Hiyo safi sana wala isikussubuwe kabisa, mimi naamini kwenye ushindani wa biashar ndipo kunazaa ubora wa huduma.
Sisi kwa upande wa Zambia, tumeliua wenyewe soko kuanzia bandarini, reli, barabara mpaka pale Tunduma,
Hao wametuheshimu sana kuvumilia yote hayo kwa miaka mingi sana. Ukiitazama TAZARA utafikiri imepigwa bomu, ukiitazama bandari hohehahe. Ukienda Tunduma kama nidereva wa kutoka nchi za nje basi huna hamu ya kurudia tena njia za Tanzania.
Ukija kutazama madereva wa IT wanaokuja kuchukuwa gari zao Dar. Hao ndiyo kabisa hawana hamu, wanacheleweshewa kutoa magari, yanaibiwa vifaa yakiwa bandarini, wanasumbuliwa na mapolisi njia nzima, kila sehemu kukaguliwa, na hakuna cha kukaguliwa bali ni lazima watowe posho ya kusafisha viatu.
Binafsi nawapongeza sana kwa uamuzi huo.
Kama wanavyosema wengine humu, kuwa mizigo yetu ya Tanzania tu inatutisha, ni heri tubaki kuwa omba-omba wa bajeti yetu kwa wazungu kuliko kuwa na sisi na ubora wa kuwaajiri wazungu.
Heko sana Watanzania wazalendo, tutapakia kwenye tazara mzigi wetu wenyewe. Tutatumia bandari yetu kwa meli zetu wenyewe. Kwani tataizo nini? Si wazungu wanatulisha? Waende zao haraka sana, wasitunyanyase.
Kwa upande wa Zambia na Congo nawaunga mkono, maana hapa mpaka shaba zenu zilikuwa zinaibiwa. Abiria chunga mzigo wako.