa uliowahi kutekelezwa wilayani humo na miradi mingi sasa imekuja katika kipindi cha Rais Samia.

Aidha, Chiwelesa amewapongeza wananchama hao kwa ushindi mkubwa wa ambao chama chake ulipata katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika November 27, mwaka huu ambapo wilaya ya Biharamulo iliongoza kwa wingi wa kura.
 
Back
Top Bottom