Zanzibar Kumpokea Sultan Jamshid: Ziara ya Kihistoria Baada ya Miaka 60 Uhamishoni

Zanzibar Kumpokea Sultan Jamshid: Ziara ya Kihistoria Baada ya Miaka 60 Uhamishoni

Mffyuuu.
Alokwambia hatufanyi kazi nani. Lini tulikuja kula kwako!?
We huwezi kujifananisha na mie katu.
Lkn ukweli usemwe tu, dhulma imepita na bado inatuadhibu, sote...tulokuwemo na tusokuwemo.
Poleni wazanzibar.
Tanganyika itaendelea ku control kila kitu kwenye hicho kisiwa.
Yaani remote ipo dodoma inacontrol kila kitu huko paje na mchambawima
 
Poleni wazanzibar.
Tanganyika itaendelea ku control kila kitu kwenye hicho kisiwa.
Yaani remote ipo dodoma inacontrol kila kitu huko paje na mchambawima
Insha'Allah kheri
Na ahsante kwa Pole 😍
 
Huyu anapaswa kupewa heshima zote aliwafanyia Tanganyika mambo mema, ndo aliowafundisha watanganyika kuvaa nguo, alishirikiana na serikali ya uingereza kukomesha biashara ya utumwa, alizuia kazi za manamba, alitengeneza utawala wa sheria, aliruhusu vyama vingi vya siasa. wahuni wakatumia uungwana wake kumfanyia mambo ya hovyo,
Kuwafanya tu wanzanzibar kutamani kuwa waarabu muda wote inapaswa kuwa crime against humanity, hapo hatujazungumzia forced labour ya weusi waliotumika kumtengenezea maisha yake ya kifahari.
 
Ndio view ya Wazanzibari hio? Ama nyie wa Bara? Wazanzibari wengi ukiwaambia wachague utawala wa Sultan na huu wa sasa hawataki wa sasa, uchaguzi kila mwaka unaonesha.

Pia masultan wa Znz wengi wa miaka 100 iliopita ni weusi kushinda hata wewe.
Tatizo wazanzibar wanafikra za utumwa vichwani mwao hata Mombasa Kuna jamii ya kiarabu lakini huwezi kusikia watu wa Mombasa wakiwalilia waOman waje wawatawale
 
View attachment 3186808

Mnamo Januari 9, 2025, Zanzibar itashuhudia tukio la kihistoria itakapompokea Sultan Jamshid bin Abdullah kurejea kwenye pwani zake. Hili ni tukio muhimu sana kihistoria, kwani mtawala wa zamani wa Zanzibar anarudi baada ya miongo sita ya uhamisho nchini Uingereza na Oman, kufuatia kuondolewa kwake madarakani wakati wa mapinduzi ya 1964.

Cc Pascal Mayalla

Maelezo kuhusu jinsi ziara hii ilivyopangwa bado hayajafahamika, lakini umuhimu wake hauwezi kupuuzwa. Kurudi kwa Sultan Jamshid kunawakilisha ishara ya upatanisho wa kipekee kutoka kwa serikali ya Zanzibar. Ziara yake inaweza kuwa daraja kati ya enzi za kabla na baada ya mapinduzi, ikichochea mshikamano na uponyaji wa kitaifa.

Zanzibar inaweza kuchukua nafasi hii kumwalika Sultan kuishi katika mojawapo ya majumba yake ya zamani kama raia wa kawaida. Hatua kama hiyo haitaimarisha tu taswira ya Zanzibar kimataifa bali pia inaweza kuinua sekta yake ya utalii, kwani uwepo wake utavutia shauku kubwa. Zaidi ya hayo, inaweza kuashiria sura mpya ya upatanisho kati ya Sultan na serikali ya mapinduzi, ikitoa mfano wa maendeleo na mshikamano.

Dunia inaposhuhudia tukio hili la kihistoria, Zanzibar inasimama katika nafasi ya kubadilisha urithi wake kuwa simulizi ya mshikamano na heshima ya pande zote.
Issa AlHarthy.
Upatanisho na wakoloni 😆😆😆😆😆. Hivi hamjui kuwa wana machungu na mlichowafanyia. Wakaribisheni baadae waanze figisu.
 
Yaani ulivyandika kwa Shauku na kujikweza😀😀😀😀

Hakika MTUMWA NI MTUMWA tu, babu zako wamatumbi na wamwera huko waliko wanakunja mafuvu yao na kujipigiza kwenye kuta za makaburi kwa gadhabu baada ya kuona huu uzi wako.

Hivi wazanzibari wnajua historia yao vizuri yaani wanajisahaulisha wao ni kizazi cha kitumwa tena watumwa sio kutoka OMAN ila kutoka Tanganyika ila wanaona Waoman waliotesa babu zao ni watu wa maana sana na wao wanajiona waomani🤣🤣🤣🤣

Ukienda Uarabuni mwafrica ni katika kiumbe daraja la chini sana tena ambaye unaruhusiwa kumiliki kama mali. Lakini waarabu hawa wa kubabatiza huku africa wanavyowahusudu waarabu orijinal sasa🤗🤗🤗

Anyway, kupanga ni kuchagua!!!
 
Back
Top Bottom