Zanzibar ni bomu linalosubiri kulipuka, Watawala mkifanya kiburi halitoiacha nchi salama

Zanzibar ni bomu linalosubiri kulipuka, Watawala mkifanya kiburi halitoiacha nchi salama

jambo la msingi kwa wazanzibari na watanzania wote keshokutwa jumaa tano tujitokeze kwenda kupiga kura.
kura yako ndio itakayo amua nani awe kiongozi wako.
kura ndio itatoa matokeo.tuacha mihemko.kura ndio itakayo amua.
wajibu wa kila mtanzania mwenye sifa kwanza ni kwenda kupiga kura.
na ninaamini kila chama kina wakala wake atakaye hakikisha kura za mgombea wake, tuache kuwa na wasiwasi, jipangeni tu.
 
Umeonesha ni kwa jinsi gani una upeo wa kuchambua mambo mbalimbali. Hongera sana

Ila wasichokijua bara ni kua Zanzibar ni tofauti sana na bara. Zanzibar wanashindwa kufanya maendeleo mengi kwa udhalimu wa chama tawala na bara kuwapangia nani awe mshirika wao kwenye maswala yote hasa ya kiuchumi na nani hawamtaki. Namuonea sana huruma mwinyi maana ndio CCM wa kwanza kushindwa kuchaguliwa kuwa Raisi za Zanzibar.
 
Little too late, wazanzibari sio leo tuu kwenye uchaguzi. Tuko occupied tokea siku ya muungano! Nikupe mfano tuu, utasafiri Dar hadi Moshi hupiti road-block, ukisafiri Zanzibar km kila baada ya 10km road-block !

Sidhani kama nahitaji kutoa mifano zaidi, lakini tazama icho kichapo kinachotolewa na vyombo vya dola jeshi na polisi dhidi ya wazanzibari. Nakumbuka nilipokuwa mdogo nilienda kambini kumtembelea mzee (jeshi/jwtz), basi mlangoni kuingia kambini nilikutana na mtanganyika akanitolea maneno hapo ya kunisimanga.

Kwa bahati nilikuwa mtoto mdogo sikumfahamu hadi sasa nishakuwa mtu, ndio nafahamu udugu wa damu baina ya Zanzibar na Tanganyika!
 
Jeshi haliwezi kushinda mapambano baina yake na majority ya watu katika nchi.
Mission za jeshi zinahitaji bajeti, time ya operesheni na moral ground ya kufanya operesheni zake. Kama Majority ya watu hawataki na wako determined litaishia kuua watu tu na hatimaye makamanda wake kufunguliwa mashitaka ya uhalifu wa kivita.
 
Ninavyojua mimi, CCM itashinda Bara na Zanzibar na pande zote za muungano zitaendelea kuwa salama na zenye amani chini ya Serikali za Chama cha Mapinduzi!
 
Ninavyojua mimi, CCM itashinda Bara na Zanzibar na pande zote za muungano zitaendelea kuwa salama na zenye amani chini ya Serikali za Chama cha Mapinduzi!
Sio kwa Zanzibar kiongozi, kinachoendelea Zanzibar ni wazi kwamba hawapo tayari kuyakubali matokeo ambayo yataonyesha CCM kushinda. Na hii ni kutokana na kuwepo kwa dalili ama viashiria vya uhujumu wa uchaguzi
 
Hakuna vurugu yoyote itakayo tokea Zanzibar, Tunategemea uchaguzi utakwisha salama na kila mmoja atapata haki yake. Tunategemea Raia na vyombo vya ulinzi na usalama kushirikiana katika zoezi zima la uchaguzi.
 
.....
labda muandamane mtandaoni....lakini live mtapewa kipigo cha mbwa koko.....kwa jinsi watz walivyo waoga siku hiyo mtaani kutakuwa kimya na utulivu kabisa
 
sio kwa Zanzibar kiongozi.... kinachoendelea Zanzibar ni wazi kwamba hawapo tayari kuyakubali matokeo ambayo yataonyesha CCM kushinda... na hii ni kutokana na kuwepo kwa Dalili ama viashiria vya uhujumu wa uchaguzi
Mkuu utabiri wako utajidhihiri ndani ya siku mbili tatu zijazo. Tusubiri.
 
tumefika hapa baada ya waliodhaniwa watakua viongozi wamegeuka watawala
 
Mazingira ya wizi haya. Wasafirishe masanduku ya kura ili wapate nafasi ya kujaza kura FAKE.
 
Maalim amekuwa akishinda kuanzia mwaka 1995, lakini amekuwa hatangazwi.

Joto la mwaka huu sijui litapoa vipi
 
Back
Top Bottom