Zanzibar kukodisha/kuuza visiwa vyake: Iko vipi?

Zanzibar ni sehemu ya JMT, kwa maana ya kuuzwa kwa kipande cha ardhi ndani ya JMT ina maana gani kwa mamlaka ya JMT?
Je watu wanaonunua visiwa hivyo watatawalwa kwa sheria zipi? za JMT, SMZ, au za nchi zao?
Fuatilia vizuri juu ya hili mkuu.

Tunasema hivi, Zanzibar ni nchi kamili na ina mamlak na ardhi yake. Tunasema hivyo kwa vitendo na hatusemi kwa maneno maneno tu.

Halafu nikuweke tu sawa, hakuna kipande cha ardhi kinachouzwa. JMT kuna mambo itaiachia Zanzibar ili ifanye inavyoona inafaa kwa Wazanzibari.
 
Rabika
 
Ule uchaguzi ulitumia pesa nyingi sana. Wanafukia mashimo.
 
Pesa hizo zikijulikana zinakoenda mnishtue.
 
Upo Sahihi mkuu, Mtu yoyote wameruhusu kwenda kuwekeza,kampuni na uandae proposal kabla ya kwenda kuwekeza Kwenye kisiwa unachohitaji.

Wametumia mfumo wa Public Private Partnership (PPP), na unapoomba kuwekeza Kwenye kutuma tenda unatakiwa kudeposit USD 1500 non refundable. Na nimeona mfumo wa Lease Acquisition Cost hii wawekezaji wowote lazima watachangia gharama za tangu mwanzo Mpaka mradi utapofikia.

Zanzibar baada ya miaka michache hivyo visiwa vitakuwa kivutio kubwa cha utalii sawia na visiwa vya wenzetu huko Ulaya na America.
 
Wam
Kuna wazanzibar wamepata ajira kutokana na uwekezaji wa Bill?
Wamepata ajira wangapi wanalipwa kiasi gani. Maana siyo watu walipwe kama watumwa. Je hao walioajiriwa wakiacha kazi baada ya miaka 2 wanaweza waka survive muda gani kwa saving zao. Jamhuri ni Mali ya umma (Res Publica) kuna haja ya kila maamzi hekima na busara vikatumika maana hawa wazungu walishaonyesha hawana nia na sisi. Miaka ya 1903 Cuba leased Guantanamo bay to the US ,and now marekani haitako kuirudisha. Tuwe tu makini kwa tunavyofanya na kuamua leo, maana tunaweza kufanya makosa akawagharimu watoto wakaja kutulaumu. Uzalendo kwanza
 
It's the same approach ambayo Maldives waliichukua some years ago. Leo Sisi hapa watu wanalishwa matango pori tu.

Tutafika lakini
 
Hapo hapo tukumbuke kwamba Zanzibar ni sehemu ya Jamhuri ya Tanzania. Mipaka ya Jamhuri imeainishwa kwa kujumlisha ardhi yote ya Zanzibar na ya Tanganyika. Serikali ya Jamhuri ndiyo pekee yenye mamlaka ya kutamka kuhusu sehemu yo yote ya ardhi ya Jamhuri. Mahusiano na nchi za nje ni suala la Muungano. Zanzibar hairuhusiwi kuingia mkataba kuhusiana na ardhi yake bila kuihusisha Jamhuri. Kwa mfano haiwezi kuanzisha ubalozi na nchi ambayo haina mahusiano na Jamhuri. Hilo ndilo tatizo lililojitokeza wakati Zanzibar ilipotaka kujiunga na umoja wa nchi za Kiislamu.
 
Wewe unaejua sana tuambie hizo hela zilizopatikana zimefanyia nini?

Sijui elimu yako lakini nina uhakika uelewa wako ni mdogo sana juu ya masuala ya sovereignity,eg.umeshindwa kabisa kujua kuwa kuuza ardhi ni sawa na kuuza nchi,uhuru au sawa na kuuza nyumba...na hakuna kurudishiwa ni forever.

Kwa maana nyingine Zanzibar imeuza uhuru wake kwa wageni,unaunga mkono upumbavu huu!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…