Zanzibar ni nchi huru au ni sehemu ya Tanzania?

Zanzibar Is land
1. Ina katiba
2. Ina wimbo
3. Ina rais
4. Ina waziri mkuu. Kule anaitwa waziri kiongozi
5. Ina bunge
6. Ina serikali kamili yaani baraza la mawaziri
6. Ina mipaka

Jeshi na currency tunachangia
 
Jana nikiwa sehemu fulani nilisikia baadhi ya wasomi wakijadili mambo kadhaa hasa wakiitaja nchi iitwayo Zanzibar.

Kwa walio na ufahamu vizuri nitaomba msaada hapa. Kwa uelewa wangu, ili sehemu ya ardhi inayokaliwa na watu iitwe nchi(state), ni lazime pawepo na mambo yafuatayo:
1. Mipaka kamili inayotambulika kimataifa
2. Serikali
3. Watu na makazi
4. Iwe na uwezo wa kuingia makubaliano na nchi nyingine bila kuingiliwa au kuhitaji ruhusa kutoka sehemu nyingine.

Ikiwa sehemu inajitosheleza kwa mambo yote hayo manne basi, huitwa na kutambulika kama nchi.

Lakini sehemu hiyo (nchi) inaweza kupoteza sifa ya kuitwa nchi na jumuia za kimataifa kama:
1. Itaungana na nchi nyingine kutengeneza nchi au taifa moja
2. Itakubali kutawaliwa na nchi nyingine
3. Mipaka yake itamezwa na nchi nyingine
4. Itagawanyika katika sehemu ndogondogo zenye mamlaka kamili

Je, baada ya Zanzibar kuungana na Tanganyika na kuunda serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bado Zanzibar inatambulika kama nchi? ni vigezo gani huifanya zanzibar kuitwa nchi?
Ameandika MALCOM LUMUMBA
Nimepata elimu nzuri sana hapa,,,,
Zanzibar siyo nchi (Country), bali ni dola(State) inayounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu muungano uliwekwa kimkataba na hati idhini (Union Charter/Articles of the Union). Hivyo Zanzibar ilipunguza sehemu ya uhuru wake kujitawala (State Sovereignty) kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pili, suala la ajira lina pembe mbili. Kuna pembe ya Muungano na pembe ya Zanzibari. Watanganyika wapo Zanzibari na wanafanya kazi, lakini ni katika zile sehemu za mambo yanayohusu Muungano tu. Jambo kama hili liko hata kule Hong-Kong Uchina, na maisha yanaenda kama kawaida.

Tatu, suala la bendera siyo shida, maana bendera ni utambulisho tu (Emblem of Identity). Hata wewe ukiamua kuwa na bendera yako unaweza kuitengeneza na kuisajili kupitia HAKI-MILIKI (Intellectual Property). Nchini Marekani kila jimbo lina bendera yake na maisha yanaenda vizuri tu. Tena wanaenda mbali kabisa na kutumia bendera (The Confederate Flag) ya madola ya kusini (Dixie-Land) ambayo yaliasi muungano.

Nne, nadhani jina Raisi ni cheyo tu, hivyo unaweza leo ukamua kumuita Raisi wa Zanzibari wa Zanzibar Waziri Mkuu wa visiwani, Gavana,Sultani au Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Lakini muhimu kujiuliza ni hili: Je, madaraka yake ya Uraisi yanaishia wapi na ukimlinganisha na Raisi mwenzake ??? Utakuja kufahamu ni kwamba Uraisi wa Zanzibari hauvuki maji ya Pemba na Unguja, lakini Raisi wa Tanganyika madaraka yake yanavuka maji na kufika Pemba hadi Unguja, katika ngazi ya kitaifa hadi kichama.

Tano, mashirikisho mengi huwa na mihimili na taasisi zinazojitegemea kama mahakama, bunge na serikali zao. Wengine kama Ethiopia walienda mbali zaidi kuwa hata vikosi vyao binafsi vya ulinzi. Nchini Marekani kuna baadhi ya majimbo yana nguvu sana hadi kumuwezesha Gavana kutoa adhabu ya kifo. Hivyo hili la Zanzibar lisikutatize kabisa mkuu.

Sita, kuhusu uwakilishi wa Zanzibari kwenye siasa za kimataifa hilo ni jambo la kawaida sana maana sheria za kimataifa hazikatazi. Tokea mwaka 1945 hadi 1991 Umoja wa Kisovieti ulikuwa una viti vitatu kule Umoja wa Mataifa ambavyo ni vya USSR, Ukraine na Belarus ilhali wote wanatoka kwenye nchi moja iitwayo The Union of Soviets Socialist Republics (USSR). Hivyo hapa napo binafsi sioni tatizo kabisa.

Saba, kuhusu taasisi kujiendesha kwa utofauti hilo linatokana na uwepo wa madaraka ya ndani ya kujiendesha (Internal Sovereignty/Semi-Autonomy). Hata nchini Uchina, Hong-Kong inajiendesha kitofauti kabisa, nchini Marekani jimbo kama California ambalo huwa linajiendesha kitofauti kabisa na sera zake za kiliberi. Ambacho wengi kinatukera ni kwamba Tanganyika kutoweza kujiamulia mambo yake binafsi. Tunalitaka taifa letu.

Nane, hili la mikopo nakubaliana na wewe kabisa. Zanzibari haitakiwi ipate fungu lolote lile kwenye masuala yasiyo ya muungano (Non-Union Matters) ambayo yanaihusu Tanganyika. Mbaya zaidi hili la kukopa kupitia mngongo wa Tanganyika, ilhali sheria za kimataifa zinaruhusu Zanzibar iweze kukopa yenyewe binafsi. Katiba ya Ujerumani inaruhusu Ujerumani Mashariki na Ujerumani Magharibi kuingia katika mikataba binafsi ya kimataifa na nchi nyingine. Hivyo Ujerumani Mashariki inaruhusiwa hadi kukopa nje, ili mradi tu itoe taarifa kwa serikali ya Muungano.

Tunataka Zanzibar nao wakope kwa jina lao, maana inaruhusiwa kabisa. Huu ujanja wa kutaka kuiumiza Tanganyika, umenza kututia kinyaa watu wengi na kutukera sana. Hasahasa unapofanywa na Raisi Mzanzibari ambaye kiuhalisia hakutakuwa kabisa kugusa mambo ya Tanganyika.

Tisa, kuhusu ardhi. Wazanzibari ni watu wenye midomo sana na wanapenda kuongea siasa zao ambazo zimejaa ubaguzi wa rangi na dini. Lakini ukweli mchungu ni kwamba kuna mambo ambayo Tanganyika ikitutumua misuli, lazima wataumia sana. Mwaka 2014 ilifanyika tafiti na kufahamika kwamba kule Zanzibar (1 Square Kilometer inakaliwa na watu 200) wakati huku Tanganyika (1 Square Kilometer inaliwa na watu 20-30).

Tukisema tuanze kuwakazia, nadhani watu kama Raisi Hussein Mwinyi, Raisi Samia, Bakhresa na wapemba wengine ambao wako Dar es Salaam kisheria inabidi wamiliki ardhi kama wawekezaji kupitia kitu kiitwacho The Derivetive Right. Lakini jambo jingine kubwa utafiti wa mafuta ya Zanzibar ulifanywa kipindi cha Raisi Magufuli na kutambulika kwamba baadhi ya miamba yenye mafuta ambayo Zanzibari ingechimba imefika hadi Tanganyika, tena sehemu kubwa iko Tanganyika.

Kiukweli mimi natamani Tanganyika irudi, ikiwezekana kabisa tuvunje huu muungano.
 
Jana nikiwa sehemu fulani nilisikia baadhi ya wasomi wakijadili mambo kadhaa hasa wakiitaja nchi iitwayo Zanzibar.

Kwa walio na ufahamu vizuri nitaomba msaada hapa. Kwa uelewa wangu, ili sehemu ya ardhi inayokaliwa na watu iitwe nchi(state), ni lazime pawepo na mambo yafuatayo:
1. Mipaka kamili inayotambulika kimataifa
2. Serikali
3. Watu na makazi
4. Iwe na uwezo wa kuingia makubaliano na nchi nyingine bila kuingiliwa au kuhitaji ruhusa kutoka sehemu nyingine.

Ikiwa sehemu inajitosheleza kwa mambo yote hayo manne basi, huitwa na kutambulika kama nchi.

Lakini sehemu hiyo (nchi) inaweza kupoteza sifa ya kuitwa nchi na jumuia za kimataifa kama:
1. Itaungana na nchi nyingine kutengeneza nchi au taifa moja
2. Itakubali kutawaliwa na nchi nyingine
3. Mipaka yake itamezwa na nchi nyingine
4. Itagawanyika katika sehemu ndogondogo zenye mamlaka kamili

Je, baada ya Zanzibar kuungana na Tanganyika na kuunda serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bado Zanzibar inatambulika kama nchi? ni vigezo gani huifanya zanzibar kuitwa nchi?
*Kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar ya 2010£
 
Nchi gani unawakusanya raia wake kwa filimbi na unazunguka ardhi yote kwa bicycle kwa less than 4hrs
 
Je, baada ya Zanzibar kuungana na Tanganyika na kuunda serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bado Zanzibar inatambulika kama nchi? ni vigezo gani huifanya zanzibar kuitwa nchi?
Kabla ya muungano, mataifa mawili ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar yalikuwa mataifa kamili, yakaungana kwa muungano wa union, na kuunda taifa jipya la JMT, hivyo mataifa yote mawili kupoteza utaifa wake, yaani sovereignty na sasa mataifa hayo yote mawili hayapo, dead and buried, kilichopo ni taifa jipya la JMT.

Ila kitaifa muungano wetu ni muungano wa federation, wenye two federal states, Tanzania Bara, iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar iliyokuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

Hivyo kimataifa Zanzibar sio nchi, ni sehemu ya JMT, ila kitaifa Zanzibar ni nchi, yenye eneo lake, mipaka yake, serikali yake, rais wake, Bunge lake, Mahakama yake, bendera yake, wimbo wake wa taifa, taifa na raia wake waitwao wakaazi, pia ina majeshi yake ya KMKM, JKU na vikosi vya SMZ na kuhesabika ni nchi ya Zanzibar ambayo ni moja ya nchi mbili zinazounda JMT.

Hivyo Zanzibar sii nchi kimataifa, nchi ni moja tuu ya JMT, ila kitaifa, Zanzibar ni nchi ndani ya nchi.

P
 
Ni nchi inakidhi vigezo vyote
Watu
Bunge
Mipaka
Jeshi
Sarafu
Wimbo wa taifa
Bendera
Zanzibar haina sarafu na haina Jeshi.

Nilitegemea ujue kitu kama hicho, uko muda mrefu hapa na una jina kubwa sana we mtu. Sasa usijiaibishe.
 
Hivyo Zanzibar sii nchi kimataifa, nchi ni moja tuu ya JMT, ila kitaifa, Zanzibar ni nchi ndani ya nchi.
Rubbish.

Hayo ni maelezo yaliyotolewa bungeni na douchebag mmoja aliyeamua iwe hivyo. Na wewe unameza tu kama sponge bila kuzingatia sheria, katiba na hati ya muungano zinasemaje.

Duniani hakuna nchi ya kitaifa na ya kitaifa. That"s bull crap.
 
Huu ndio uzuri mmoja wa JF, uelimishaji umma, huna haja ya hairs na kutokana watu humu, rubbish, bull crap, huu ni uwanja wa kuelimishana, muungano wetu ni unique haupo pengine popote duniani!, muungano wetu kimataifa tuu ndio muungano wa union uliounda nchi moja ya JMT, lakini kitaifa, muungano wetu sio union, ni federation yenye nchi mbili, katiba mbili, marais wawili, mabunge mawili, Mahakama mbili, nyimbo mbili za taifa, bendera mbili, majeshi mawili, sarafu ndio moja. Tofauti pekee kati ya nchi hizi mbili ni moja ndio yenye sovereignty na nyingine haina.
P
 
Kabla ya muungano, mataifa mawili ya Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar yalikuwa mataifa kamili, yakaungana kwa muungano wa union, na kuunda taifa jipya la JMT, hivyo mataifa yote mawili kupoteza utaifa wake, yaani sovereignty na sasa mataifa hayo yote mawili hayapo, dead and buried, kilichopo ni taifa jipya la JMT.

Ila kitaifa muungano wetu ni muungano wa federation, wenye two federal states, Tanzania Bara, iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika na Tanzania Visiwani au Tanzania Zanzibar iliyokuwa Jamhuri ya Watu wa Zanzibar.

Hivyo kimataifa Zanzibar sio nchi, ni sehemu ya JMT, ila kitaifa Zanzibar ni nchi, yenye eneo lake, mipaka yake, serikali yake, rais wake, Bunge lake, Mahakama yake, bendera yake, wimbo wake wa taifa, taifa na raia wake waitwao wakaazi, pia ina majeshi yake ya KMKM, JKU na vikosi vya SMZ na kuhesabika ni nchi ya Zanzibar ambayo ni moja ya nchi mbili zinazounda JMT.

Hivyo Zanzibar sii nchi kimataifa, nchi ni moja tuu ya JMT, ila kitaifa, Zanzibar ni nchi ndani ya nchi.

P
Shukran sana kwa ufafanuzi mzuri.
 
Rubbish.

Hayo ni maelezo yaliyotolewa bungeni na douchebag mmoja aliyeamua iwe hivyo. Na wewe unameza tu kama sponge bila kuzingatia sheria, katiba na hati ya muungano zinasemaje.

Duniani hakuna nchi ya kitaifa na ya kitaifa. That"s bull crap.
Tuelimishane mkuu.
 
Jana nikiwa sehemu fulani nilisikia baadhi ya wasomi wakijadili mambo kadhaa hasa wakiitaja nchi iitwayo Zanzibar.

Kwa walio na ufahamu vizuri nitaomba msaada hapa. Kwa uelewa wangu, ili sehemu ya ardhi inayokaliwa na watu iitwe nchi(state), ni lazime pawepo na mambo yafuatayo:
1. Mipaka kamili inayotambulika kimataifa
2. Serikali
3. Watu na makazi
4. Iwe na uwezo wa kuingia makubaliano na nchi nyingine bila kuingiliwa au kuhitaji ruhusa kutoka sehemu nyingine.

Ikiwa sehemu inajitosheleza kwa mambo yote hayo manne basi, huitwa na kutambulika kama nchi.

Lakini sehemu hiyo (nchi) inaweza kupoteza sifa ya kuitwa nchi na jumuia za kimataifa kama:
1. Itaungana na nchi nyingine kutengeneza nchi au taifa moja
2. Itakubali kutawaliwa na nchi nyingine
3. Mipaka yake itamezwa na nchi nyingine
4. Itagawanyika katika sehemu ndogondogo zenye mamlaka kamili

Je, baada ya Zanzibar kuungana na Tanganyika na kuunda serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bado Zanzibar inatambulika kama nchi? ni vigezo gani huifanya zanzibar kuitwa nchi?
Hili swali lilishajibiwa miaka mingi iliyopita vinginevyo uzi huu ni kujaza nafasi bila umuhimu. Uondolee mbali
 
Kuna kipengele kwamba ili iwe nchi kamili, ni lazima itambuliwe na jumuia nyingine za kimataifa sambamba na kuwa na uakilishi UN.
Mipango hiyo inaendelea , na hata code ya namba ya simu yao siyo +255 , wao yao ni +259
 
Back
Top Bottom