Zanzibar ni nchi huru au ni sehemu ya Tanzania?

Zanzibar ni nchi huru au ni sehemu ya Tanzania?

Kwaiyo unamaanisha Zanzibar ni dola na Tanganyika ni dola nchi ni Tanzania
Ndiyo, Zanzibar ni dola kwasababu haijawahi kupoteza mamlaka yake yote ya kujitawala (State-Hood and Sovereignty), Tanganyika haipo. Japo kuna wataalamu wengi wanaamini kwamba Tanganyika bado ipo, ilichofanya ni kubadilisha tu jina na kuitwa JMT baada ya kupoka madaraka ya Zanzibar.

Hili linakuwaje gumu kueleweka ilhali nchini Marekani kuna madola 50 (States) yanayojitawala na kujiendesha yenyewe chini ya Serikali Kuu ya Shirikisho ??
 
Jana nikiwa sehemu fulani nilisikia baadhi ya wasomi wakijadili mambo kadhaa hasa wakiitaja nchi iitwayo Zanzibar.

Kwa walio na ufahamu vizuri nitaomba msaada hapa. Kwa uelewa wangu, ili sehemu ya ardhi inayokaliwa na watu iitwe nchi(state), ni lazime pawepo na mambo yafuatayo:
1. Mipaka kamili inayotambulika kimataifa
2. Serikali
3. Watu na makazi
4. Iwe na uwezo wa kuingia makubaliano na nchi nyingine bila kuingiliwa au kuhitaji ruhusa kutoka sehemu nyingine.

Ikiwa sehemu inajitosheleza kwa mambo yote hayo manne basi, huitwa na kutambulika kama nchi.

Lakini sehemu hiyo (nchi) inaweza kupoteza sifa ya kuitwa nchi na jumuia za kimataifa kama:
1. Itaungana na nchi nyingine kutengeneza nchi au taifa moja
2. Itakubali kutawaliwa na nchi nyingine
3. Mipaka yake itamezwa na nchi nyingine
4. Itagawanyika katika sehemu ndogondogo zenye mamlaka kamili

Je, baada ya Zanzibar kuungana na Tanganyika na kuunda serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bado Zanzibar inatambulika kama nchi? ni vigezo gani huifanya zanzibar kuitwa nchi?
Zanzibar ni mkoa uliochangamka, hadhi ya Hussein Mwinyi kwenye baraza la Mawaziri haina tofauti na hadhi ya kipara mkata umeme.
 
Ndugu yangu angalia usije kufa kwa ugonjwa wa moyo, huu Muungano hakuna wa kuuvunja hayupo hajazaliwa na hatozaliwa wee umia vumilia mpaka mwisho wa dahari.


Unaambiwa na Pengo , uulinde Muungano uliowekwa na mungu wenu



Kardinali Pengo: Muungano si bahati nasibu​



- May 02, 2016

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amewataka waamini na wananchi kwa ujumla kutambua kuwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar si jambo la bahati nasibu.

Kardinali Pengo ameyasema hayo ofisini kwake hivi karibuni alipoitisha vyombo vya habari vya Kanisa Katoliki kuzungumzia pamoja na mambo mengine ongezeko la Parokia mpya jimboni kwake pamoja na mabadiliko kwa Maparoko na Maparoko Wasaidizi katika baadhi ya Parokia jimboni humo.

Asemema suala la Muungano linapaswa kuchukuliwa kwa uzito wa pekee kwa kila Mtanzania hasa waamini Wakatoliki na kwamba kila mwamini anapaswa kutambua kuwa amepewa jukumu na Mwenyezi Mungu kulinda na kuombea Muungano huo.
 
Huu ndio uzuri mmoja wa JF, uelimishaji umma, huna haja ya hairs na kutokana watu humu, rubbish, bull crap, huu ni uwanja wa kuelimishana, muungano wetu ni unique haupo pengine popote duniani!, muungano wetu kimataifa tuu ndio muungano wa union uliounda nchi moja ya JMT, lakini kitaifa, muungano wetu sio union, ni federation yenye nchi mbili, katiba mbili, marais wawili, mabunge mawili, Mahakama mbili, nyimbo mbili za taifa, bendera mbili, majeshi mawili, sarafu ndio moja. Tofauti pekee kati ya nchi hizi mbili ni moja ndio yenye sovereignty na nyingine haina.
P
Jeshi la Zbr linaitwaje ?
 
Anapatikana mtaa wa Tandamti na Congo Kariakoo location namba nitafute.


Januari 2000


Wazanzibari waambiwa:
Jihadharini na Pengo




WAZANZIBAR wametakiwa wachukue hadhari dhidi ya majaribio ya kutaka kuwaingiza katika balaa sambamba wakiitafakari kwa makini kauli ya Kardinali Pengo.


Aidha wametakiwa kuelewa historia ya kanisa Katoliki kuwa halijakuwa na rekodi nzuri hasa katika ukanda wa maziwa makuu pale linapojitumbukiza katika siasa.

Hayo yameelezwa na Wananchi kadhaa walioongea na gazeti hili mjini Zanzibar kufuatia kauli ya Kardinali huyo juu ya siasa za Zanzibar.

"Huko Rwanda Maaskofu wamelaumiwa kushiriki katika mauaji ya halaiki ya Wanyarwanda, huko Burundi pia wanalaumiwa, tunapowasikia leo wakizungumzia siasa zetu lazima tuhofu balaa zao, alisema bwana Hassan Mazrui.

Kama ni kuitakia mema Zanzibar, haiwezi kuwa nia ya askofu alisema bw. Mazrui

Alieleza kuwa chama tawala CCM kimejiwekea tabia ya kusimamia mabadiliko ambapo moja ya mabadiliko makubwa yaliyofanywa ni kuingilia makubaliano ya Muungano. Mabadiliko ambayo yalimuondoa Rais wa Zanzibar kuwa makamu wa Rais.

"Kanisa katoliki lilikuwa wapi kukemea mabadiliko hayo yaliyovunja makubaliano ya muungano", alihoji bwana huyo.

Aidha amesema Nyerere alikaa zaidi ya miaka 20 akibadili mambo apendavyo mara kofia mbili mtu mmoja mara kofia moja tena kofia mbili, "Mbona hakuna askofu aliyehoji na kumwambia kakaa sana. Hiyo Demokrasia wameijua lini? Alihoji



"Katika kikao kile wakatoliki hawakuwepo? Pengo leo anazungumza kwa niaba ya nani, Kanisa katoliki au yeye binafsi? Alihoji bw. Ameir.

"Kama anaona mabadiliko yataathiri Kanisa Katoliki basi Masheikh watatembea nyumba kwa nyumba kuyaunga mkono aliongeza na kama yatalinufaisha kanisa pia watafanya hivyo kuwaepusha Wazanzibar na balaa hilo, alisema bw. Ameir.

Mama mmoja Safia Shaame aliyedai ni mwana CCM alisema Pengo na kanisa lake hawezi kudai anawatakia mema Wazanzibar.

Alisema muungano 1964 ulikuwa wa Mambo11 Serikali za Tanganyika na Zanzibar zilibaki na wizara zao na mambo mengine ila 11 tu ndiyo wakakubaliana yawe ya Muungano.

Ina maana kama ni Wizara 11 ndio zingekuwa za Muungano. Lakini wizara zote na watumishi wote wa serikali ya Tanganyika wakapandishwa daraja na kuwa wa Serikali ya Muungano ya Tanzania.

Matokeo yake anasema Wizara ya Maendeleo ya Jamii wanawake na watoto Tanzania ni ya muungano wakati ya Zanzibar sio ya muungano na misaada ikija inaishia kwa Marry Nagu. Hali ni hiyo hiyo kwa Wizara za kilimo, Elimu na nyinginezo.

"Je Maaskofu hata wale waliomtangulia Pengo hilo hawakuliona"? Alihoji

Alisema kwa upande mwingine imekuwa ikidaiwa kuwa Mwalimu Nyerere alipigania kudumu kwa muungano amani na utulivu.

Hata hivyo akahoji mbona Mwalimu hakufika Zanzibar toka 1995. Alidai kuwa Mwalimu alikuwa hodari wa kuwasimanga Wazanzibar kwamba wanabaguana Waunguja na Wapemba.

" Kama aliwatakia mema mbona hakuwapatanisha bali akawafanya kama somo katika mikutano yake ya hadhara, alisema Bi Safia na kuongeza kuwa "kama ni umoja na amani Zanzibar italetwa na Wazanzibar wenyewe.

Aidha alisema haya yanayotokea sasa ni mipango ya makusudi iliyopangwa nje ya Zanzibar kupitia chama tawala ili kuwapambanisha wazanzibar.
 
Ndiyo, Zanzibar ni dola kwasababu haijawahi kupoteza mamlaka yake yote ya kujitawala (State-Hood and Sovereignty), Tanganyika haipo. Japo kuna wataalamu wengi wanaamini kwamba Tanganyika bado ipo, ilichofanya ni kubadilisha tu jina na kuitwa JMT baada ya kupoka madaraka ya Zanzibar.

Hili linakuwaje gumu kueleweka ilhali nchini Marekani kuna madola 50 (States) yanayojitawala na kujiendesha yenyewe chini ya Serikali Kuu ya Shirikisho ??


KITABU CHA MAREHEMU ABOUD JUMBE

 
Na wakuu wa vikosi wote Mwinyi kaleta kutoka kwao Tanganyika
Zanzibar tangu imezaliwa, ukimuondoa Mwinyi Mkuu, Dr. Salmin na Dr. Shein, Zanzibar haijawahi kutawaliwa na MZanzibari, hivyo sii ajabu, kuongozwa na Wabara!, kama Zanzibar iliongozwa watu kutoka Oman, Malawi na Bara, kuna ajabu gani Wabara wakawa ndio wakuu wa hivyo vikosi kutokana na ukweli huu Je, Kuna Uhusiano wa Dini, Kabila na Ukakamavu? Watu wa Dini, Kabila fulani, ni wazuri zaidi jeshini kuliko dini, kabila nyingine?
P
 
Zanzibar tangu imezaliwa, ukimuondoa Mwinyi Mkuu, Dr. Salmin na Dr. Shein, Zanzibar haijawahi kutawaliwa na MZanzibari, hivyo sii ajabu, kuongozwa na Wabara!, kama Zanzibar iliongozwa watu kutoka Oman, Malawi na Bara, kuna ajabu gani Wabara wakawa ndio wakuu wa hivyo vikosi kutokana na ukweli huu Je, Kuna Uhusiano wa Dini, Kabila na Ukakamavu? Watu wa Dini, Kabila fulani, ni wazuri zaidi jeshini kuliko dini, kabila nyingine?
P
Yaani PM Muhammed Shamte Mpemba wa Ole si Mzanzibari ??

Ndivyo sheria na katiba zinavyosema hivyo ???
 
HATUTAKI MUUNGANO NIKIJA KUWA RAISI NINAWEZA KUGEUZA HIVYO VISIWA MAJIVU WAKIJITIA VICHWA NGUMU
 
Back
Top Bottom