Rais wa Zambia Hakainde Hichilema amewataka Watumishi wa Serikali wanaotaka wapewe magari ya kifahari aina ya Toyota Land Cruiser VX kwa ajili ya kuyatumia kwenye kazi wasahau hilo na kama wanaona yana umuhimu sana basi wajinunulie wao lakini sio kwa pesa za Serikali.
Hichilema amehoji “Kwanini mnatumia pesa kumnunulia Meya VX? hiyo pesa ya kumnunulia Meya VX inaweza kuweka vyoo katika masoko yote kwenye miji yenu, piteni katika mstari huo. Meya bado anaweza kuendesha gari zuri kama vile Hilux double cabin sio lazima gari liwe VX, mkitaka kuendesha VX nunueni kwa pesa zenu”
Kwa upande mwingine Rais huyu ambaye hakutaka kupokea mshahara wa Urais kwa miezi nane akisema kilichomsukuma kuingia madarakani sio pesa bali uzalendo wa kuijenga Nchi yake, aliwataka pia Watumishi wa Serikali wanaotaka kuongezewa mishahara wafikirie Wananchi ambao wanateseka kabla ya kutaka nyongeza hiyo "Unapoona mshahara unaingia kwenye akaunti yako ya benki kumbuka ni Mama Mjane amenilipa mshahara huu kwa hiyo kabla ya kuomba nyongeza jiulize vipi kuhusu yule anayekulipa mshahara wako wa sasa? Mtoto wake anakaa chini darasani.” Hakainde Hichilema.
Kwa Tanzania hii kitu haipo, make tutambue kwanza Zambia Raia wao wanajitambua tofauti na Tanzania ambako CCM inaongoza. Viongozi Tanzania hawawezi fanya kama Zambia kwa sababu kwanza wanaongoza wajinga hii inafanyika kwenye nchi yenye watu wenye akili.
Mabadiliko ya Zambia au Malawi hayakuletwa na vyama vya siasa bali wananchi.
Watanzania akili zetu zimedumaa, tunawategemea wanasiasa kwa kila kitu... Yaani sijui Chadema hapa mara CCM pale... Ooh hao nyumbu sijui wengine buku saba. Hii inasaidia nini kwenye maendeleo ya mtu mmoja mmoja na ya nchi kwa ujumla?
Watanzania tumefitinishwa na wanasiasa na tumefitinika kweli kweli.
Kama hatutaacha tabia ya "sifia sifia" viongozi hatutafanikiwa kujitoa kwenye huu udumavu.
Huyu ni mzalendo wa kweli Kwa Taifa lake. Kuna siku niliwaza Sana haya magari ya V8, gari linakwenda kumchukua jaji /mkurugenzi Mbezi linakwenda Kisutu/posta na linakaa kwenye foleni likitafuna wese. Yakiruhusiwa yanafatana sawa tu na ki ist. Iko haj ya kubana matumizi pesa ziende kwenye miundo mbinu ya wananchi, maji afya na Elimu.
Mabadiliko ya Zambia au Malawi hayakuletwa na vyama vya siasa bali wananchi.
Watanzania akili zetu zimedumaa, tunawategemea wanasiasa kwa kila kitu... Yaani sijui Chadema hapa mara Ccm pale... Ooh hao nyumbu sijui wengine buku saba... Hii inasaidia nini kwenye maendeleo ya mtu mmoja mmoja na ya nchi kwa ujumla?
Watanzania tumefitinishwa na wanasiasa na tumefitinika kweli kweli.
Kama hatutaacha tabia ya "sifia sifia" viongozi hatutafanikiwa kujitoa kwenye huu udumavu.
Kabisa, sisis tunazania Mbowe, Lisu au Zitto ndio wataleta mabadiliko, kwa kifupi Dunia nzima mabadiliko yaliletwa na Raia sasa Tanzania tunataka yaletwe na individual.
Kwa Tanzania hii kitu haipo, make tutambue kwanza Zambia raia wao wanajitambua tofauti na Tanzania ambako CCM inaongoza maiti/ mazezeta. Viongozi Tanzania hawawezi fanya huo ujinga wa Zambia kwa sababu kwanza wanaongoza wajinga hii inafanyika kwenye nchi yenye watu wenye akili.
Hiyo bado, angetumia mabasi na malori ya jeshi, kuwe na kituo maalum wanakusanyika saa moja asubuhi kuendeshwa kazini na ambaye atachelewa apigishwe kwata na viboko juu.