Zanzibar: Kanisa la T.A.G pamoja na makazi ya Mchungaji wake Daudi Suna, yamebomolewa na wanaodaiwa ni wakazi wa eneo hilo

Mbona waislamu wana misikiti ipo Ulaya na Marekani na maeneo yenye wakristo wengi na hakuna mtu anawabugudhi

Hata hapa Tanzania bara maeneo ya wakristo wengi misikiti ipo na hakuna mtu wa wakubugudhi
Hawa jamaa wana matatizo dunia nzima! Ukiwaona kule Finsbury park wanavyolazimisha kuwa Yemen utashangaa!
 
Hii iko kwa pande zote hata wakristo huwa tunapiga vita uislam baadhi ya maeneo.

Mimi ni mwenyeji wa kibosho Moshi, walitokea waislam katika kijiji kimoja kinaitwa Mweka ambapo kuna taasisi kama Chuo cha wanyamapori, geti la kushukia watalii kutoka Mt kilimanjaro, mashule nk, hivyo wakataka kujenga misikiti ili waweze kuswali karibu maana misikiti upo moshi mjini.

Waliponunua eneo na kumwaga tofali na mchanga, fitna zikaanza na padre akasema kanisani mnakubalije misikiti hapa, kilichotokea ni vita mpaka mradi ukafa.

Nafikiri Watu wa dini zote wanahitaji kustaarabika na kuelewa kwamba tunatakiwa tuishi wote kwa kuchukuliana.
 
Mbona waislamu wana misikiti ipo Ulaya na Marekani na maeneo yenye wakristo wengi na hakuna mtu anawabugudhi

Hata hapa Tanzania bara maeneo ya wakristo wengi misikiti ipo na hakuna mtu wa wakubugudhi
Sababu Uislamu ndio Dini ya Haqi na kweli, sio huu utapeli wenu wa akina Zumaridi na Masanja
 
Kwani lengo la kufungua kanisa ni nini??unadhani hapo kulikuwa hakuna watu wanaoenda kusali??
 
Twende mbele na turudi nyuma.

Haya makanisa ya TAG si ndiyo Yale ya kupiga mziki mnene masaa yote bila kuheshimu Uhuru wa watu wengine?

Watu wako watano kanisani lkn wameweka ma Ndugai huko nje.

Wanapiga mziki wakati Kuna watoto na magonjwa wamepumzika?

Lkn pia Huyo muchungachi alikua na leseni ya kuendesha Hilo kanisa hapo au watu mnalaumu tu.
 
Zanzibar ni nchi ya kiislamu japo eneo hilo lina historia ya kuwepo kwa ukristo kwa muda mrefu na historia inaweka wazi kupitia majengo ya makanisa yaliyopo unguja kwa miongo kadhaa.

Mfano kanisa la Anglican lililopo mbweni karibu na afisi ya tume ya uchaguzi au lile jengo lililopo mji mkongwe kule ndani ndani karibu na ilipokuwa ngome ya CUF now ACT hayatangazwi sana ila ukifika pale ndipo utaelewa.

Kikubwa na uwazi uliopo ni kuwa SMZ inajivika kuonyesha inajali wakristo ila siyo kweli, hii ni nchi ya kiislamu hata kama jamaa amekosea kiviile haikutakiwa kuvunja maana serikali ina nguvu zaidi ya kuvunja.
 
Kwanza tusiwe na jazba,swali la msingi,anayetoa kibali Cha ujenzi wa Kanisa au kitu chochote ni serikali,mamlaka husika ya eneo,je huyo pastor alipata vibari vya ujenzi wa Kanisa?

Pili sio sahihi kujenga nyumba ya Ibada karibu na makazi ya watu na kufanya mahubili kwa sauti kubwa wakati wa usiku,hata zile adhana za ndugu zetu za alfajiri Mimi huwa zinanikela kwa maeneo ambayo misikiti ipo kwenye makazi ya watu.

Tatizo la makanisa ya ndugu zetu walokole,Ibada zao ni ndefu Tena mziki mkubwa kwa sauti ya juu,sasa Kanisa likiwa kwenye makazi ya watu hii inakuwa ni shida sana.

Fikeni Dodoma,kisasa muone makazi yalivyopangiliwa,makanisa,misikiti,bar,lodge nk,hakuna KERO maana sayansi imetumika kwenye plan ya mji,sio kujijengea tu.

Kwenye hii story,kichwa kinasema wananchi wamebomoa Kanisa,je wao ndio wameleta Hilo gari la kubomoa?mi nilitegemea nione shoka,nyundo,wananchi wakivunja Kuta!
 
waumini wapoollee nawaza wale wa mfale wa mwanza walokuwa wakiruka sarakasi
 
Umehukumu wakati huna taarifa za kutosha. Tusubiri taarifa kamili ambayo itakuwa ina mizania sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…