Zamani nilikuwa namshangaa mtu aliyefanikiwa kimaisha na hasaidii ndugu zake, Leo mimi natamani hata kuwapiga Risasi

Mbona baba humsemi?
Baba akikutana na kimada hachelewi kuwapiga chini. Mama ni mama tu. Mama hamtupi mwanae. True love iko kwa mama.

Kuna kipindi unapitia magum kila mtu humuoni ila mama Yuko nawe kwa upendo na moyo wote. Japo hata baba wa dizaini hiyo wapo ila mama ni zaidi.


I love all Mama out there...
 
Hakika mkuu

Mama ana upendo wa kweli
 
Ngoja ndugu zako waje kususia maiti yako ukajizike na pesa zako ndipo utajua umuhimu wa ndugu!
Mfu hahisi kitu kamwe, hata wakisusa wakaacha ujiozee barabarani haina impact kwa marehemu
 
Tenda wema uwende zako usingoje shukrani. Hayo ndio maombi yangu kila siku Kwa Mungu. Hata ninapo msaidia Dada yangu sipendi Sana mume ajuwe nimesaidia au Nani ninmm nayeye. Ukifanya mema utatendewa mema wala sio kazima awe Yule ulie mtendea hapo ndipo nampenda Mungu.
 
Hakika mkuu

Mama ana upendo wa kweli
Mwaka 2017 nilipata mushkeri kwenye kibarua changu, watu waliokuwa na Mimi ni mama na dada yangu pamoja na girlfriend wangu.

Wengine wote waliishia kuwa wananipigia simu na kusema hivi hela ulikuwa unazifanyia nini Hadi unaishi maisha ya shida. Nilikuwa naumia sana. Unakumbuka si Hawa kila mwisho wa mwezi ulikuwa unatuma hela kwao hupati jibu. Harusi zao na misiba yote ulikuwa unapigiwa simu utoe hela kiasi tofauti na wachangiaji wa kawaida. Ila ukiyumba wanasema eti hela ulikuwa unapeleka wapi na kashifa kibao.


Ila Mama alibaki na true love , She was and still a comforter of all time. Maza unampa Buku ten analia Hadi machozi kwa furaha ila hao ndugu wengine unawapa 20,000 wanasema haitoshi na kukuongelea ushenzi.



Nilichojifunza baki na ndugu zako na wa kwanza awe mama. Hao wengine Piga mstari kabisa toa pale unapoona inafaa kutoa msaada.


Kingine kwa ndugu saidia watoto acha kusaidia majitu mazima. Kama Kuna mtoto anaumwa saidia. Kama mtoto anahitaji ada saidia pale unapoweza.


Mimi mjomba wangu alikuwa na hii principal kasaidia waroto ukoo mzima Hadi tumefika vyuo. Ametengeneza kizazi tunampenda sana maaana tulikuwa tunaona anavyotusaidia hata Kama unahitaji Ada ya milion unapewa. Na alikuwa na muhasibu wake kabisa wa kusimamia hayo mahesabu ya ndugu.


Na ndugu zake wakubwa aliwaambia hamtakuja kula hela yangu maana hamna shukran ila nitawasaidia watoto wenu ambao ni malaika. Huwezi amin mpaka Sasa Nina kumbukumbu za nilivyokuwa darasa la kwanza mjomba anatuma watu walete hela nyumbani mimi niende shule. Mpaka nafika chuo.
 
Kupitia andiko lako hili nimejifunza kitu
 
Safi momy ale..za masiku...nakumiss.hivi sijui kwanini inakua hivi? Ila Kuna rafiki yangu kwao wako 5! Wanasaidiana Sana...Yani hakuna kukopa nje .wanakopana wenyewe na kupigana tafu balaa! Sijui wengine inakuwa ishu
Watanzania wengi ndivyo tulivyo, majungu na roho mbaya
 
Kabisa kabisa mkuu,daah
 
Huku kutunziana watoto sina imani nako sana miaka hii
Kabisa mkuu mi mshua alikufa ndo nipo seven then nikamaliza shule nikafail kuingia sekondari nakumbuka kulikuwa na msiba wa bibi yangu mzaa baba sasa kwenye vikundi vyake wakawa wametoa rambi rambi kama milioni tatu huwezi amini nilipoomba kupelekwa shule baba yangu mkubwa alinambia siwezi kusoma mi mi muhuni nililia sana akatokea mdhamini rafiki yake na baba akanipeleka shule nilisoma kwa hasira nyingi na kufika chuo saivi wanabaki wanaona aibu tu na wote waliokuwa na pesa wamefirisika watoto wao hawaishi kunipiga vizinga kuna time mpaka nasema sijui nisiwasaidie ila naona wao hawana makosa
 
Ndugu miyeyusho sana..mi wazazi wamefariki nipo std 4, hakuna hata ndugu aliyejishughulisha na mimi, nilivyosoma na kukua Mungu mwenyewe anajua..
Leo maisha yana afadhali ndo wanaanza kuibuka, mi huwa nawachora tu..
Usitegemee ndugu upande wa baba wakusomeshee, wataishia kugawana mali kama mbweha wanavyogawana swala, nimeshaona hii kwa wengi, sijui wana nini hawa, ila wajomba ni nadra kukutupaaa
 
Usitegemee ndugu upande wa baba wakusomeshee, wataishia kugawana mali kama mbweha wanavyogawana swala, nimeshaona hii kwa wengi, sijui wana nini hawa, ila wajomba ni nadra kukutupaaa
nashawishika kuamini hili
 
Wengi munaochukia ndugu inaonekana mumetokea familia za shida na mumekulia maisha ya njaa sana,..... Kiukweli kama baba yako mdogo, wajomba, shangazi, bibi babu wapo vizuri, wao na watoto wao..... Kuna shida gani, mi naona fahali tu kusaidia mtu yeyote aliye na shida duniani
 
Usitegemee ndugu upande wa baba wakusomeshee, wataishia kugawana mali kama mbweha wanavyogawana swala, nimeshaona hii kwa wengi, sijui wana nini hawa, ila wajomba ni nadra kukutupaaa
Uliloandika Ni kweli ndugu wa mume watakupenda kaka yao akiwa hai siku akiondoka duniani ndio wa kwanza kukimbilia Mali, ujombani ndio hulea watoto wa dada zao bila shida Kama mtoto wa familia. Shikamooni wajomba wote
 
Tatizo la binadamu ukimpa samaki jiandae kulaumiwa akimaliza! Mfundishe kuvua. Mimi ndugu HATA aje ameshikilia mkono umekatika namwambia kauze vyako kwanza vikiisha ndio nikusaidie. Huwezi kukizi mahitaji ys binadamu kwa kumpa fresh money!
 
Tatizo la watu wanaosaidia wanataka gratification. Hapo ndipo mateso yenu yanapoanzia...

Ukimsaidia mtu huwekezi, ukimsaidia mtu ni Wema ambao kanuni yake ni kwenda zako.

Jitahidini kuishi kwa kanuni na mnapotaka kuzivunja kanuni hakikisheni mmezielewa kwanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…