Zanzibar ni nchi huru au ni sehemu ya Tanzania?

Zanzibar ni nchi huru au ni sehemu ya Tanzania?

Ni nchi Ila unaweza kukusanya watu wote kwa kupiga filimbi

Mzee Aboud “Mmasai”

Khiyana imekuwa kubwa, kubwa sana. Na hii yote, kwa sababu mbili. Sababu ya kwanza, ni ujinga wa Karume.

Yeye alikuwa na khofu na watu walokuwa na ilimu, hata mapinduzi bado.

Aliwahi hata kuhutubia kusema “wakimbieni wenye ilimu.” Na sababu hizo ndo akenda kujiunga moja kwa moja na Nyerere bila ya kumshauri mtu kwamba asipinduliwe na hawa halafu wataleta Waarabu. Mimi nilikuwa sijui habari za muungano. Pia Babu alikuwa na Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na yeye alikuwa hajuwi habari hio. Mimi nilikuwa nakwenda kazini, nafika kwa Sapriji, mbele si kuna duka la yule Muhindi anatengeneza radio anaitwa Dawud, nimesikia radio pale inasema juu, habari za muungano. Babu akasema yeye hajuwi habari hizo na yeye alikuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje. Na Nyerere kakubali kwa makusudi kuitawala Zanzibar. Hichi ndicho ninachokiamini. Sababu moja ni hiyo ya Karume, ya pili ya Nyerere kukubali bila ya kuwashauri wananchi.

Halafu Karume Mawaziri wote walosoma kawapeleka bara. Kina Babu, kina Idris, Hasnu Makame. Wote wamepelekwa bara wakawa wanacheza ngoma huko. Na ndivo inavotawaliwa Zanzibar, manake mpaka leo hakuna Bunge la Muungano. Kuna Bunge la Tanganyika. Lina watu mia sita na ngapi, na watu wa Zanzibar wametiwa ndani watu khamsini, watafanya nini ndani yake?

Kinachotawaliwa kwenye muungano si idadi ya watu, bali ni mambo ya nchi za nje na ulinzi.1 Zanzibar ina nguvu yake kama Tanganyika hata kama Tanganyika ina mamilioni ya watu zaidi. Zanzibar ni nchi huru kama weye wa Tanganyika. Ningelikuwa mimi ni mtu wa kisiasa sitokubali. Namshukuru Mungu nalisema, mara tu baada ya kutangazwa muungano ikiwa kuwa hatuna Bunge la Muungano, tena mbele ya Bhoke Munanka, alikuwa ofisi yake Beitlajaibu, Waziri wa Mambo ya Muungano “ikiwa hatuna Union Parliament, Bunge la Muungano hatuwezi kulichukuwa Bunge la Tanganyia tukalifanya ni Bunge la Muungano.”

Udhaifu wa watu wetu wote hawaitetei hii Zanzibar. Nadhani kama Hanga alikuwa akiitetea ilikuwa ndo sababu ya kuuliwa. Mimi sikusikia kama aliwahi kuitetea Zanzibar. Hanga alitaka kufanyisha nishani kwa walioshiriki kwenye mapinduzi kwa sababu ni kujionyesha na kujiaminisha kwa watu. Na watu walopigana wawe na furaha. Mwalimu akamkubalia halafu akamuuwa.

source: Kwaheri uhuru kwaheri ukoloni
 
Kutoka kitabu, kwaheri ukoloni kwaheri uhuru

Mzee Faraji

Nilipata kusikia kutoka kwa mmoja wa Marais wa zamani wa Zanzibar, kuwa manunguniko na madai ya Wazanzibari yaliyoanza katika miaka ya 70; kuhusu kuvunjwa mkataba wa 1964, kwa manufaa ya Tanganyika; madai hayo yalikuwa yakiwaudhi sana viongozi wa Tanganyika.

Hivyo siku moja Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, akamwambia Raisi wa Muungano (wakati huo) Mwalimu Nyerere, kwamba kwanini hawavunji mbali muungano ili wapumzike na “kelele” za Wazanzibari? Inasemekana Mwalimu Nyerere alimjibu kwa kumkatalia kwa kusema mengi pamoja na “…tukiwaachia tu, utaona jinsi mapesa ya Waislamu na Waarabu yatakavyo miminika Zanzibar…hapana, hatuwaachii.”

Laiti shida ya Mwalimu Nyerere ingelikuwa nae anazitaka pesa hizo kwa ajili ya Tanganyika, kisa kifuatacho kisingelitokea. Kwa mujibu wa kisa hiki kama kilivyosimuliwa na Rais huyo wa zamani [wa Zanzibar], Mwalimu Nyerere, wakati huo akiwa ameshastaafu, alipita akiwa safarini, katika uwanja wa ndege Jeddah, Saudi Arabia. Balozi wa Tanzania aliyekuwepo Saudi Arabia ilimlazimu ki-protokoli, kwenda uwanja wa ndege kuzungumza nae katika muda wa transit.

Pamoja na mambo mengine, Balozi huyo alimwambia Mwalimu Nyerere “…katika nchi hizi kuna mapesa mengi, na jamaa yaelekea wapo tayari kutusaidia mipango yetu mingi ya maendeleo, ilimradi tu, tuwaombe.” Nasikia Mwalimu alimjibu kwa mkato na kwa kiasi cha kuonekana kakasirishwa: “Hapana. Acha kabisa!”1

Ni dhahiri, mpishi wa mapinduzi na muungano, Mwalimu Nyerere, alikuwa ameacha “grand design” [mpango mkubwa] katika kuipata Zanzibar, bila shaka si kwa manufaa ya nchi (Tanganyika na Zanzibar), bali kwa manufaa ya wale wasiowatakia mema Waislam (pamoja na Waarabu ambao wengi wao ni Waislam).

Niliwahi kumuuliza mmoja wa Maraisi waliopita wa Zanzibar kama aliwahi kuuona waraka asilia [wa Muungano baina ya Zanzibar na Tanganyika] uliotiwa saini tarehe 26 April 1964, akaniambia hapana, hajawahi kuuona. Nikamuuliza tena, je, yule uliyemuachia nafasi yako unaweza kumuuliza kama kawahi kuuona? Akanijibu: “hapana haja ya kumuuliza, kwa sababu nafahamu kuwa nae pia hajauona.”

Kwa kawaida nchi inapotaka kujiunga na Umoja wa Mataifa (UN), hutowa taarifa ya mwezi mmoja na kisha kuwasilisha maelezo/vielelezo na vithibitisho kuwa ni nchi (yenye sifa ya kuwa na Utaifa), inayostahili heshma ya uwanachama huo. Nchi zilizokuwa zinapata uhuru wake toka ukoloni zilitoa taarifa ambayo tarehe yake ya mwisho ilisadifia na tarehe ya kupandisha bendera mpya.

Hivyo nchi iliyojisajili UN na kupewa kiti, bila shaka ilipobadili nafasi iliyoiondosha uwananchi wake, haikuondoka katika umoja huo bila ya taarifa yoyote. Bila shaka patakuwepo maelezo na vielelezo vilivyokubalika kiti chake kurudishwa, bendera yake kushushwa katika mlingoti wa UN, na majukumu yake kame vile michango n.k., kufutwa.

Vipi leo nchi kama hiyo isiwe na hati halisi ya makubaliano ya muungano ambayo wananchi waliona Sheikh Karume na Mwalimu Nyerere wakisaini na kupeana April 26, 1964? Na vipi nchi isiwe hata na zile nakala halisi za vielelezo japo vile vilivyopelekwa UN kuhusu suala zito la utaifa wake? Au hata ushahidi wa kisheria kuwa hakuna nchi inayoitwa “Tanganyika” au yakuwapi maelezo/vielelezo kuhusu kuongezeka kwa mambo ya muungano na nani alotia saini kwa niaba ya Zanzibar? Ni saini yake au ni ya nani na kwa ushahidi gani wa kisheria?

Wenye kuumizwa na yote hayo khasa ni Wazanzibari na si Watanganyika. Mapinduzi ndo yalioipinduwa nusu ya jamii ya Zanzibar ilioshinda uchaguzi [wa Julai 1963]. Mapinduzi ndo yaloleta muungano na kuyapinduwa makubaliano ya mwanzo ya muungano. Mapinduzi ndo yaliokifuta kiti cha Zanzibar UN kwa nia ambazo Wazanzibari bado hawajazitambuwa.

Mapinduzi ndio yaliomuondowa Al Hajj Aboud Jumbe madarakani, na kilichomponza khasa Mzee Jumbe ni pale alipolianzisha Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA); yakamtia ndani Maalim Seif Sharif Hamad; na ndiyo yaliyopelekea Dk. Salmin Amour akataliwe kuiingiza Zanzibar/Tanzania katika OIC na kuiakhirishia Zanzibar kutojiunga na taasisi hiyo. Ndiyo yaliyoifanya Katiba ya nchi itamke kuwa Raisi wa Zanzibar siyo tena Makamo wa Kwanza wa Rais wa muungano, kama ilivotamkwa 1964. Na ndiyo yaliyo “thibitisha” kuwa nchi ya Zanzibar sasa ni Mkoa kama mkoa wowote Tanzania. Na kubwa zaidi, hayo ndiyo yaliyofanywa kuwaonesha rasmi Wazanzibari kuwa hata ndani ya chama kilichoundwa kwa kuunganisha ASP na TANU, TANU, CCM Bara, ndiyo itakayoamua nani atagombea Uraisi Zanzibar.

Hivi sasa hakuna udhibiti kwa watu kutoka bara kuingia na kuishi Zanzibar. Lengo ni kubadilisha “demographic situation in favor” [hali ya wingi wa watu] ya bara katika miaka michache ijayo. Na hiyo population [idadi ya watu] mpya inaandaliwa kuwa “superior” katika uchumi, ilimu na ushawishi wa kisiasa. Wapemba kuunga mkono chama kinachoongozwa na Maalim Seif Sharifu, Mpemba, university graduate [mhitimu wa Chuo Kikuu] na mzoefu katika serikali na siasa; mtu ambae alikhitalifiana na Mwalimu Nyerere inakaa vizuri katika “grand design” [mkakati mkubwa] ya Mwalimu ya kuwatenga Waunguja. Nyerere alipoenda Zanzibar kueleza kwa nini CCM iliwafukuza Seif na wenzake, alimtaja Seif kama watu “…tuliokuwa tukiwapokea katika chama pasipo kuwachunguza kwa undani ili kujua asili yao na huko watokako…” Mbali ya maneno hayo, Nyerere pia alianzisha propaganda za kwamba watu wenye rangi ya kuchovya kama ya Seif, japo si Waarabu, alitaka watazamwe kama Waarabu. Siasa zao zitakuwa za kutaka kumrudisha Mwarabu Zanzibar.

Nyerere pia alianzisha lugha ya kampeni ya “kuwanasihi” watu wa bara (Tanganyika), kama moja ya propaganda zake za kujenga hoja ya kujitetea pale itakapoonekana kuwa bara inatumia nguvu kulazimisha muungano. Ikawa akisema mara kwa mara kuwa “…hawa wanataka kuuvunja muungano, mkiwaachia, watauana ovyo…sasa wameshaanza kugawanyika na kubaguana, kati ya Wazanzibari na Wazanzibara…Wapemba na Waunguja…” Ingawa hoja hiyo inakusudiwa kuwaomba Watanganyika “kuwanusuru” Wazanzibari ili wasi-jeuana, haikumpitikia Mwalimu wala wengineo kuhoji; kama Wazanzibari wamegawika kiasi hicho, msimamo wa uhalali wa muungano ukoje hivi sasa? Tanganyika hivi sasa imeungana na nani; Wapemba, Waunguja, Wazanzibari au Wazanzibara? Siri ya mapinduzi ya wazee inatowa jawabu lililo safi; Tanganyika iliungana na Waafrika kutoka bara kuwapinduwa Wapemba na Waunguja—Wazanzibari.

Katika mambo ya kudhulumiana nchi, wajanja hufanya kila njia kuepuka masuala ya mfumo. Watakupelekeni kwenye utendaji kazi. Huko mtazungumza na wale waliopewa kazi ya ku “run” government [kuendesha serikali]. Hamtokutana tena na wale wanao “rule” [wanaotawala]. Sioni sahihi kuutegemea Muwafaka badala ya Mkataba wa Muungano na Katiba na sheria za nchi, kutupa muelekeo wa kule tunakostahili kwenda. Hivyo hivyo, siamini kuwa mtu atayewekwa na madhalim katika madaraka ya nchi, ana uwezo wa kujua na kuipeleka nchi hiyo pahali pasipokuwa pale panapo takiwa na madhalim hao.

Kwa vyoyote vile, endapo tutatanabahi, tukatambua kuwa nguvu za wananchi ni muhimu kuliko chochote, na kwamba nguvu hizo hazipatikani ila kwa kuwatoa katika umasikini wa kiza cha ujinga wa ilimu duni; tunakoelekea si kubaya. Kuwatowa wananchi kunako giza la tunakotoka na Zanzibar kujiwakilisha nchi za nje, kuujenga na kuulinda uchumi wake, pamoja na kulindwa na Wazanzibari, ni kuzuri, na huko ndiko kwa kuanzia.
Aisee! Asante sana kwa mchango mzuri. Nina imani bado tunahitaji kujifunza zaidi kuhusu muungano wetu. Lakini kwaninin malalamiko haya yapo pande zote? Bara wanaona kama Zanzibar inanufaika zaidi na muungano kuliko Tanganyika. Mfano, Mikopo kutoka taasisi za fedha za kimataifa, hukopwa kwa jina la Tanzania na kisha marejesho ya mkopo hufanyika kwa jina la Tanzania. Je, kuna kipengele chochote katika katiba yetu ambacho hutaja asilimia ambazo zanzibar wanatakiwa kuchangia kurudisha mkopo hali kadhalika Tanganyika vile vile? Maana ninavyoelewa, mikopo hii imekuwa ikigawanywa bara na visiwani. Vipi kuhusu mgawanyo wa ajira katika pande zote mbili? vipi kuhusu mgawanyo wa matumizi wa rasilimali asilia za muungano?
 
Msikilize huyu Mwinyi , hii ni miezi miwili tu iliyopita, Zanzibar haipati chochote kwenye mikopo inayokopa Tanganyika / Tanzania

HAKUNA mahakama mbili. Ndio maana UAMSHO walishtakiwa na kufungwa bara.

HAKUNA majeshi mawili ndo maana jeshi linaitwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Na ndo maana wanajeshi wa JWTZ wako kote Zanzibar na bara.

Na HAKUNA sarafu mbili, kama Mshana alivyotaka kutudanganya danganya hapa kama watoto.

WEWE PASKALI NA MSHANA of all the people msijue kwamba Zanzibar hawana hela yao na jeshi lao na mahakama ???? Au mnaleta mizaha mizaha na uongo wa makusudi ambao kizungu wanauita bull crap ????

Sasa umekuja na ki rubbish kipya eti nchi moja ndio yenye sovereignty. Nchi gani ndio ina sovereignty, Tanganyika au Zanzibar ?
Uamsho walishtakiwa ila hawakufungwa.
 
Zanzibar siyo dola huru kwa sababu:

Haina kiti UN na haitambuliki Kimataifa kama dola yaani state. Vigezo vingine vya kuwa dola vipo ila kimojawapo pekee cha uhuru wa Kimataifa yaani external sovereignty haina.
Mkuu, bado unaendelea na huu msimamo, au umebadilika ?
 
Mkuu, bado unaendelea na huu msimamo, au umebadilika ?
Siyo msimamo wangu. Ni msimamo wa Sheria za Tanzania na zile za Kimataifa. Rejea pia case ya Machano Hamis Machano iliyoamuliwa na Mahakama ya Rufaa ya Tanzania
 
Zanzibar ni chawa wa Tanganyika.
Kama Zanzibar ni Chawa wa Tanganyika basi huyo chawa ni mkubwa kiasi kwamba humfunika Tanganyika kwa kiasi kikubwa saana,

Kifupi ni kwamba Tanganyika lilikuwa koloni la wa Oman, muda wote walipokuwa Zanzibar, Hivyo kabla ya uhuru kwa chini chini kulikuwa mapatano ya kuipa uhuru Tanganyika but Not Zanzibar ili waoman waendelee kutawala remotely, and this has been accomplished.

Sent from my TA-1004 using JamiiForums mobile app
 
Ukinambia ni sehemu ya Tanzania nitakuuliza maswali yafuatayo:

1. Kwanini Watanganyika hawaruhusiwi kumiliki ardhi Zanzibar?

2. Kwanini ni ngumu ajira za Zanzibar kuhusisha Watanganyika?

3. Kwanini wana rais wao na bendera yao?

4. Kwanini wana taasisi zao zinazojitegemea kama mahakama, bunge, tume ya uchaguzi nk?

5. Kwanini timu za Zanzibar zinaiwakilisha Zanzibar kama nchi kwenye mashindano mbalimbali ya CAF kwa ngazi ya vilabu?

6. Kwanini taasisi zao zinaendeshwa tofauti kabisa na Tanzania, mfano kule watu wanatibiwa bure kwa hospitali za serikali, gharama za umeme ni nafuu sana nk?

Ukinambia Zanzibar ni nchi huru nitakuuliza maswali yafuatayo:

1. Kwanini haina amiri jeshi mkuu kwa maana ya kwamba haina jeshi linalojitegemea?

2. Kwanini Tanzania ikikopa Zanzibar wanapata fungu lao tena kwa uwiano usio sawa (Zanzibar inapata ratio kubwa) huku ikiwa mlipaji wa mkopo akiwa Tanzania bara pekee.

3. Kwanini haina sarafu yake yenyewe?

Mtazamo wangu: Muungano una mapungufu mengi.

Huwezi kuwa na Nchi ambayo kuna wakati inakuwa nchi kamili na kuna wakati inakuwa sehemu ya nchi nyingine.

Nadhani ni muda sahihi Zanzibar kuwa mkoa wa Tanzania, ama tuwaachie nchi yao wajitegemee.

Inavyoonekana ni kuwa Nyerere alitaka kuwalaghai Wazanzibari mwisho wa siku akajikuta anatengeneza muungano usioeleweka na sasa madhara yake yapo dhahiri.

Hoja ya usalama kwangu haina mashiko! Kama tumeweza kuilinda mipaka yetu yote dhidi ya nchi korofi zinazotuzunguka tutashindwaje kujilinda dhidi ya Zanzibar?
Kasome Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema hivi endapo itatungwa sheria yoyote inayokwenda kinyume na Katiba hii ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hiyo sheria ni batili kwa hiyo ile sheria iliyotungwa na baraza la Wawakilishi kwamba Zanzinzibar ni nchi ni batili.
 
Ndiyo maana Tanganyika hulazimisha kumweka kibaraka wao kila unapokuja Huo unaoitwa uchaguzi
 
Kama Zanzibar ni Chawa wa Tanganyika basi huyo chawa ni mkubwa kiasi kwamba humfunika Tanganyika kwa kiasi kikubwa saana,

Kifupi ni kwamba Tanganyika lilikuwa koloni la wa Oman, muda wote walipokuwa Zanzibar, Hivyo kabla ya uhuru kwa chini chini kulikuwa mapatano ya kuipa uhuru Tanganyika but Not Zanzibar ili waoman waendelee kutawala remotely, and this has been accomplished.

Sent from my TA-1004 using JamiiForums mobile app
Unaweza kutuletea ushahidi wa ulichokiandika
 
Ukinambia ni sehemu ya Tanzania nitakuuliza maswali yafuatayo:

1. Kwanini Watanganyika hawaruhusiwi kumiliki ardhi Zanzibar?

2. Kwanini ni ngumu ajira za Zanzibar kuhusisha Watanganyika?

3. Kwanini wana rais wao na bendera yao?

4. Kwanini wana taasisi zao zinazojitegemea kama mahakama, bunge, tume ya uchaguzi nk?

5. Kwanini timu za Zanzibar zinaiwakilisha Zanzibar kama nchi kwenye mashindano mbalimbali ya CAF kwa ngazi ya vilabu?

6. Kwanini taasisi zao zinaendeshwa tofauti kabisa na Tanzania, mfano kule watu wanatibiwa bure kwa hospitali za serikali, gharama za umeme ni nafuu sana nk?

Ukinambia Zanzibar ni nchi huru nitakuuliza maswali yafuatayo:

1. Kwanini haina amiri jeshi mkuu kwa maana ya kwamba haina jeshi linalojitegemea?

2. Kwanini Tanzania ikikopa Zanzibar wanapata fungu lao tena kwa uwiano usio sawa (Zanzibar inapata ratio kubwa) huku ikiwa mlipaji wa mkopo akiwa Tanzania bara pekee.

3. Kwanini haina sarafu yake yenyewe?

Mtazamo wangu: Muungano una mapungufu mengi.

Huwezi kuwa na Nchi ambayo kuna wakati inakuwa nchi kamili na kuna wakati inakuwa sehemu ya nchi nyingine.

Nadhani ni muda sahihi Zanzibar kuwa mkoa wa Tanzania, ama tuwaachie nchi yao wajitegemee.

Inavyoonekana ni kuwa Nyerere alitaka kuwalaghai Wazanzibari mwisho wa siku akajikuta anatengeneza muungano usioeleweka na sasa madhara yake yapo dhahiri.

Hoja ya usalama kwangu haina mashiko! Kama tumeweza kuilinda mipaka yetu yote dhidi ya nchi korofi zinazotuzunguka tutashindwaje kujilinda dhidi ya Zanzibar?
Hapo mwisho umejijibu mwenyewe. Sera ya Ccm ni Serekali mbili kuelekea moja. Yaani nia na madhumuni ya CCM ni kuona siku moja Zanzibar inamezwa na kua mkoa. Haya unayoyaona sana ni kama peremende tu tumepewa Wazanzibari na in fact ni small price Tanganyika paid to swallow Zanzibar.
 
Msikilize huyu Mwinyi , hii ni miezi miwili tu iliyopita, Zanzibar haipati chochote kwenye mikopo inayokopa Tanganyika / Tanzania

mwanzo nlikuwa na hasira sana nkidhan wanapata mgao na walipaji ni bara lkn baada ya kuona hii clip kidg afadhal acha wanyonywe tu kama bara ndo anakopa na wanalipa wao wenyewe kuna shida gani na ili haya yaishe zanzibar ifanywe mkoa tu lakini kilichopo sasa lawama hazitakuj isha wabara tunalaum kama kote ni tanzania kwann tuingie kwa vibal zenji na kwann haturuhusiwi kumiliki ardhi wakat huo wazanzibar bara wamejaa na wanamiliki ardhi ,kuwe na rais mmoja, bunge moja na mamlaka moja kama ilivyo kwenye jeshi hapa ndo kelele zitaisha unless otherwise Muungano ufe maan kila mmoja ataona ananyonywa na mwenzie
 
Ndiyo maana Tanganyika hulazimisha kumweka kibaraka wao kila unapokuja Huo unaoitwa uchaguzi
Hata ungekuwa ni wewe kutoka huko unakodhani wanakandamizwa ni lazima uitii Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila kujali anayekandamizwa ni nani kinyume na hapo utakandamizwa wewe.
 
Hata ungekuwa ni wewe kutoka huko unakodhani wanakandamizwa ni lazima uitii Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bila kujali anayekandamizwa ni nani kinyume na hapo utakandamizwa wewe.
Hiyo Katiba ianze kufuatwa na hao walioiandika . Chaguzi zote zinafanywa kwa kuzivunja katiba na kanuni Za uchaguzi. Tuanzie hapo kwanza
 
Back
Top Bottom