Zanzibar ni nchi huru au ni sehemu ya Tanzania?

Zanzibar ni nchi huru au ni sehemu ya Tanzania?

Labda kwa mambo madogo madogo sio kwa jambo kubwa kama hilo !
Yaani uchaguzi wa Rais Na wabunge unaona jambo dogo huku watu wanapotezwa maisha Na wengine kuuliwa ? Hongera sana
 
Yaani uchaguzi wa Rais Na wabunge unaona jambo dogo huku watu wanapotezwa maisha Na wengine kuuliwa ? Hongera sana
Pole sana kwa kupotelewa na ndugu zako..naomba tusahau yaliyopita tusonge mbele kuipata serikali moja ya JMT.

Kubaki na hasira..chuki na visasi haitosaidia.

#MaendeleoHayanaChama
 
Pole sana kwa kupotelewa na ndugu zako..naomba tusahau yaliyopita tusonge mbele kuipata serikali moja ya JMT.

Kubaki na hasira..chuki na visasi haitosaidia.

#MaendeleoHayanaChama
Mbona unabadilisha hos angani?

Tunaongelea kuvunjwa katiba au unaota mchana?
 
D
Yaani uchaguzi wa Rais Na wabunge unaona jambo dogo huku watu wanapotezwa maisha Na wengine kuuliwa ? Hongera sana
Duh ! Sina maana Hiyo huenda nimekuelewa vibaya au umenielewa vibaya ! Sorry tuachie hapo !
 
Jana nikiwa sehemu fulani nilisikia baadhi ya wasomi wakijadili mambo kadhaa hasa wakiitaja nchi iitwayo Zanzibar.

Kwa walio na ufahamu vizuri nitaomba msaada hapa. Kwa uelewa wangu, ili sehemu ya ardhi inayokaliwa na watu iitwe nchi(state), ni lazime pawepo na mambo yafuatayo:
1. Mipaka kamili inayotambulika kimataifa
2. Serikali
3. Watu na makazi
4. Iwe na uwezo wa kuingia makubaliano na nchi nyingine bila kuingiliwa au kuhitaji ruhusa kutoka sehemu nyingine.

Ikiwa sehemu inajitosheleza kwa mambo yote hayo manne basi, huitwa na kutambulika kama nchi.

Lakini sehemu hiyo (nchi) inaweza kupoteza sifa ya kuitwa nchi na jumuia za kimataifa kama:
1. Itaungana na nchi nyingine kutengeneza nchi au taifa moja
2. Itakubali kutawaliwa na nchi nyingine
3. Mipaka yake itamezwa na nchi nyingine
4. Itagawanyika katika sehemu ndogondogo zenye mamlaka kamili

Je, baada ya Zanzibar kuungana na Tanganyika na kuunda serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bado Zanzibar inatambulika kama nchi? ni vigezo gani huifanya zanzibar kuitwa nchi?
 
"Zanzibar siyo nchi".

By Mizengo Pinda (former PM)

Hii imekaaje??
52AD5B6D-7497-4097-923B-72A6C7C8A7F4.jpeg
 
"Zanzibar siyo nchi".

By Mizengo Pinda (former PM)
Hii kauli ya Mizengo Pinda, July 2008, ilipingwa vikali na wajumbe wa baraza la wawakilishi huku wakitaka zanzibar iendelee kutambulika kama nchi.
 
Back
Top Bottom