Zamani nilivyokuwa Mjinga!

Hivi umesema ulivokuwa mtoto au hadi sahivi una ujinga mpenzi?
 
Me nilikuwa najua eti Posta kuna bomba kuubwaa ukienda kupost barua inasafirishwa ndani ya bomba hadi inafika ulikotuma!! Thijui kungekuwa na mabomba mangapi!
 
Mimi nilikuwa nafikili mtu akifia hospitali hutakiwi kulipia gharama za matibabu kwani nilidhani wanalipia waliopona tu.

kumbe mtu akifia hospital lazima umlipie gharama za matibabu??
Nilikuwa sijui.
 
Me nilikuwa najua eti Posta kuna bomba kuubwaa ukienda kupost barua inasafirishwa ndani ya bomba hadi inafika ulikotuma!! Thijui kungekuwa na mabomba mangapi!

Hahahaaa! Aisee kumbe mie nlikua na afadhali e? We ulikua empty kabisaa!!
 
nikiwa std iv mwalimu aliyekuja shuleni kwetu kufanya majaribio kwa vitendo kutoka chuoni alikuwa anasoma insha na ktk mkato anasema koma,.....basi nikajikuta nimeweka neno koma sehemu zote alizotamka.....................
 
mimi nilikua naamini kuna watu wamekaaa sehemu wananiangalia. na ni baada tu ya kuanza kuangalia sinema eti unamuona mtu anaiba au amejificha alafu wenzie hawamuoni nikajua na sisi ni hivyo hivyo kuna watu wanatuona na sisi hatuwaoni.
 
Sipati picha ulivyokua ukidokoa nyama unavyonyata na kujificha!
 
Afu Chimbuvu kuna swali nlikuuliza hujajibu.

Mimi bana wakati mdogo tukisafiri afu mkapishana na gari kuna mlio ule wa vuuuum mi nkamuuliza mama vipi mbona gari letu halina akasema mpaka ununue ufunge kwenye gari..
 
Last edited by a moderator:
miaka ya 1988 ninakumbuka nilikuwa na rafiki yangu wa utoto alitudanganya maalbino ni wazungu kumbe walemavu wa ngozi, mawingu ya angani nilijua ni moshi unaotokana na moto. wakati wa mchakamchaka darasa la kwanza wimbo wa mandela afunguliwe gerezani ulinifanya nijue kuwa mandela ni mtanzania.
 
Mi nilikuwa nikimuona mtu alievaa miwani alafu anakipara basi najua ni daktari pia tajiri wakutupa
 
Mi nilikuwa nikimuona mtu alievaa miwani alafu anakipara basi najua ni daktari pia tajiri wakutupa

mimi nliharibu redio yetu ya mkulima iliniwaone watangazaj manake mzee nlimuuliza akasema kuna watu ndani ya redio,nlidata kukuta waya na mende wakikimbizana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…