EINSTEIN112
JF-Expert Member
- Oct 26, 2018
- 21,711
- 35,644
Kwani walichokifanya kina tofauti gani na walichofanya wale jamaa?Umejuaje kama ni UAMSHO? Huwa mnaanzisha chokochoko
Sio lazima wawe walewale au watumie jina lilelile
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani walichokifanya kina tofauti gani na walichofanya wale jamaa?Umejuaje kama ni UAMSHO? Huwa mnaanzisha chokochoko
Hawa jamaa wana matatizo dunia nzima! Ukiwaona kule Finsbury park wanavyolazimisha kuwa Yemen utashangaa!Mbona waislamu wana misikiti ipo Ulaya na Marekani na maeneo yenye wakristo wengi na hakuna mtu anawabugudhi
Hata hapa Tanzania bara maeneo ya wakristo wengi misikiti ipo na hakuna mtu wa wakubugudhi
Kwani walichokifanya kina tofauti gani na walichofanya wale jamaa?
Sio lazima wawe walewale au watumie jina lilelile
Umesoma uzi?? Rudia tena kusomaJibu swali acha kurukaruka.
Umejuaje kama ni UAMSHO/WAISILAMU?
Sababu Uislamu ndio Dini ya Haqi na kweli, sio huu utapeli wenu wa akina Zumaridi na MasanjaMbona waislamu wana misikiti ipo Ulaya na Marekani na maeneo yenye wakristo wengi na hakuna mtu anawabugudhi
Hata hapa Tanzania bara maeneo ya wakristo wengi misikiti ipo na hakuna mtu wa wakubugudhi
Kwani lengo la kufungua kanisa ni nini??unadhani hapo kulikuwa hakuna watu wanaoenda kusali??Mm Ni mkiristo sioni sababu huyo mtumishi kwenda kufanya ujenzi ktk maeneo ya wanao ishi waislmu yaani unakwenda uarabuni kufungua kanisa hapan aise. usijaribu Imani za watu haondoke Hapo kbsa Tena ashukuru ajapigwa kipigo kikali mnk hvyo yey ndie mchokozi ..watu wasitafute usaw wa kidini hapa
Kenya umewahi sikia muslami kaw rais au hata kiongoz mkuu hkn hvyo vitu sas na huku iwe Hvyo uwez kwenda kufanya ibada Zanzibar Tena siku hz wamestarabika zamani waliwamwagia tindikali .....
basi ndo muache kulalamika tu......mmiliki aende mahakamani atapata msaada wa kisheria....Wewe wasema.
Yesu hakuwahi kuingia kanisaniJe, una kithibitisho kuwa yesu aliingia kanisani?
Duh!Nitajie kanisa lililowahi kujengwa na Yesu japo moja tu.
Kwanza tusiwe na jazba,swali la msingi,anayetoa kibali Cha ujenzi wa Kanisa au kitu chochote ni serikali,mamlaka husika ya eneo,je huyo pastor alipata vibari vya ujenzi wa Kanisa?Kanisa la T.A.G pamoja na makazi ya Mchungaji wake Daudi Suna yamebomolewa na wanaodaiwa ni wakazi wa eneo hilo wakishinikiza kuwa hawataki Kanisa katika eneo lao.
Hii ni kunyume kabisa na sheria za nchi zinazoruhusu Uhuru wa Kuabudu. Kama jambo halitafanyika basi ni wazi kuna kiongozi mbaguzi wa dini anaewalinda wabomoaji na pia hii itachochea sehemu nyingine makanisa na makazi ya wachungaji kubomolewa.
Pia miezi michache ijayo kipindi cha mfungo kikianza huwa ni marufuku kwa wakristo kula sehemu za wazi, ukikutwa unafungwa mpaka mfungo uishe, wengine huwa wanapigwa sana, sasa hapa ni kwamba mtu kama umeamua kufunga kwa imani yako iwaje hutaki kuona wenzako hawali, ni kwamba imani yako no nyepesi sana kuisimamia, kama ni hivyo kuna haja gani ya kufunga.
View attachment 2146530
View attachment 2146523
============================================
Taarifa uhakika juu ya tukio hilo ni kuwa Mchungaji David Victor Suna ni mzaliwa wa Sumbawanga, lakini kwa miaka mingi amekuwa akiishi Zanzibar baada ya familia yake kuhamia huko. Kaka yake naye ni mtu wa kanisani lakini anafanya shughuli zake Dar es Salaam.
Alipoanza harakati za kutafuta eneo kwa ajili ya kanisa alipata wakati mgumu kwa kuwa walikuwa wanamkatalia, baadaye akabadili gia na kutafuta eneo la kununua la kwake binafsi na siyo kwa ajili ya kanisa.
Baada ya kutafuta eneo lake binafsi ndipo akapata eneo hilo lililopo Sebleni, Unguja. Akanunua kwa Sh 16,000,000 (milioni 16) akalipa fedha taslimu, akasaini mkataba rasmi wa mauziano (tazama picha), japokuwa katika eneo hilo alikuta mmiliki tayari amejenga banda ambalo nalo lilikuwa sehemu ya mkataba wa manunuzi.
Baada ya kununua akajenga ukuta kuzungushia eneo husika kisha akaanza shughuli zake za ibada, baada ya majirani kubaini kuwa mnunuzi ameanzisha kanisa eneo hilo ndipo mgogoro ulipoanzia.
Wakamwabia hatakiwi kuwa na kanisa eneo husika lakini David Victor Suna akashikilia msimamo wake kuwa ataendelea na shughuli zake za kanisa.
Mhusika ambaye aliuza eneo hilo naye akamvaa David Victor Suna na kumtaka arejeshe eneo hilo kwa kuwa hakuuza kwa ajili ya kanisa bali kwa ajili ya kujenga makazi, bado David Victor Suna akagoma kubadilisha matumizi wala kurudisha eneo.
David Victor Suna akawa asisistiza kuwa yeyote mwenye malalamiko aende Mahakamani ambapo haki itatendeka, hata waliposhirikisha Serikali za mtaa nao wakawa wanamshawishi ama kubadili matumizi au kurejesha eneo, msimamo ukawa ni uleule.
Ndipo siku ya tukio, lilikuka bulldoza likaanza kuvunja eneo husika wakati wahusika wakiwepo wachache wakiendelea na ibada kama kawaida, kanisa likavunjwa na baadhi ya vitu vikiwemo viti vikaharibiwa na gari hilo.
Mamlaka za Serikali za mtaa hazijawa tayari kuzungumzia tukio hilo, naye David Victor Suna amekuwa mgumu kuzungumzia kinachoendelea kwa kile kinachodaiwa hajatulia hadi sasa.
SERIKALI YAINGILIA
Taarifa zinaelezwa kuwa Mkuu wa Wilaya wa eneo husika anatarajiwa kutolea ufafanuzi suala hilo mchana wa leo Machi 11, 2022.
Nitarudi kuwapa kilichoendelea kuhusu tamko la Serikali.
ITAENDELEA...
View attachment 2146667
View attachment 2146668
View attachment 2146670
View attachment 2146671 View attachment 2146672
Umehukumu wakati huna taarifa za kutosha. Tusubiri taarifa kamili ambayo itakuwa ina mizania sawa.Kwanza tusiwe na jazba,swali la msingi,anayetoa kibali Cha ujenzi wa Kanisa au kitu chochote ni serikali,mamlaka husika ya eneo,je huyo pastor alipata vibari vya ujenzi wa Kanisa?
Pili sio sahihi kujenga nyumba ya Ibada karibu na makazi ya watu na kufanya mahubili kwa sauti kubwa wakati wa usiku,hata zile adhana za ndugu zetu za alfajiri Mimi huwa zinanikela kwa maeneo ambayo misikiti ipo kwenye makazi ya watu.
Tatizo la makanisa ya ndugu zetu walokole,Ibada zao ni ndefu Tena mziki mkubwa kwa sauti ya juu,sasa Kanisa likiwa kwenye makazi ya watu hii inakuwa ni shida sana.
Fikeni Dodoma,kisasa muone makazi yalivyopangiliwa,makanisa,misikiti,bar,lodge nk,hakuna KERO maana sayansi imetumika kwenye plan ya mji,sio kujijengea tu.
Kwenye hii story,kichwa kinasema wananchi wamebomoa Kanisa,je wao ndio wameleta Hilo gari la kubomoa?mi nilitegemea nione shoka,nyundo,wananchi wakivunja Kuta!