Kwa maoni yangu mimi binafsi, Unguja ni kisiwa kizuri sana na kinavutia. Wauache mji mkongwe ila kuwe na mji mpya mbali kidogo na mji mkongwe pawe na ofisi za serikali na majengo ya kibiashara ya watu binafsi.
Tatizo ni mji mkongwe na surrounding areas ambao ni mji mdogo sana, kutumiwa kiserikali na biashara za kibinafsi . Majengo yale, kwa kuwa ni UNESCO heritage site yangeachwa yapumue na serikali ikajenge mji wake nje kidogo ya mji mkongwe angalau 10 miles away. Wafanyabiashara nao watawafuata.
Malalmiko mengi ni neighbourhoods za Zanzibar, zipo very unplanned kama Dar ilivyo ila tofauti Zanzibar wakazi wake inaonyeesha wazi aidha hawana kipato cha kutosha au basi hawana ile nia ya kuishi mahali palipojengeka vizuri, ingawa ni watu wasfi sana. Nyumba zao ndani ni safi sana na ni watu wanaojiweka kiusafi kwa ndani. Ila nje unaweza ukaona kama kuna uchafu mwingi umezagaa kutokana na kutokuwa na tabia kama za kuwa na makaro, utaona maji ya kuparia samaki yanatupwa tu kwenye mchanga na kufyonzwa.
Kingine kilichonishangaza (Na nimefika Zanzibar mara nyingi naijua tangu 1986) ni upungufu a misikiti mikubwa yenye shule kubwa za kiislam. Yaani, Dar es salaam ina misikiti mingi mikubwa kulinganisha na miji mingi ya kiislam ukanda wa Pwani ya AFRIKA MASHARIKI. Nashangaa sana kila nikiangalia miji ya kiislam ukanda wa East Africa, hukuti misikiti mikubwa au taasisi kubwa za kiislam mijini au vitongojini kama ulivyo mji wa Dar es salaam.
Mfano mzuri wilaya ya Temeke, ingawa haipo mjini lakini ina misikiti mikubwa na taasisi kubwa za kiislam zilizojengwa na watu tu wa kawaida. Zanzibar vitongojini misikiti yake ni midogo na taasisi za kiislam hazijapenya sana vitongojini. Hilo wazanzibari mpende msipende ni jambo la kufanyia kazi ukilinganisha na wingi wa waumini Zanzibar.
Mwisho, wazanzibari wengi wapo diaspora na hupenda kujilipua, hata kurudi hawataki na hii nadhani inatokana na kutokuwa na imani na serikali ya Mapinduzi hasa kwa vijana. Serikali ya Mapinduzi sidhani kama historia yake kwa vizazi vya muda huu ni nzuri. Ni kama kuna kutokupenda nyumbani kwa vijana hasa wa unguja. Labda Serikali ya Mapinduzi ijitahidi kuwashirikisha zaidi vijana kwenye maamuzi na kuwapa vyeo vya juu vya kimaamuzi vijana hasa wilayani.
Sikubaliani na mdau
Emiir kuwa majengo mazuri siyo hulka au mambo ya kiislam kwa sababu kama kuna kitu ambacho uislam umeleta dunia hii ni majengo na kasri za kifahari. Angalia miji yote ya kiislam kuanzia Muscat, Riyadh, Mecca, Basra, Qoum, Cordoba, etc.. ni miji iliyojengeka haswa ukizingatia miaka hiyo ambapo New York ilikuwa ni kijiji tu.