- Source #1
- View Source #1
Kumekuwepo Chapisho linalosambazwa kwenye mitandao ya kijamii, ikiwemo Facebook na Instagram, linadai kuwa Zambia ilisajili wapiga kura milioni 14 na kwamba katika uchaguzi huo zaidi ya watu milioni 14 walipiga kura.
- Tunachokijua
- Chapisho hilo limekuja mara baada ya kuhusanisha chapisho la peter msigwa ambaye alikuwa anahoji juu ya mda ambao tume ya uchaguzi nchini zambaia imetumia katika kuhesabu na kutangaza kura hadi kufikia mchakato kukamilika huku akihusisha kwa namna ambavyo mchakato ulifanyika nchini tanzania
Katika kufuatilia zaidi kwa kutumia njia utafutaji wa maneno kupitia Takwimu rasmi kutoka Tume ya Uchaguzi ya Zambia (ECZ) zinaonyesha kuwa jumla ya wapiga kura waliosajiliwa nchini humo ilikuwa 8,786,300, si milioni 14
Kwa mujibu wa takwimu hizo, wanawake walikuwa 4,665,431, huku wanaume wakiwa 4,120,869.
Takwimu za Tume ya Uchaguzi ya Zambia ECZ zinaonyesha kuwa nchi hiyo ilikuwa na majimbo 10, wilaya 116, kata 1,858, vituo vya kupigia kura 13,529 na majimbo ya uchaguzi 226.
Kwa mujibu wa matokeo hayo ya mwisho Hichilema alipata kura 2,965,326, sawa na asilimia 60.49, dhidi ya kura 1,856,217, sawa na asilimia 37.87, alizopata mpinzani wake Brian Mundubile.
Chapisho linachanganya au kupotosha takwimu za wapiga kura nchini Zambia. Takwimu rasmi zinaonyesha kuwa wapiga kura waliosajiliwa walikuwa 8,786,300.