Zamani: Hii cable ya kihindi ilitaka kuuwa mtu

Zamani: Hii cable ya kihindi ilitaka kuuwa mtu

View attachment 3626987
Nimepita mitandaoni huko nikaona hii Cable ya umeme , nikakumbuka miaka ya 2000. Kuna siku nilitoa hii Cable kwa nje nikachomeka mashine ya kunyolea.

Sasa wakati nasubiri katokea mtoto wa jirani na msumari wa nchi 6. (Misumari tulikuwa tunatumia kucheza mchezo unaitwa domeka) Mnachora jedwali chini halafu mnakuwa mnacheza huo.

Dogo katoka huko na msumari wake akaja akachomeka kwenye cable halafu ilikuwa on. Aisee ile shoti aliyopigwa yule dogo nashindwa hata kuelezea maana alinasa akawa analia huku anakata viuno na ile taharuki iliyokuwepo nikawa namuangalia nashindwa hata la kufanya.
Mkuu mbona lugha uliyotumia kuelezea ni kama ya mtu anayeelezea juu ya sinema ya kuchekesha aliyoiona? No empathy, no regreat.
 
Mkuu mbona lugha uliyotumia kuelezea ni kama ya mtu anayeelezea juu ya sinema ya kuchekesha aliyoiona? No empathy, no regreat.
Mkuu ni karibia miaka 26 iliyopita na nimeelezea hivyo baada ya kuona uzi wa jamaa akielezea zile heater tulizokuwa tunaingia nazo mabwenini kuchemshia maji au chai
 
Back
Top Bottom