Zambia: Rais Hakainde Hichilema awataka Watumishi wa Serikali wanaotaka VX wajinunulie kwa pesa zao

Zambia: Rais Hakainde Hichilema awataka Watumishi wa Serikali wanaotaka VX wajinunulie kwa pesa zao

MURUSI

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2013
Posts
4,537
Reaction score
8,824
Rais wa Zambia Hakainde Hichilema amewataka Watumishi wa Serikali wanaotaka wapewe magari ya kifahari aina ya Toyota Land Cruiser VX kwa ajili ya kuyatumia kwenye kazi wasahau hilo na kama wanaona yana umuhimu sana basi wajinunulie wao lakini sio kwa pesa za Serikali.

Hichilema amehoji “Kwanini mnatumia pesa kumnunulia Meya VX? hiyo pesa ya kumnunulia Meya VX inaweza kuweka vyoo katika masoko yote kwenye miji yenu, piteni katika mstari huo. Meya bado anaweza kuendesha gari zuri kama vile Hilux double cabin sio lazima gari liwe VX, mkitaka kuendesha VX nunueni kwa pesa zenu”

Kwa upande mwingine Rais huyu ambaye hakutaka kupokea mshahara wa Urais kwa miezi nane akisema kilichomsukuma kuingia madarakani sio pesa bali uzalendo wa kuijenga Nchi yake, aliwataka pia Watumishi wa Serikali wanaotaka kuongezewa mishahara wafikirie Wananchi ambao wanateseka kabla ya kutaka nyongeza hiyo "Unapoona mshahara unaingia kwenye akaunti yako ya benki kumbuka ni Mama Mjane amenilipa mshahara huu kwa hiyo kabla ya kuomba nyongeza jiulize vipi kuhusu yule anayekulipa mshahara wako wa sasa? Mtoto wake anakaa chini darasani.” Hakainde Hichilema.

Kwa Tanzania hii kitu haipo, make tutambue kwanza Zambia Raia wao wanajitambua tofauti na Tanzania ambako CCM inaongoza. Viongozi Tanzania hawawezi fanya kama Zambia kwa sababu kwanza wanaongoza wajinga hii inafanyika kwenye nchi yenye watu wenye akili.

 
Haikande anatakiwa 'apelekwe' tuition.

Anatakiwa ajifunze kwa kina Nyerere kuwa ujima na ujamaa ulifeli.

Aache watumishi wa umma waishi kulingana na hadhi na stahiki zao.

Anaye stahili V8, aache stembelee V8.

Sera za dhiki na kuendekeza umaskini hazitamsogeza hata hatua moja katika utawala wake.

The World has moved out and away of austerity..
 
Hili jambo ni gumu sana.

Hivi kwani wale macho madogo watakubali huu ulaji uwaponyoke??

Manunuzi na maintenance za kila mwezi.

Ni bilions za pesa ya Nyerere.
 
Mabadiliko ya Zambia au Malawi hayakuletwa na vyama vya siasa bali wananchi.

Watanzania akili zetu zimedumaa, tunawategemea wanasiasa kwa kila kitu... Yaani sijui Chadema hapa mara CCM pale... Ooh hao nyumbu sijui wengine buku saba. Hii inasaidia nini kwenye maendeleo ya mtu mmoja mmoja na ya nchi kwa ujumla?

Watanzania tumefitinishwa na wanasiasa na tumefitinika kweli kweli.

Kama hatutaacha tabia ya "sifia sifia" viongozi hatutafanikiwa kujitoa kwenye huu udumavu.
 
Huyu ni mzalendo wa kweli Kwa Taifa lake. Kuna siku niliwaza Sana haya magari ya V8, gari linakwenda kumchukua jaji /mkurugenzi Mbezi linakwenda Kisutu/posta na linakaa kwenye foleni likitafuna wese. Yakiruhusiwa yanafatana sawa tu na ki ist. Iko haj ya kubana matumizi pesa ziende kwenye miundo mbinu ya wananchi, maji afya na Elimu.
 
Na gharama za matengezo ya hizo gari zinatoka serikalini?
 
Wewe unafuatilia mambo ya Nchi ya Zambia kuliko mambo ya Nchi yako au laa utakuwa ni raia harafu wa Zambia.

Sasa kwa Taarifa yako Serikali ilitangaza Bungeni kuwakopesha magari watumishi wake Ili wayahusumie wenyewe na kuwapimia mafuta.

Waziri wa Fedha Amesema hatua hizo zita cut expenditure ya serikali kutoka bil.554 kubakia Bilioni 54 tuu.

Angalizo,jambo hili halitafanywa overnight Bali hatua kwa hatua.
 
Yuko sahihi His Excellency Hichilema. Kuna msafara wa Rais niliushuhudia mahali hadi leo naota maruweruwe kwa yale madude ya ajabu niliyoshuhudia.
Halafu wakute jukwaani sasa wanavyo lia macho ya Mamba,
 
Mabadiliko ya Zambia au Malawi hayakuletwa na vyama vya siasa bali wananchi.

Watanzania akili zetu zimedumaa, tunawategemea wanasiasa kwa kila kitu... Yaani sijui Chadema hapa mara Ccm pale... Ooh hao nyumbu sijui wengine buku saba... Hii inasaidia nini kwenye maendeleo ya mtu mmoja mmoja na ya nchi kwa ujumla?

Watanzania tumefitinishwa na wanasiasa na tumefitinika kweli kweli.

Kama hatutaacha tabia ya "sifia sifia" viongozi hatutafanikiwa kujitoa kwenye huu udumavu.
Kabisa, sisis tunazania Mbowe, Lisu au Zitto ndio wataleta mabadiliko, kwa kifupi Dunia nzima mabadiliko yaliletwa na Raia sasa Tanzania tunataka yaletwe na individual.
 
Wewe unafuatilia mambo ya Nchi ya Zambia kuliko mambo ya Nchi yako au laa utakuwa ni raia harafu wa Zambia..

Sasa kwa Taarifa yako Serikali ilitangaza Bungeni kuwakopesha magari watumishi wake Ili wayahusumie wenyewe na kuwapimia mafuta..

Waziri wa Fedha Amesema hatua hizo zita cut expenditure ya serikali kutoka bil.554 kubakia Bilioni 54 tuu..

Angalizo,jambo hili halitafanywa overnight Bali hatua kwa hatua.
Hio haiwezekani
 
Kwa Tanzania hii kitu haipo, make tutambue kwanza Zambia raia wao wanajitambua tofauti na Tanzania ambako CCM inaongoza maiti/ mazezeta. Viongozi Tanzania hawawezi fanya huo ujinga wa Zambia kwa sababu kwanza wanaongoza wajinga hii inafanyika kwenye nchi yenye watu wenye akili.
Hapa umewatukana Watz wenzako.
 
Back
Top Bottom