The piece of a plane wingairline found today in the Indian Ocean on the island of Kojani, Pemba - Zanzibar off coast of Tanzania.
It is believed to be Part of the Missing Malaysia Airlines Flight MH370 and investigation is ongoing.
Transport Minister Darren Chester said the Australian Transport Safety Bureau was seeking further information on the item, which was discovered on Pemba Island.
Several pieces of debris that authorities say are almost certainly from the plane have been recovered during the past year on the shorelines of South Africa, Mozambique, and Rodrigues and Reunion islands.
======
Bawa kubwa la ndege limeokotwa na wananchi leo katika Bahari ya Hindi kwenye Kisiwa cha Kojani, Pemba. Haijafahamika ni la ndege ya shirika gani.
Sehemu ambayo inaaminika ni mabaki ya ndege imevuliwa katika bahari ya hindi katika ufukwe wa kisiwa cha kojani pemba.
Bawa la ndege lililopatikana katika bahari ya kisiwa kidogo cha kojani huko kisiwani pemba zanzibar, yamezusha mjadala mkubwa miongoni mwa wakazi wa kisiwa hicho huku wengi wakiamini ni bawa la ndege ya malaysia ambayo ilipotea bila kujuilikana hatima yake. Ndege ya shirika la Malaysia Airlines yenye chapa MH370, iliotoweka Machi 8 mwaka 2014 haijawahi onekana hadi leo.
Ingawa bado hakuna uhakika ni mabaki ya ndege gani, wataalamu wa usafiri wa anga wamenza hatua ya awali ya uchunguzi wa mabaki hayo ya ndege.
Taarifa zinasema tayari maofisa wa usalama wameanza kulifanyia uchunguzi bawa hilo na huenda si muda mrefu tukapata maelezo ya kutosha kutoka vyombo vinavyohusika
View attachment 359349 View attachment 359350 View attachment 359351
More images (June 24, 2016)
View attachment 359673
View attachment 359674
View attachment 359675
View attachment 359676
Australia imetangaza kuanza uchunguzi wa mabaki ya ndege yaliyogunduliwa kwenye kisiwa kidogo cha Kojani, visiwani Zanzibar, kutambuwa endapo ni ya ndege ya Malaysia, nambari MH370, ambayo ilipotea Machi mwaka 2014, ikiwa na watu 239. Waziri wa Usafirishaji wa Australia, Darren Chester, hakutoa maelezo zaidi kuhusu mabaki hayo, lakini mwanzoni mwa mwezi huu, wavuvi kwenye kisiwa cha Kojani waligundua kile wanachoeleza kuwa ni bawa la ndege, ambalo bado linaendelea kushikiliwa huko.
Waziri Chester amesema tayari mamlaka nchini Malaysia zimefanya mawasiliano na wenzao wa Tanzania kupanga namna ya kuyachunguza mabaki hayo. Mwezi Mei, vipande vyengine vinavyokisiwa kuwa mabaki ya ndege hiyo, viliokotwa kwenye visiwa vya Reuniun na Mauritius. Australia inaendesha operesheni kubwa kuisaka ndege hiyo kwenye eneo la kusini mwa Bahari ya Hindi lenye ukubwa wa kilomita za mraba 105,000.