Zamaradi Mketema aweka ujumbe wa siku ya Valentines kwa mumewe kwenye bango Morocco, Dar es Salaam

Zamaradi Mketema aweka ujumbe wa siku ya Valentines kwa mumewe kwenye bango Morocco, Dar es Salaam

Hapo zamaradi anaona kama amemuonesha upendo mume wake kumbe ndio anaipalilia makaa ndoa yake.

Kwanini nasema hivi? Siku zote wanawake hawapendani. Mwanamke anaweza akawa na rafiki mwenzake wa kike na kila jambo kuhusu mahusiano yake anamuweka wazi shosti yake lkn utashangaa shosti anamzunguka na kumuibia bwana.

Kumuweka kwenye bango kumewapa "alert" mashosti na wanawake wengine kuhisi Zamaradi anaishi maisha ya raha wkt wao kutwa kucha wanateseka na ndoa. HAWATOFURAHI. Mwisho wa siku watakimbizana kwa huyo jamaa na kumpa mitego ya kila aina na sidhani kama ataweza kuikwepa na mwisho atamsaliti na upendo walioujenga kwa miaka zaidi ya mitano kuisha na kuishia kupost status za kinyonge kutuita wanaume wote ma mbwa...

Haya mambo ya kuonyesha jamii umezama sana kwenye huba tuwaachie wenzetu. Huwa nawaheshimu sana wanaopendana kwa dhati na kuishi private life.

Anyways kupanga ni kuchagua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KWA UPANDE FLANI NA MUUNGA MKONO YULE DADA


ZAMA ZETU HIZI, WANAUME HATUSEMWI KWA MAZURI. TUNAONEKANA MSHETANI, MBWA, WATU KATILI!
ANGALAU HUYU KATI YA MILIONI 5O KAWEZA SIMAMA HADHARANI NA KUSEMA UKWELI.

Hakuna kitu hapo
 
Muda mwingine waja tunaweza hisi labda dada amemfanyia kosa kubwa kaka anajikosha au anataka awakomeshe wanaonyemelea au waliokwisha kula asali yake [emoji28][emoji28]
Badala ya kuwakomesha hapo ndio anawatangazia wanawake kwamba huyu jamaa anafaa kwa matumizi ya binadamu. Jamaa ashindwe mwenyewe tu maana saiz atakua anatafutwa analetewa mpaka mlangoni 😀
 
Kumuweka Mpenzi wako kwenye Mabango ni Ulimbukeni tu na Ushamba
Hiv unaweza kumpenda mtu kiasi kwamba unambandika kwenye mabango duh
Mkuu umekosea ni hivii kumbandika mpenzio ktk billboard sio ushahidi ya kwamba ndio unampenda kwa sababu wapo ambao walichorana hata ktk ngozi (tatoo) na bado uaminifu ni ZEROOO
 
Back
Top Bottom