Zanzibar Kumpokea Sultan Jamshid: Ziara ya Kihistoria Baada ya Miaka 60 Uhamishoni

Mkuu wazanzibari huwa ni watu wepesi wa kusahau.
Huyo jamaa wanaye mualika kama ngamia, ataingiza kichwa , halafu baadaye watashitukia hela ya mwarabu inawatoa madarakani waafrika,
Believe you me.
mwarabu ana tatizo gani?
 

So point yako ni nini, kuwa cheo cha usultan bado kipo zanzibar kwa hiyo anarudi kwenye kiti chake.. unaposema anarud kama ceremonial leader on what grounds? Lengo ni nini hasa ikiwa huko dunia aliishi kama raia wa kawaida inakuwaje mumlete na kumtambulisha kama kiongoz .. na kusema anakuja kama ceremonial leader kwa katiba ipi ambayo inatambua usultani?

Kama ana ndugu Zenji aje kama raia wa kawaida infact anatakiwa aombe hata visa maana sio raia wa zanzibar kumbuka hatutambui uraia pacha
 
Ndo maana nimewauliza waliposema sijui anakuja kuleta upatanishi upatanishi wa nani na nani na yeye anakuja kwa mwamvuli upi maana hana status yoyote kwenye dunia

Maana yake kitendo cha kumleta na kumtambulisha kama sultan wa zanzibar maana yake mnaeazodoa walioyasapoti mapinduzi na kuwaonyesha haikuwa sawa
 
Nafahamu mko hapa kupima upepo, ila katika jambo ambalo SAMIA asijethubutu hata kulizungumzia ni hili. Siku anafanya hivi ndiyo itakuwa mwisho wake. Kubwa zaidi Jamshid atakuwa ni MPUMBAVU asiyejifunza endapo atalazimisha kufika Zanzibar.
 
Huyo jamaa Jamshed aanze kwa kuomba radhi kwa babu zake kuuza watanganyika kama watumwa.
Na kwa vile usultani alisha vuliwa akaribishwe kama raia wa kawaida.
Kwanini usiwalaumu Machifu wa Kitanganyika waliouza mateka wao kwa waarabu? Kama akina Milambo na Abushiri wasingeuza watumwa ina maana waarabu wasingekuwa na mtu wa kumuuza.
 
Sasa unadhani anaweza kuwa Sultan kwa Katiba ipi? Kwanza ZNZ siyo sovereign state, ni sehemu ya muungano wa Tanzania.

Pili mzee mwenye miaka 95 pengine ana dementia na alzheimer, atapata wapi hizo nguvu unazomuogopea? Huyu ametaka kuja kumailizia uhai wake mahali alipozaliwa tu.
 
Kwanini usiwalaumu Machifu wa Kitanganyika waliouza mateka wao kwa waarabu? Kama akina Milambo na Abushiri wasingeuza watumwa ina maana waarabu wasingekuwa na mtu wa kumuuza.
Kwa hiyo unaungana na slave traders waarabu?
 
Ndio view ya Wazanzibari hio? Ama nyie wa Bara? Wazanzibari wengi ukiwaambia wachague utawala wa Sultan na huu wa sasa hawataki wa sasa, uchaguzi kila mwaka unaonesha.

Pia masultan wa Znz wengi wa miaka 100 iliopita ni weusi kushinda hata wewe.
Waarabu weusi sio.
We Jamaa Unazingua
 
Kama muuza bidhaa (machifu wenu) anayo bidhaa (watumwa) kwa nini mnunuzi alaumiwe kuinunua na kuiuza?
Kwa hiyo una support slave trade, kuonewa kwa waafrika, na mapinduzi ya 1964 ya waafrika kujikomboa, kwako ni upuuzi tu?
 
So Zanzibar ya leo wakazi wa mwanzo kabisa walikuwa ni waoman au kuna namna walifanya wakaonekana wao zaidi wakahodhi madaraka?
kwanza ufahamu ukanda wa pwani wote huu ndio ulijulikana kama Zanzibar na sio vile visiwa kuanzia pwani ya kenya hadi msumbiji.

historia inaanzia mbali kabisa kwa mtu anayeitwa "Almuli" chief wa kilwa huyu alikua akiongoza kisehemu kidogo cha kilwa, at same time Iran mfalme wao alifariki, aliacha watoto kama 8 ambao walikua wakigombania urithi, mtoto mmoja alikua ni chotara mama toka Africa na baba Mfalme wa Iran, huyu mtoto alishindwa kupata ufalme akakimbilia Africa na watu wake, akaenda Mogadishu lakini kule hakupatana na wasomali akaja chini hadi Kilwa, Almuli akakubali kumuuzia kisiwa akipewa nguo nyingi zitakazozunguka kisiwa kizima, wakampa wakachukua kisiwa, inasadikika Almuli baadae alighairi akarudi awarudishie nguo ila jamaa walichimba ardhi na ndio Kukawa na kilwa kisiwani.

hio ni miaka ya kuanzia 900, kuanzia hapo hadi miaka ya 1500 kilwa ika expand kwenda hadi sofala hadi lamu, wakaipiga gape hadi mogadishu, wakati huo Oman wanakuja na Monsoon wind kufanya biashara ila sio watawala. miaka ya 1500 portugal wakaja, tofauti na watu wa middle east waliokuwa wakifanya biashara portugal walikua hawajui kufanya biashara wao wakija wanakuja na jeshi kama ni soko wanasomba na kuiba vitu vyote, so watawala wote wa pwani wakaanza kupigana vita na portugal. kilwa at that time ilikua ni trade Empire kila mji ulijiongoza wenyewe

sababu portugal walikua juu kivita waliwapiga watu wa pwani, watu wa pwani wengi walikuwa ni waisilamu waliomba msaada kwa Ottoman Empire likaja jeshi chini ya Mir Ali kupigana na Portugal nalo likapigwa.

turudi Oman sasa, kule nako mfalme Wa Oman alipinduliwa akakimbilia India ya zamani, akapokelewa na wabulushi akapewa eneo akakusanya kodi, akarudi na jeshi la wabulushi akampiga aliempindua na kuirudisha Oman, wabulushi walikua vizuri sana kwenye vita, portugal alikuwa na maeneo kuanzia India hadi huku kwetu, Oman alimpiga Portugal kule Asia na kumshinda, sababu Oman walikua na interest kibiashara East Africa wakaja kuwasaidia watu wa pwani na jeshi lao la wabulushi, kama tunavyojua Mreno akapigwa na kutolewa East Africa.

miaka hio ukaanza Utawala wa Oman sasa huku kwetu, Empire ya Oman kama ilivyo Kilwa haikuingilia Tawala za Ki Africa, walikua wanafanya Biashara tu na kama nilivyosema huko juu the so called makabila makubwa nchi hii ni makabila yaliyotoboa kwa kufanya biashara na Oman kama vile Wachaga, Wahaya etc, na tofauti na Ukoloni Zanzibar haikuwa koloni la Oman bali vice versa was true, Mfalme wa Zanzibar ndio alitawala Oman.

mwaka 1861 ndio ikagawanyika, ZNZ na Oman vikatengana na Znz ikawa na MAsultan wake, ukitoa masultan wa mwanzo masultan wote kuanzia mwisho miaka ya 80 hadi Jamshid walikua ni weusi ama machotara.
 
Yaani aliondoshwa kwenye utaeala miaka 60 iliyopita mpaka Leo yupo hai?
 
😀
Watarudisha utawala wake kimtindo
Huyo mfalme sio kaja kutembea tu,huwezi jua yaliyo nyuma ya pazia.
Labda kuna makubaliano ya aina fulani ikiwa atarudi Zenj.
Na siyo ishara nzuri kwa baraza la mapinduzi.Mwenye nchi anakuja.
 
Kwa hiyo una support slave trade, kuonewa kwa waafrika, na mapinduzi ya 1964 ya waafrika kujikomboa, kwako ni upuuzi tu?
boss slave trade ni mbaya ila hakuna ambaye hajafanya, tena afadhali hao waarabu walikua na ustaarabu kidogo soma slave trade ya machief ni mbaya kupita maelezo, chief anakufa watumwa kadhaa watoto wa kike vigoli wanazikwa nae, mfalme anatoka tu na farasi wake anaenda vijijini anakamata watumwa etc.

waarabu mtumwa aliweza kujinunua mfano wewe umeuzwa utumwani kwa laki 5, ukaenda znz mashamba ya karafuu, kule unalipwa 20,000 kwa mwezi, ukisave hela zako zikatimia laki 5 unanunua uhuru wako na kuondoka. na hao walikua ni watu wa bara. watu wa pwani walikua hawauzwi kabisa utumwani, mfano wazaramo tabia yao walikua wanajiuza wenyewe kwenye utumwa znz, ndugu anachukua hela akifika kule anapanda kidau anarudi zake huku, wakapiga marufuku kununua mzaramo utumwani.
 
kama unachosema ni kweli basi wa znz wangeipenda kweli serikali yao na CUF/ACT zingekua vyama kama UDP ila tunajua kitu gani kinaendelea ZNZ, inatumika nguvu nyingi toka bara kuwaweka madarakani, wa ZNZ wenyewe hawaitaki. ikiwa ZNZ wenyewe hawataki mapinduzi wewe nani bara kuwasemea?

nikikuuliza sasa hivi mwanamuziki wa miaka 100 iliopita bara ama Africa humjui hata mmoja ila znz wapo na mpaka leo wanafanyiwa remake ya nyimbo zao, marekani Bahari yake anapakana na West Africa ila alikua anaacha NCHI zote Anakuja ZNZ, umeme, barabara za kisasa, mpaka nyumba zenye lift zilikuwepo way before.

viongozi wao walikuwa smart wamesoma, we mpaka mtu mweusi upo huku mwisho wa dunia unakuwa coronated kama Sir sio jambo la kitoto, kaangalie serikali ya 1963 iliopinduliwa speech yao UN then compare na hawa wa leo.
 
Basically unajidhalilisha kwa kuunga mkono arab slave trade.
 
Tanganyika hiyooo inarudi taratibu
 
Karume aliwasaliti wakina okelo na wenzake walioshiriki mapinduz tukufu
Kwa hofu ya usaliti karume akaona auze uhuru ambao hajaupigania kwa nyerere hakuona thaman ya ule uhuru sababu hakuupigania

Okello na wenzake walikua loyal kwake akawasiti ndo chanzo cha migogoro mpaka leo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…