Zaka ya 10% unatoa kwenye faida au kwenye utajiri wako?

Zaka haitakiwa itolewe kipindi hiki ambacho serikali zimechukiq majukumu ya kuhudumia wananchi. Ulishalipa kodi serikali ni inatosha zaidi ya hapo ni kutoa sadaka tu kwa wahitaji na ukienda kwenye ibadan.
 
Ile net inayoingia kwenye account baada ya makato Mimi hua nafanya ivo
Uwa kuna mafundisho kwamba zaka inatakiwa itolewe kwa usahihi yaani bila kuongeza au kupunguza, hivyo ibaki moja ya kumi ya faida. Sasa bila kutoa PAYE, NSSF na gharama nyingine zilizopelekea kupata huo mshahara kama usafiri wa kwenda kazini, chakula n.k. hicho kiasi sahihi cha kupunguzwa moja ya kumi yake kama zaka utakipataje?
 
Yaani sijaelewa [emoji854]

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Nafikiri Unaitaji kujua tofauti ya baadhi ya vitu unavyovitaja...

Kuna Matoleo,malimbuko, Zaka ,sadaka na Nadhiri...

Wengi sana vinakuchanganyeni mnatakiwa kujifunza kuhusu hivyo vitu..
Zakayo aliuza nusu ya mali zake (Hii ilikuwa sadaka)

Mama mjano (alitoa sadaka)
Anania na safira na barnaba walitoa malimbuko ya mali zao na kufanya thamani ile kuendeleza injili.. japo anania alificha sehemu ya mali ile ...

Kipindi nikiwa mchungaji hatukuwa na mindset hii...naona wengi wa siku hizi ni wachungaji wa mishahara...

Yohana 10:12-13

"Mtu wa mshahara, wala si mchungaji, ambaye kondoo si mali yake, humwona mbwa-mwitu anakuja, akawaacha kondoo na kukimbia; na mbwa-mwitu huwakamata na kuwatawanya.
Yule hukimbia kwa kuwa ni mtu wa mshahara; wala mambo ya kondoo si kitu kwake."


wachungaji siku hizi wako radhi kuon muumuni anaumia kwa sababu ya wao kuwadai zaka zao watu wanafatwa mpaka makazini watu wanashida ila bado wanalazimishwa si kati ya mafundisho ya yesu
 
Yohana 10:12-13

"Mtu wa mshahara, wala si mchungaji, ambaye kondoo si mali yake, humwona mbwa-mwitu anakuja, akawaacha kondoo na kukimbia; na mbwa-mwitu huwakamata na kuwatawanya.
Yule hukimbia kwa kuwa ni mtu wa mshahara; wala mambo ya kondoo si kitu kwake."

Tafsiri ya BHN

11 Mimi ni mchungaji mwema. Mchungaji mwema huyatoa maisha yake kwa ajili ya kondoo. 12 Mtumishi anayelipwa ili kuwachunga kondoo yuko tofauti na mchungaji. Mtumishi wa mshahara, kondoo siyo mali yake. Hivyo anapomwona mbwa mwitu anakuja, hukimbia na kuwaacha kondoo peke yao. Mbwa mwitu huwashambulia na kuwatawanya kondoo. 13 Mtu huyu huwakimbia kondoo kwa sababu yeye ni mfanyakazi wa mshahara tu. Hawajali kabisa kondoo.


Kwa kuongeza zaidi...

1 Petro 5:2

lichungeni kundi la Mungu lililo kwenu, na kulisimamia, si kwa kulazimishwa, bali kwa hiari kama Mungu atakavyo; si kwa kutaka fedha , bali kwa moyo.
 
Hujajibu swali....

Nimeuliza tofauti ya hekalu na kanisa ni nini ?
Kajifunze tofauti ya hekalu na sinagogi ....kanisa ni kama sinagogi tu hekalu ni moja tu...kasome hata maandiko...pazia la hekalu likapapuka katikati kwanini siyo la sinagogi.
 
1,000,000+70,000=(Mapato yote)
1/10 ya mapato = Mapato yote/10.
Nionesheeni mahali palipoandikwa 10% inatokana na faida niache kuchangia.
Hiyo haipo bwana! Ukienda kichwa kichwa tunafunga biashara. Tena mimi nimeenda mbali zaidi kama nina rejesho natoa kabisa hilo rejesho kwenye faida inayobaki ndiyo nakokotoa 10% yake!
 
Kajifunze tofauti ya hekalu na sinagogi ....kanisa ni kama sinagogi tu hekalu ni moja tu...kasome hata maandiko...pazia la hekalu likapapuka katikati kwanini siyo la sinagogi.
Okay....hekalu ni zaidi ya Sinagogi ila ni kwa desturi za Kiyahudi tu.

Sasa tuje kwa wakristo je kupeleka zaka kanisani kuna ubaya ?
 
AGANO jipya hakuna katazo la Kutoa sadaka na ZAKA.

Ndomana hata usipotoa, hudaiwi.

AGANO jipya tunaongozwa na Roho mtakatifu.

Kulipa ZAKA ni Kwa faida ya mtoaji na Si mpokeaji.

Apendaye sana hutoa sana, asiyependa ni bahiri.

Ukimpenda Mungu, lazima ulipe ZAKA zaidi hata ya 10% na utatoka sadaka na matoleo mengine, sawasawa na maelekezo ya Roho mtakatifu.

Amen
 
NDyo zaka lazma ilipwe na inalipwa kwa wanaohotaji tu na watu wasiokuwa na uwezo nndo watakaopatiwa
 
Kajifunze tofauti ya hekalu na sinagogi ....kanisa ni kama sinagogi tu hekalu ni moja tu...kasome hata maandiko...pazia la hekalu likapapuka katikati kwanini siyo la sinagogi.
Dah huwa tunapishana sana ila niseme tu leo uko sahihi kwa 100%
Unashusha sana ukweli uneacha kujifikira wewe leo unafikiria watu zaidi waelimike
 
In maana mpaka karne hii hekalu ni moja tu ?

Kwani ibada za hekaluni na kwenye sinagogi zina tofauti gani ?
Sinagogi hata chumba chako unaweza kukifanya sinagogo ila hekalu hata daudi na kuongea kwake na mungu na kukubalika na mungu akuweza kupata ruhusa kulijenga ...je sinagogi na kanisa si mtu yoyote anajenga atakavyo ...tumia akili acha upumbavu wa ubishi husio na faida .
 
Kama fungu la kumi alikupelekwa kwenye masinagogi imekuwaje upeleke kanisani wewe ni kichaa haswa
 
Wapi pameandikwa kwenye faida?
Faida ni kile Mungu alichokuwezesha kukipata baada ya wewe kuwekeza mtaji, hicho ndicho unachopaswa kukitolea zaka ya asilimia 10 au zaidi ukiamua hivyo.

Mwanzo 14:16
Naye akarudisha mali zote, akamrudisha na Lutu nduguye na mali zake, na wanawake pia, na watu.

Mwanzo 14:20
Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.

Abraham alimpa kuhani Melikizedeki fungu la kumi la vitu vyote alivyovitwaa kutoka kwa wale wavamizi (asilimia kumi ya faida aliyopata).

Kumbukumbu la Torati 14:22
Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka.

Toa fungu la kumi la 'maongeo: yote ya mbegu zako......(faida inayotokana na mbegu zako kwenye shamba mwaka baada ya mwaka).



Kumbukumbu la Torati 14 28
Kila mwaka wa tatu, mwisho wake, toa fungu la kumi lote la maongeo yako ya mwaka huo, uliweke ndani ya malango yako;

Toa fungu la kumi la maongeo (mapato,maongezeko) yako ya mwaka huo ndani ya malango yakk.
 
Kama ni mtumishi serikali imkate PAYE, makato ya mifuko ya kijamii (NSSF n.k.), makato ya mikopo, makato ya uanachama wa vyama vya wafanyakazi, bima ya afya kisha mtumishi huyo huyo atoe matoleo, malimbuko, zaka, sadaka, nadhiri n.k. mbona atakuwa na maisha magumu sana huyo mtumishi wajameni?
 
Acha kunitukana, jadili kistaarabu.

Sababu ya Daudi kutoruhusiwa kumjengea Mungu hekalu inajulikana wazi ndio maana baadae Sulemani alilijenga, hivyo yeyote angeweza tu kujenga hata wewe.

Hekalu na Sinagogi hakuna tofauti yeyote, ila Sinagogi kubwa ndio huitwa hekalu kwa desturi za Kiyahudi.

Hekalu ni mahali pa ibada katika dini ya Kiyahudi, wakati sinagogi ni jengo la ibada na kusanyiko la Kiyahudi lililotumika kwa sala na kufundisha Torati. Hekalu kuu lililokuwepo lilikuwa Hekalu la Yerusalemu lililoharibiwa, na sinagogi ni vituo vya ibada vya jamii za Kiyahudi duniani kote.

Hata Kanisa ni hekalu pia
 
Kama fungu la kumi alikupelekwa kwenye masinagogi imekuwaje upeleke kanisani wewe ni kichaa haswa
Sisi wakristo tuna Kanisa sio Sinagogi hivyo kupeleka zaka kanisani ni sahihi kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…