,,,Usipende kuona mawazo YAKO ndo ya WAZANZIBARI woote bana,kuna wengine tuna mawazo tofauti kabisa na wewe,,Mwanakijji hilo ni wazo zuuri sana,hakika kuna watu wanafikiria mbali,Muungano uwepo au usiwepo daraja litasaidia pande zote mbili KIUCHUMI na hata KIJAMII kwa ujumla,kwani tuna akina ANKALI zetu huko moro,akina AUNTIE zetu NATA NZEGA huko.
Kama mliweza kupata ankali bila daraja sasa tatizo nini? Na kuhusu mawazo sawa hayo yawe yako na pia hayawezi kuwa ndio uamuzi wa mwisho kwa Wazanzibari. Lakini sioni kama hawa jamaa wana uwezo wa kufanya hivyo hasa nikitilia maanani yale majumba makubwa kule ni ya watu wengine sio Watanganyika original.
Naam! Tunapokea hiyo chalenge yako!Wewe inaelekea sio mzanzibari wewe itakuwa either wakuja zanzibar au mropokaji nikuulize MTU ZANZIBAR ANAWEZA KUJIITA YEYE MZANZIBARI MZAWA!!!! Sema tukuaibishe sasa hivi.
Mimi nawaambia tungekuwa na viongozi kweli wenye maono ya kuthubutu, uthabiti wa vitendo na siyo "tutafikiria na kupanga mchakato" tungeweza kujenga Kigamboni (miaka kumi iliyopita) na la Zanzibar lingekuwa tayari; tungekuwa tayari tumejenga Stielger's Gorge dam badala ya hivi vya 20MW na 100MW plants! Stielger's ilipokaridiwa wakati ule ingegharimu dola bilioni kama 2 hivi! kiasi ambacho tunakipoteza kwa ufisadi every two years or so.
Hivi, mmesahau mambo ya opportunity cost? Gharama ya kweli ukiangalia siyo ya vile ambavyo tunafikiria tumevifanya!!
lakigamboni limetushinda,ndoto za mchana kwa nchi hii isiyo na uongozi wala vision.in tanzania? oooh day dreaming
Ndio nshasema hivyo, labda wewe unanijua.
Naam! Tunapokea hiyo chalenge yako!
Huyu jamaa nadhani wale wanzanzibari mamluki wasioyoijua zanzibar kila kukicha anadai zanzibar yao iachwe itengwe. Kuitenga Zanzibar ni ujinga na kukosa mantiki yote nia na madhumuni ni kuficha ufisadi ulio nyuma ya fikra zao. Wakijitenga wataanza kubaguana wenyewe kwa wenyewe hasa baina ya wapemba na waunguja. Macho yao yote yamekalia kwenye mafuta hakuna kengine.
Pili Zanzibar ikijitenga kuna swala la mipaka ya Zanzibar iko wapi ramani ya kabla inaonyesha mpaka wa zanzibar ni pwani yote ya tanganyika na kenya na visiwa vya unguja na pemba matatizo yataanzia hapo je mipaka ya zanzibar ipi? Bora na afadhali tudumishe muungano kurekebisha kasoro zilizopo au kuunda serikali tatu. Kujitenga kwa zanzibar kunaweza kutibua masuala mengi.
Hilo sio mada husika hapa ni mada je daraja lina faida gani? Mile 22 sio nyingi na daraja litasaidia mengi badala kuwa na fikra chanya vijitu vichache vyenye fikra mgando kama huyu wanakuja na kelele za kujitenga kila siku. Wanawadanganya wazanzibari walio wengi ambao hawajasoma kwa kuwajaza fikra hasi kwa matakwa yao.
Muungano una mapungufu na kweli kuna maeneo umechangia kuua uchumi wa zanzibar ila hizo ni hasara za muungano la msingi ni kuimarisha yale mapungufu ili tuendelee na sio kila siku kujitenga kujitenga.
Mdondoaji said:Pili Zanzibar ikijitenga kuna swala la mipaka ya Zanzibar iko wapi ramani ya kabla inaonyesha mpaka wa zanzibar ni pwani yote ya tanganyika na kenya na visiwa vya unguja na pemba matatizo yataanzia hapo je mipaka ya zanzibar ipi? Bora na afadhali tudumishe muungano kurekebisha kasoro zilizopo au kuunda serikali tatu. Kujitenga kwa zanzibar kunaweza kutibua masuala mengi.
Wazo hata mimi nimelipenda. Kutokea maeneo ya Mbweni, Bagamoyo kuelekea kusini ya kisiwa cha Unguja maeneo ya Kizimkazi Dimbani ni kilomita 36.4 au 22 miles. Mradi kama huu utaleta maantiki zaidi ikiwa toll road mosi - ili fedha za mradi zirudi na pili - ili daraja liweze kujiendesha lenyewe.
Cheki ramani hapo chini nimechukua screen shot toka google earth
..Zanzibar itachangia kiasi gani?
..wa-Tanganyika watafaidika vipi na mradi huu?
..naomba mnieleze faida za KIUCHUMI za mradi kama huo, kwa maoni yangu umekaa kisiasa-siasa zaidi.
Acha utani! Tumeshindwa kujenga daraja kigamboni lisilozidi mita 400.Thubutu across Zanzibar channel thats beyond our wildest dream and honestly a herculian engineering task.Muzuri zaidi kuandaa timu ya marathon ikapige lap Qingdao Jiazhoij bridge, hii burudani tosha.