Zanzibar: Aliyechukuliwa na Polisi kwa ajili ya Mahojiano akutwa ameuawa

"Kuna kitu kinaitwa legacy au urithi"

Kwa hii comment yako ulikuwa una maanisha nini hasa mbwea wewe??

Kwamba haya mauaji yanayoendelea ni legacy iliyoachwa na mtangulizi wa Samia na hatupaswi kushangaaa Wala kumlaumu kivyovyote vile? Na kwanini aendeleze legacy ya kipumbavu hivi ilihali legacies zingine mbaya zote ameshaziondoa?
Use your brain.

Kupayuka wakati hujaelewa kitu ni ujinga mkubwa sana mithili ya upumbavu. Ungeuliza ningekuelewesha vizuri tu.
 
Intelijensia ya polisi hapa imefeli.Ila ingegundua haraka sana CDM kuandamana
 
Uzi una likes 11, watu wanaroho ngumu sana.
 
“Tukio hilo lipo uchunguzi bado unaendelea, tukikamilisha tutaeleza zaidi,” amesema Mchomvu.

Mwananchi
Ni taarifa hii iliyo fanya na wao Mwanachi wafungiwe, au kuna mengine?

Hawa ndugu hawaelezi chochote, wanalia tu. Huyo ndugu yao alikuwa akijihusisha na mambo gani ambayo pengine ndiyo yaliyo sababisha mkasa huu umpate?
 
Hii ndio Taarifa Mpya kutoka Mwananchi
---
View attachment 3113434
Ramadhan Iddi Shaaban anayedaiwa kutekwa na kuuawa kikatili enzi za uhai wake

Familia ya Ramadhan anayedaiwa kutekwa, kuuawa kikatili yamlilia Rais Mwinyi. Mama yake asema ana hofu na usalama wake.

“Mwanangu ameuawa, kifo cha kikatili naomba haki itendeke waliofanya hivi wachunguzwe, ni kweli kifo kipo lakini sio cha namna hii…”

Hii ni kauli ya Saada Ramadhan Mwendwa mama mzazi wa Ramadhan Idd Shaaban (48) akianza kusimulia jinsi mwanaye alivyochukuliwa na watu waliojitambulisha ni askari wakidai wanakwenda kufanya mahojiano naye lakini aliokotwa akiwa amefariki dunia eneo la Mbuzini, Kijichi - Unguja.

Kwa kipindi cha hivi karibuni matukio ya watu kutekwa, kupigwa, kuumizwa na kuuawa yameshika kasi kwa upande wa Tanzania Bara, hata hivyo kwa Zanzibar hayajawahi kusikika.

Kwa tukio la karibuni zaidi ni lile la Mjumbe wa Sekretarieti ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Ali Kibao ambaye alichukuliwa kwenye gari Septemba 6, 2024 akitoka Dar es Salaam kwenda Tanga na mwili wake uliokotwa Ununio uso wake ukiwa umeharibika kiasi cha kutotambulika.

Akisumulia, mama huyo huku akitokwa na machozi, Saada ametumia fursa hiyo kumuomba Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama kuchunguza tukio hilo na waliofanya hivyo wachukuliwe hatua.

Akisimulia mkasa huo nyumbani kwake Chumbuni Oktoba 2, 2024 Saada amesema mwanaye alichukuliwa Septemba 24, 2024 saa 12:00 jioni lakini mwili wake uliokotwa kesho yake Septemba 25 ukiwa umeunguzwa, jicho moja limetobolewa na ulimi umetoka nje ambapo uchunguzi wa Polisi ulieleza kuwa ameuawa.

“Siku hiyo mwanangu alikwenda kutembea jioni eneo la Amani Baa, saa 12:00 za jioni walikuja vijana watano wakamfuata alipokuwa amekaa na kumuita kwa jina wakasema wana shida naye waende nje wakazungumze wakidai wao ni askari na wana RB wanamtafuta.

“Walipanda naye kwenye gari wakamwambia wanampeleka Polisi Mwanakwerekwe lakini walipofika walipitiliza. Saada anasema mwanaye alikuwa na rafiki yake ambaye aliongozana naye kwenda kituo cha Polisi ila baada ya kupitiliza alipohoji mbona wamepita walimshusha.

“Walichokifanya ndio hicho kilichotokea, wamempiga mwanangu wamemuunguza moto kwa shoti za umeme na kumtoboa jicho moja la kulia," amesimulia akieleza kifo cha mwanaye wa kwanza ambaye ameacha mjane na watoto wanne.

Anasema usiku wa siku hiyo mke wake Shaaban alipiga simu baada ya kuona mumewe hajarejea lakini kuna mtu alipokea simu hiyo akasema asiwe na wasiwasi bado anahojiwa na askari akimaliza atarejea nyumbani.

Baada ya kuambiwa hivyo, alitulia lakini kadri muda ilivyoendelea akawa anaingiwa zaidi na wasiwawasi ndipo alinipigia mimi simu akisema kuna muda alimpigia askari wakasema bado wapo naye lakini mpaka sasa hajarejea.

“Baadaye mimi nilipiga simu ikawa haipatikani nikaanza kumtumia meseji, mwanangu upo wapi mbona hujarudi baba, simu haipatikani nikajua ujumbe unaingia kumbe matokeo yake wameshampiga na kumfanyia ukatili huo,” amesema.

Amesema walipoamka asubuhi Septemba 25 walienda kutoa taarifa katika vituo vitatu vya polisi.

Hata hivyo, amesema anashukuru polisi kwani walionesha jitihada za kupiga simu katika vituo vingi kuulizia iwapo kuna mtu wa namna hiyo lakini majibu yalikuwa hapana.

Akiendelea kusimulia, Saada amesema ulipofika mchana alipigiwa simu na mwanawe mkubwa kuwa kuna maiti imeokotwa katika njia ya Mbuzini - Kijichi akiwa na vitambulisho na limeonekana kuna jina la Ramadhani Iddi na walipokwenda katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Mnazi Mmoja wakakuta ni yeye.

“Mdomo ulikuwa wazi, jicho limetumbuliwa na mwili wote umechomwa chomwa, ila niliwaambia wanangu tufanye utaratibu kuchukua maiti,” amesema.

“Kwa kweli kilichotokea kwa mwanangu naomba sana, serikali yangu ni sikivu ya Zanzibar na inatupenda wananchi wanyonge, kwa hili nataka isikie kilio changu waliofanya ukatili huu aliyefanya ukatili huu wapatikane haki itendeke,” amesema na kuongeza.

“Mwanagu kaonewa…, kapata mateso ndani ya nafsi yake, kwasababu unapotiwa moto kila mtu anajua, kama ni kifo kila mtu atakufa lakini sio kwa kifo kile, naomba serikali ichukue hatua haina uonevu watu wote ni watu wake, tumeumia familia hatuna pa kulilia serikai ina mkono mrefu itawapata waliofanya kitendo hiki sheria ni kwa watu wote,” amesisitiza.

Saada amesema ameshakuwa na woga hata kwa watoto wake wengine kwasababu hajui kilichofanywa mwanaye kuuawa.

“Sasa sijui kama litaishia kwa Ramadhan au mimi mwenyewe au watoto wangu wengine hadi wajukuu zangu wangu kwakweli tunakosa amani.”

Mama mdogo wa marehemu, Yunes Kitarao amesema jambo hilo linawasikitisha na kuwaumiza kwanini auawe kwa ukatili wa namna ile.

“Kwanini mtu atekwe, anaambiwa anachukuliwa na askari na wanasema yupo katika mikono salama watamrudisha na kwanini hakurudishwa akiwa mzima, dhamira hiyo imeniumiza sana, mtoto wa dada yangu, sijawahi kusikia amegombana wala kutukanana na mtu,” amesema Yunes.

Amesema mambo hayo yamekuwa yakitendeka maeneo mengine, sasa na Zanzibar yameanza.

“Haya yanayotukuta ni makubwa, tunachokiomba hawa watu wakamatwe mbona majambazi yanakamatwa, liwe fundisho, bila kufanya hivyo hili jambo litaendelea hata kama sio kwa familia hii lakini kwa wananchi wengine,” amesema huku akipeleka kilio hicho kwa viongozi wakuu wa nchi.

Mjomba wa marehemu ambaye hakutaka jina lake litajwe, amesema kinachowasikitisha zaidi watu hao kujitambulisha wametoka kwenye vikosi na simu ilipopigwa wakajibiwa yupo kwenye mikono salama halafu wakaokota maiti.

Akizungumza na Mwananchi kuhusu tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Richard Mchomvu bila kufafanua zaidi amesema wanaendelea na upelelezi wa tukio hilo na ukikamilika zitatolewa taarifa zaidi.

Kuna taasisi zinahitaji reforms. Hii inazidi kuonyesha uozo na kujiondolea uhalali wa kufanya kazi ambazo kisheria wanatakiwa kuzifanya
 
Ni taarifa hii iliyo fanya na wao Mwanachi wafungiwe, au kuna mengine?

Hawa ndugu hawaelezi chochote, wanalia tu. Huyo ndugu yao alikuwa akijihusisha na mambo gani ambayo pengine ndiyo yaliyo sababisha mkasa huu umpate?

Kuuwawa na baadae mwili kuokotwa! Hiyo kisheria kuna taasisi yoyote inayoruhusiwa kufanya hivyo? Tena baada ya kukamatwa? Ukishakamatwa, halafu ukaokotwa umeuwawa, inaleta ukakasi.
Kwa lolote lile alilokuwa analifanya, kwanini akamatwe na baadae kuuwawa. Labda waliomkamata ni yale magenge ya kihalifu ya Haiti
 
Hatujui, bali kila mhalifu anapaswa kufikishwa Mahakamani, hii ni kwa mujibu wa sheria za Tanzania
 
SSH tafadhali warudishe gerezani wale masheikh magaidi.
 
Huyo marehemu alikuwa anajishugulisha na nini??
Au naye alikuwa mwanaharakati

Ova
 
Kuuwawa na baadae mwili kuokotwa! Hiyo kisheria kuna taasisi yoyote inayoruhusiwa kufanya hivyo? Tena baada ya kukamatwa? Ukishakamatwa, halafu ukaokotwa umeuwawa, inaleta ukakasi.
Kwa lolote lile alilokuwa analifanya, kwanini akamatwe na baadae kuuwawa. Labda waliomkamata ni yale magenge ya kihalifu ya Haiti
Mimi sijatetea chochote hapo kuhusu yaliyo tokea; sasa sijui wewe umenielewaje hadi kuandika haya.

Hivi taarifa inaeleza kakamatwa na akina nani mkuu 'Tangawizi', unajuwa?

Kama ndugu, ama wengine wanao mfahamu marehemu wange dokeza tu aina ya shughuli zake au msimamo wake katika baadhi ya maswala, kidogo ingesaidia kujuwa tatizo lilipo, hadi kusababisha kupoteza maisha, tena kikatiri vile; na wanaotiliwa mashaka katika tukio hili wangeanza kudhaniwa.

Lakini pamoja na hayo yote, serikali na vyombo vyake vina wajibu wa kulinda usalama wa kila raia; na kama raia anayo makosa kuna sheria zinazotakiwa kufuatwa kumtia hatiani, na siyo kuondoa uhai wake.

Kinacho onekana wazi katika matukio ya namna hii kipo wazi. Ni jitihada za kuwatia hofu na woga wananchi; wasihoji chochote kinacho fanywa na serikali.
Ni maandalizi ya kuchukua madaraka kwa nguvu hiyo 2025.
 
Hatujui, bali kila mhalifu anapaswa kufikishwa Mahakamani, hii ni kwa mujibu wa sheria za Tanzania
Na wewe bado unaamini kuwa kuna sheria zinazo heshimiwa na serikali ya Tanzania?
Uwepo wa maandamano, hakuna sheria inayo ruhusu jambo hilo?

Mkuu 'Erythro' mbona unanishangaza kwa maneno yako haya!

Sheria pekee iliyo baki, ambayo serikali na Chama chake wanayo ifuata sasa hivi ni kuhakikisha 2025 wanaendelea kuwepo madarakani. Kama wewe hili bado hulioni, utakuwa umebaki nyuma sana.
 
Hii ndio Taarifa Mpya kutoka Mwananchi
---
View attachment 3113434
Ramadhan Iddi Shaaban anayedaiwa kutekwa na kuuawa kikatili enzi za uhai wake

Familia ya Ramadhan anayedaiwa kutekwa, kuuawa kikatili yamlilia Rais Mwinyi. Mama yake asema ana hofu na usalama wake.

“Mwanangu ameuawa, kifo cha kikatili naomba haki itendeke waliofanya hivi wachunguzwe, ni kweli kifo kipo lakini sio cha namna hii…”

Hii ni kauli ya Saada Ramadhan Mwendwa mama mzazi wa Ramadhan Idd Shaaban (48) akianza kusimulia jinsi mwanaye alivyochukuliwa na watu waliojitambulisha ni askari wakidai wanakwenda kufanya mahojiano naye lakini aliokotwa akiwa amefariki dunia eneo la Mbuzini, Kijichi - Unguja.

Kwa kipindi cha hivi karibuni matukio ya watu kutekwa, kupigwa, kuumizwa na kuuawa yameshika kasi kwa upande wa Tanzania Bara, hata hivyo kwa Zanzibar hayajawahi kusikika.

Kwa tukio la karibuni zaidi ni lile la Mjumbe wa Sekretarieti ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Ali Kibao ambaye alichukuliwa kwenye gari Septemba 6, 2024 akitoka Dar es Salaam kwenda Tanga na mwili wake uliokotwa Ununio uso wake ukiwa umeharibika kiasi cha kutotambulika.

Akisumulia, mama huyo huku akitokwa na machozi, Saada ametumia fursa hiyo kumuomba Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama kuchunguza tukio hilo na waliofanya hivyo wachukuliwe hatua.

Akisimulia mkasa huo nyumbani kwake Chumbuni Oktoba 2, 2024 Saada amesema mwanaye alichukuliwa Septemba 24, 2024 saa 12:00 jioni lakini mwili wake uliokotwa kesho yake Septemba 25 ukiwa umeunguzwa, jicho moja limetobolewa na ulimi umetoka nje ambapo uchunguzi wa Polisi ulieleza kuwa ameuawa.

“Siku hiyo mwanangu alikwenda kutembea jioni eneo la Amani Baa, saa 12:00 za jioni walikuja vijana watano wakamfuata alipokuwa amekaa na kumuita kwa jina wakasema wana shida naye waende nje wakazungumze wakidai wao ni askari na wana RB wanamtafuta.

“Walipanda naye kwenye gari wakamwambia wanampeleka Polisi Mwanakwerekwe lakini walipofika walipitiliza. Saada anasema mwanaye alikuwa na rafiki yake ambaye aliongozana naye kwenda kituo cha Polisi ila baada ya kupitiliza alipohoji mbona wamepita walimshusha.

“Walichokifanya ndio hicho kilichotokea, wamempiga mwanangu wamemuunguza moto kwa shoti za umeme na kumtoboa jicho moja la kulia," amesimulia akieleza kifo cha mwanaye wa kwanza ambaye ameacha mjane na watoto wanne.

Anasema usiku wa siku hiyo mke wake Shaaban alipiga simu baada ya kuona mumewe hajarejea lakini kuna mtu alipokea simu hiyo akasema asiwe na wasiwasi bado anahojiwa na askari akimaliza atarejea nyumbani.

Baada ya kuambiwa hivyo, alitulia lakini kadri muda ilivyoendelea akawa anaingiwa zaidi na wasiwawasi ndipo alinipigia mimi simu akisema kuna muda alimpigia askari wakasema bado wapo naye lakini mpaka sasa hajarejea.

“Baadaye mimi nilipiga simu ikawa haipatikani nikaanza kumtumia meseji, mwanangu upo wapi mbona hujarudi baba, simu haipatikani nikajua ujumbe unaingia kumbe matokeo yake wameshampiga na kumfanyia ukatili huo,” amesema.

Amesema walipoamka asubuhi Septemba 25 walienda kutoa taarifa katika vituo vitatu vya polisi.

Hata hivyo, amesema anashukuru polisi kwani walionesha jitihada za kupiga simu katika vituo vingi kuulizia iwapo kuna mtu wa namna hiyo lakini majibu yalikuwa hapana.

Akiendelea kusimulia, Saada amesema ulipofika mchana alipigiwa simu na mwanawe mkubwa kuwa kuna maiti imeokotwa katika njia ya Mbuzini - Kijichi akiwa na vitambulisho na limeonekana kuna jina la Ramadhani Iddi na walipokwenda katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Mnazi Mmoja wakakuta ni yeye.

“Mdomo ulikuwa wazi, jicho limetumbuliwa na mwili wote umechomwa chomwa, ila niliwaambia wanangu tufanye utaratibu kuchukua maiti,” amesema.

“Kwa kweli kilichotokea kwa mwanangu naomba sana, serikali yangu ni sikivu ya Zanzibar na inatupenda wananchi wanyonge, kwa hili nataka isikie kilio changu waliofanya ukatili huu aliyefanya ukatili huu wapatikane haki itendeke,” amesema na kuongeza.

“Mwanagu kaonewa…, kapata mateso ndani ya nafsi yake, kwasababu unapotiwa moto kila mtu anajua, kama ni kifo kila mtu atakufa lakini sio kwa kifo kile, naomba serikali ichukue hatua haina uonevu watu wote ni watu wake, tumeumia familia hatuna pa kulilia serikai ina mkono mrefu itawapata waliofanya kitendo hiki sheria ni kwa watu wote,” amesisitiza.

Saada amesema ameshakuwa na woga hata kwa watoto wake wengine kwasababu hajui kilichofanywa mwanaye kuuawa.

“Sasa sijui kama litaishia kwa Ramadhan au mimi mwenyewe au watoto wangu wengine hadi wajukuu zangu wangu kwakweli tunakosa amani.”

Mama mdogo wa marehemu, Yunes Kitarao amesema jambo hilo linawasikitisha na kuwaumiza kwanini auawe kwa ukatili wa namna ile.

“Kwanini mtu atekwe, anaambiwa anachukuliwa na askari na wanasema yupo katika mikono salama watamrudisha na kwanini hakurudishwa akiwa mzima, dhamira hiyo imeniumiza sana, mtoto wa dada yangu, sijawahi kusikia amegombana wala kutukanana na mtu,” amesema Yunes.

Amesema mambo hayo yamekuwa yakitendeka maeneo mengine, sasa na Zanzibar yameanza.

“Haya yanayotukuta ni makubwa, tunachokiomba hawa watu wakamatwe mbona majambazi yanakamatwa, liwe fundisho, bila kufanya hivyo hili jambo litaendelea hata kama sio kwa familia hii lakini kwa wananchi wengine,” amesema huku akipeleka kilio hicho kwa viongozi wakuu wa nchi.

Mjomba wa marehemu ambaye hakutaka jina lake litajwe, amesema kinachowasikitisha zaidi watu hao kujitambulisha wametoka kwenye vikosi na simu ilipopigwa wakajibiwa yupo kwenye mikono salama halafu wakaokota maiti.

Akizungumza na Mwananchi kuhusu tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Richard Mchomvu bila kufafanua zaidi amesema wanaendelea na upelelezi wa tukio hilo na ukikamilika zitatolewa taarifa zaidi.

“Tukio hilo lipo uchunguzi bado unaendelea, tukikamilisha tutaeleza zaidi,” amesema Mchomvu.

Mwananchi
Hili jambo la kutekana nahisi linawahusu wafanya biashara za madawaya kulevya. Polisi wanasingiziwa tu na wanasiasa wanadakia kufaidika na siasa zao za upinzani. Wanaotekwa wala sio wanasiasa wakubwa wa upinzani hadi wapinzani kurukia eti wanatekwa watu wao. Kanuni ya washiriki wa biashara ya madawa ya kulevya ukidhulumu au kutoa siri wanakula kichwa chako. Vinginevyo huu ni mzimu gani wa kutekana? Kule DRC kuna ADF kinajidaini chama cha kidini kueneza uislaam kwa nguvu lakini kwa hakika ni wauaji kwa biashara za madini na magendo. M23 nao ni wavamizi kuteka maeneo ili waibe madini. Nachotaka kusema vyombo vya usalama viwajibike maana kama wao wanatumiwa na wahalifu nchi itavurugika kabisa jambo ambalo pengine ndio nia ya adui zetu kama taifa.
 
Na wewe bado unaamini kuwa kuna sheria zinazo heshimiwa na serikali ya Tanzania?
Uwepo wa maandamano, hakuna sheria inayo ruhusu jambo hilo?

Mkuu 'Erythro' mbona unanishangaza kwa maneno yako haya!

Sheria pekee iliyo baki, ambayo serikali na Chama chake wanayo ifuata sasa hivi ni kuhakikisha 2025 wanaendelea kuwepo madarakani. Kama wewe hili bado hulioni, utakuwa umebaki nyuma sana.
Nakuelewa sana lakini na wewe uwe unanielewa
 
Back
Top Bottom