Zanzibar ni nchi huru au ni sehemu ya Tanzania?

Zanzibar ni nchi huru au ni sehemu ya Tanzania?

Hili swali lilishajibiwa miaka mingi iliyopita vinginevyo uzi huu ni kujaza nafasi bila umuhimu. Uondolee mbali
Japo ni kweli hili swali lilishajibiwa siku nyingi nyuma, kila siku wanazaliwa wapya wasiojua kilitokea nini jana, hivyo wakiuliza, nyinyi mliokuwepo hiyo jana, muwaelimishe.
P
 
Zanzibar Is land
1. Ina katiba
2. Ina wimbo
3. Ina rais
4. Ina waziri mkuu. Kule anaitwa waziri kiongozi
5. Ina bunge
6. Ina serikali kamili yaani baraza la mawaziri
6. Ina mipaka


Jeshi na currency tunachangia
Wana jeshi lao la JKU
 
Tanzania ni Muungano wa sio nchi mbili. Tanganyika na Zanzibar. Nilimsikia mwendawazimu mmoja akisema.
 
Zanzibar Is land
1. Ina katiba
2. Ina wimbo
3. Ina rais
4. Ina waziri mkuu. Kule anaitwa waziri kiongozi
5. Ina bunge
6. Ina serikali kamili yaani baraza la mawaziri
6. Ina mipaka


Jeshi na currency tunachangia
Unaweza kutusaidi kufahamu mipaka ya Tanganyika na Zanzibar tuanzia hapo
 
Je, baada ya Zanzibar kuungana na Tanganyika na kuunda serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bado Zanzibar inatambulika kama nchi? ni vigezo gani huifanya zanzibar kuitwa nchi?
Baada ya Zanzibar kutekwa na Tanganyika.
 
Mipango hiyo inaendelea , na hata code ya namba ya simu yao siyo +255 , wao yao ni +259
Baadhi hatujawahi kufika Zanzibar. Je, kwa mtanzania atokae Tanganyika, atalazimika kuwa na pasipoti ya kusafiriria anapoingia Zanzibar sawa na raia kutoka nchi za kigeni? Kuna masharti yoyote au hakuna?
 
Jana nikiwa sehemu fulani nilisikia baadhi ya wasomi wakijadili mambo kadhaa hasa wakiitaja nchi iitwayo Zanzibar.

Kwa walio na ufahamu vizuri nitaomba msaada hapa. Kwa uelewa wangu, ili sehemu ya ardhi inayokaliwa na watu iitwe nchi(state), ni lazime pawepo na mambo yafuatayo:
1. Mipaka kamili inayotambulika kimataifa
2. Serikali
3. Watu na makazi
4. Iwe na uwezo wa kuingia makubaliano na nchi nyingine bila kuingiliwa au kuhitaji ruhusa kutoka sehemu nyingine.

Ikiwa sehemu inajitosheleza kwa mambo yote hayo manne basi, huitwa na kutambulika kama nchi.

Lakini sehemu hiyo (nchi) inaweza kupoteza sifa ya kuitwa nchi na jumuia za kimataifa kama:
1. Itaungana na nchi nyingine kutengeneza nchi au taifa moja
2. Itakubali kutawaliwa na nchi nyingine
3. Mipaka yake itamezwa na nchi nyingine
4. Itagawanyika katika sehemu ndogondogo zenye mamlaka kamili

Je, baada ya Zanzibar kuungana na Tanganyika na kuunda serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bado Zanzibar inatambulika kama nchi? ni vigezo gani huifanya zanzibar kuitwa nchi?
Zanzibar ni nchi iliyovamiwa na Tanganyika chini ya Laanatullahi Nyerere , lengo likiwa ni kuupiga vita uislamu na kuifanya Nchi hii kuwa ni sehemu ya Tanganyika huko mbeleni.

Januari 1964 Jeshi la nyerere liliivamia na kuilkalia zanzibar huku likimkamata Waziri Mkuu wake aliyechaguliwa na wananchi chini ya Tume huru ya Uchaguzi ,Mohammed Shamte mzaliwa wa Ole Pemba.

Pamoja naye walikamatwa mawaziri wake wote na wote walipelekwa Tanganyika na kufungwa jela zaidi ya miaka 10 bila kupelekwa mahakamani.

Hii ndio hali ya nchi iitwayo Zanzibar na mpaka leo wananchi wake wanapitia mateso chini ya vibaraka wanaowekwa na Tanganyika.
 
Jana nikiwa sehemu fulani nilisikia baadhi ya wasomi wakijadili mambo kadhaa hasa wakiitaja nchi iitwayo Zanzibar.

Kwa walio na ufahamu vizuri nitaomba msaada hapa. Kwa uelewa wangu, ili sehemu ya ardhi inayokaliwa na watu iitwe nchi(state), ni lazime pawepo na mambo yafuatayo:
1. Mipaka kamili inayotambulika kimataifa
2. Serikali
3. Watu na makazi
4. Iwe na uwezo wa kuingia makubaliano na nchi nyingine bila kuingiliwa au kuhitaji ruhusa kutoka sehemu nyingine.

Ikiwa sehemu inajitosheleza kwa mambo yote hayo manne basi, huitwa na kutambulika kama nchi.

Lakini sehemu hiyo (nchi) inaweza kupoteza sifa ya kuitwa nchi na jumuia za kimataifa kama:
1. Itaungana na nchi nyingine kutengeneza nchi au taifa moja
2. Itakubali kutawaliwa na nchi nyingine
3. Mipaka yake itamezwa na nchi nyingine
4. Itagawanyika katika sehemu ndogondogo zenye mamlaka kamili

Je, baada ya Zanzibar kuungana na Tanganyika na kuunda serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bado Zanzibar inatambulika kama nchi? ni vigezo gani huifanya zanzibar kuitwa nchi?
Nikiwanja Cha ujinga
 
Nenda ka search ktk orodha ya nchi za ulimwengu alafu urudi hapa, ule ni mkoa
 
Baadhi hatujawahi kufika Zanzibar. Je, kwa mtanzania atokae Tanganyika, atalazimika kuwa na pasipoti ya kusafiriria anapoingia Zanzibar sawa na raia kutoka nchi za kigeni? Kuna masharti yoyote au hakuna?

Katika jitihada zake za kuupiga vita uislamu Zanzibar Laanatullahi Nyerere na chama chake cha CCM wamelazimisha hii nchi kuwa ni wakfu kwa mtu yeyote kuingia bila viza wala passport kutokea Tanganyika. awe Mrundi , Mkenya , Mganda au yeyote hata mzungu , mchina muhindi yuko huru kuingia Zanzibar kwa kuitumia Tanganyika
 
Nenda ka search ktk orodha ya nchi za ulimwengu alafu urudi hapa, ule ni mkoa



Kutoka kitabu, kwaheri ukoloni kwaheri uhuru




Mzee Faraji

Nilipata kusikia kutoka kwa mmoja wa Marais wa zamani wa Zanzibar, kuwa manunguniko na madai ya Wazanzibari yaliyoanza katika miaka ya 70; kuhusu kuvunjwa mkataba wa 1964, kwa manufaa ya Tanganyika; madai hayo yalikuwa yakiwaudhi sana viongozi wa Tanganyika.

Hivyo siku moja Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje, akamwambia Raisi wa Muungano (wakati huo) Mwalimu Nyerere, kwamba kwanini hawavunji mbali muungano ili wapumzike na “kelele” za Wazanzibari? Inasemekana Mwalimu Nyerere alimjibu kwa kumkatalia kwa kusema mengi pamoja na “…tukiwaachia tu, utaona jinsi mapesa ya Waislamu na Waarabu yatakavyo miminika Zanzibar…hapana, hatuwaachii.”

Laiti shida ya Mwalimu Nyerere ingelikuwa nae anazitaka pesa hizo kwa ajili ya Tanganyika, kisa kifuatacho kisingelitokea. Kwa mujibu wa kisa hiki kama kilivyosimuliwa na Rais huyo wa zamani [wa Zanzibar], Mwalimu Nyerere, wakati huo akiwa ameshastaafu, alipita akiwa safarini, katika uwanja wa ndege Jeddah, Saudi Arabia. Balozi wa Tanzania aliyekuwepo Saudi Arabia ilimlazimu ki-protokoli, kwenda uwanja wa ndege kuzungumza nae katika muda wa transit.

Pamoja na mambo mengine, Balozi huyo alimwambia Mwalimu Nyerere “…katika nchi hizi kuna mapesa mengi, na jamaa yaelekea wapo tayari kutusaidia mipango yetu mingi ya maendeleo, ilimradi tu, tuwaombe.” Nasikia Mwalimu alimjibu kwa mkato na kwa kiasi cha kuonekana kakasirishwa: “Hapana. Acha kabisa!”1

Ni dhahiri, mpishi wa mapinduzi na muungano, Mwalimu Nyerere, alikuwa ameacha “grand design” [mpango mkubwa] katika kuipata Zanzibar, bila shaka si kwa manufaa ya nchi (Tanganyika na Zanzibar), bali kwa manufaa ya wale wasiowatakia mema Waislam (pamoja na Waarabu ambao wengi wao ni Waislam).

Niliwahi kumuuliza mmoja wa Maraisi waliopita wa Zanzibar kama aliwahi kuuona waraka asilia [wa Muungano baina ya Zanzibar na Tanganyika] uliotiwa saini tarehe 26 April 1964, akaniambia hapana, hajawahi kuuona. Nikamuuliza tena, je, yule uliyemuachia nafasi yako unaweza kumuuliza kama kawahi kuuona? Akanijibu: “hapana haja ya kumuuliza, kwa sababu nafahamu kuwa nae pia hajauona.”

Kwa kawaida nchi inapotaka kujiunga na Umoja wa Mataifa (UN), hutowa taarifa ya mwezi mmoja na kisha kuwasilisha maelezo/vielelezo na vithibitisho kuwa ni nchi (yenye sifa ya kuwa na Utaifa), inayostahili heshma ya uwanachama huo. Nchi zilizokuwa zinapata uhuru wake toka ukoloni zilitoa taarifa ambayo tarehe yake ya mwisho ilisadifia na tarehe ya kupandisha bendera mpya.

Hivyo nchi iliyojisajili UN na kupewa kiti, bila shaka ilipobadili nafasi iliyoiondosha uwananchi wake, haikuondoka katika umoja huo bila ya taarifa yoyote. Bila shaka patakuwepo maelezo na vielelezo vilivyokubalika kiti chake kurudishwa, bendera yake kushushwa katika mlingoti wa UN, na majukumu yake kame vile michango n.k., kufutwa.

Vipi leo nchi kama hiyo isiwe na hati halisi ya makubaliano ya muungano ambayo wananchi waliona Sheikh Karume na Mwalimu Nyerere wakisaini na kupeana April 26, 1964? Na vipi nchi isiwe hata na zile nakala halisi za vielelezo japo vile vilivyopelekwa UN kuhusu suala zito la utaifa wake? Au hata ushahidi wa kisheria kuwa hakuna nchi inayoitwa “Tanganyika” au yakuwapi maelezo/vielelezo kuhusu kuongezeka kwa mambo ya muungano na nani alotia saini kwa niaba ya Zanzibar? Ni saini yake au ni ya nani na kwa ushahidi gani wa kisheria?

Wenye kuumizwa na yote hayo khasa ni Wazanzibari na si Watanganyika. Mapinduzi ndo yalioipinduwa nusu ya jamii ya Zanzibar ilioshinda uchaguzi [wa Julai 1963]. Mapinduzi ndo yaloleta muungano na kuyapinduwa makubaliano ya mwanzo ya muungano. Mapinduzi ndo yaliokifuta kiti cha Zanzibar UN kwa nia ambazo Wazanzibari bado hawajazitambuwa.

Mapinduzi ndio yaliomuondowa Al Hajj Aboud Jumbe madarakani, na kilichomponza khasa Mzee Jumbe ni pale alipolianzisha Baraza la Misikiti Tanzania (BAMITA); yakamtia ndani Maalim Seif Sharif Hamad; na ndiyo yaliyopelekea Dk. Salmin Amour akataliwe kuiingiza Zanzibar/Tanzania katika OIC na kuiakhirishia Zanzibar kutojiunga na taasisi hiyo. Ndiyo yaliyoifanya Katiba ya nchi itamke kuwa Raisi wa Zanzibar siyo tena Makamo wa Kwanza wa Rais wa muungano, kama ilivotamkwa 1964. Na ndiyo yaliyo “thibitisha” kuwa nchi ya Zanzibar sasa ni Mkoa kama mkoa wowote Tanzania. Na kubwa zaidi, hayo ndiyo yaliyofanywa kuwaonesha rasmi Wazanzibari kuwa hata ndani ya chama kilichoundwa kwa kuunganisha ASP na TANU, TANU, CCM Bara, ndiyo itakayoamua nani atagombea Uraisi Zanzibar.

Hivi sasa hakuna udhibiti kwa watu kutoka bara kuingia na kuishi Zanzibar. Lengo ni kubadilisha “demographic situation in favor” [hali ya wingi wa watu] ya bara katika miaka michache ijayo. Na hiyo population [idadi ya watu] mpya inaandaliwa kuwa “superior” katika uchumi, ilimu na ushawishi wa kisiasa. Wapemba kuunga mkono chama kinachoongozwa na Maalim Seif Sharifu, Mpemba, university graduate [mhitimu wa Chuo Kikuu] na mzoefu katika serikali na siasa; mtu ambae alikhitalifiana na Mwalimu Nyerere inakaa vizuri katika “grand design” [mkakati mkubwa] ya Mwalimu ya kuwatenga Waunguja. Nyerere alipoenda Zanzibar kueleza kwa nini CCM iliwafukuza Seif na wenzake, alimtaja Seif kama watu “…tuliokuwa tukiwapokea katika chama pasipo kuwachunguza kwa undani ili kujua asili yao na huko watokako…” Mbali ya maneno hayo, Nyerere pia alianzisha propaganda za kwamba watu wenye rangi ya kuchovya kama ya Seif, japo si Waarabu, alitaka watazamwe kama Waarabu. Siasa zao zitakuwa za kutaka kumrudisha Mwarabu Zanzibar.

Nyerere pia alianzisha lugha ya kampeni ya “kuwanasihi” watu wa bara (Tanganyika), kama moja ya propaganda zake za kujenga hoja ya kujitetea pale itakapoonekana kuwa bara inatumia nguvu kulazimisha muungano. Ikawa akisema mara kwa mara kuwa “…hawa wanataka kuuvunja muungano, mkiwaachia, watauana ovyo…sasa wameshaanza kugawanyika na kubaguana, kati ya Wazanzibari na Wazanzibara…Wapemba na Waunguja…” Ingawa hoja hiyo inakusudiwa kuwaomba Watanganyika “kuwanusuru” Wazanzibari ili wasi-jeuana, haikumpitikia Mwalimu wala wengineo kuhoji; kama Wazanzibari wamegawika kiasi hicho, msimamo wa uhalali wa muungano ukoje hivi sasa? Tanganyika hivi sasa imeungana na nani; Wapemba, Waunguja, Wazanzibari au Wazanzibara? Siri ya mapinduzi ya wazee inatowa jawabu lililo safi; Tanganyika iliungana na Waafrika kutoka bara kuwapinduwa Wapemba na Waunguja—Wazanzibari.

Katika mambo ya kudhulumiana nchi, wajanja hufanya kila njia kuepuka masuala ya mfumo. Watakupelekeni kwenye utendaji kazi. Huko mtazungumza na wale waliopewa kazi ya ku “run” government [kuendesha serikali]. Hamtokutana tena na wale wanao “rule” [wanaotawala]. Sioni sahihi kuutegemea Muwafaka badala ya Mkataba wa Muungano na Katiba na sheria za nchi, kutupa muelekeo wa kule tunakostahili kwenda. Hivyo hivyo, siamini kuwa mtu atayewekwa na madhalim katika madaraka ya nchi, ana uwezo wa kujua na kuipeleka nchi hiyo pahali pasipokuwa pale panapo takiwa na madhalim hao.

Kwa vyoyote vile, endapo tutatanabahi, tukatambua kuwa nguvu za wananchi ni muhimu kuliko chochote, na kwamba nguvu hizo hazipatikani ila kwa kuwatoa katika umasikini wa kiza cha ujinga wa ilimu duni; tunakoelekea si kubaya. Kuwatowa wananchi kunako giza la tunakotoka na Zanzibar kujiwakilisha nchi za nje, kuujenga na kuulinda uchumi wake, pamoja na kulindwa na Wazanzibari, ni kuzuri, na huko ndiko kwa kuanzia.
 
Ni nchi Ila unaweza kukusanya watu wote kwa kupiga filimbi
 
Ni nchi Ila unaweza kukusanya watu wote kwa kupiga filimbi


The smallest countries by area​

We have marked with an asterisk (explanation at the end of the page) all those countries that are not independent and sovereign states. In this table it is clearly noticeable that a significant portion of the smallest "countries" are dependent on other states. A full 21 out of 30 countries are not independent states. After all, seven of them are in Europe, and eight are in the Caribbean. A full 21 are small island states.
RankCountryAreaPopulationPopulation per km²
1Vatican0.4 km²1,0002,272.73
2Monaco2.0 km²39,52019,564.36
3Gibraltar *6.8 km²33,6914,954.56
4Tokelau *12.2 km²1,647135.00
5Cocos Islands *14.2 km²59641.97
6Saint Barthelemy *21.0 km²7,103338.24
7Nauru21.1 km²10,873515.31
8Tuvalu26.0 km²11,925458.65
9Macao *30.4 km²658,39121,657.60
10Saint Martin *34.0 km²42,8461,260.18
11Norfolk Island *34.6 km²1,74850.52
12Pitcairn Islands *49.0 km²501.02
13Bermuda *53.2 km²63,8671,200.51
14St. Martin *53.2 km²39,239737.58
15San Marino61.2 km²34,010555.81
16British Indian Ocean Territory *63.2 km²3,50055.41
17Guernsey *78.0 km²67,491865.27
18Anguilla *96.0 km²18,741195.22
19Montserrat *102.0 km²5,41453.08
20Jersey *119.6 km²102,146854.06
21Christmas Island *135.0 km²2,20516.33
22Wallis and Futuna *142.0 km²15,891111.91
23British Virgin Islands *150.0 km²30,423202.82
24Liechtenstein160.5 km²38,254238.34
25Aruba *178.9 km²107,195599.16
26Marshall Islands181.4 km²59,618328.62
27American Samoa *199.0 km²55,103276.90
28Cook Islands241.7 km²8,12833.63
29Saint Pierre and Miquelon *242.0 km²5,25721.72
30Saint Kitts and Nevis260.0 km²53,546205.95
 
muungano wa union uliounda nchi moja ya JMT, lakini kitaifa, muungano wetu sio union, ni federation yenye nchi mbili, katiba mbili, marais wawili, mabunge mawili, Mahakama mbili, nyimbo mbili za taifa, bendera mbili, majeshi mawili, sarafu ndio moja. Tofauti pekee kati ya nchi hizi mbili ni moja ndio yenye sovereignty na nyingine haina.
P
HAKUNA mahakama mbili. Ndio maana UAMSHO walishtakiwa na kufungwa bara.

HAKUNA majeshi mawili ndo maana jeshi linaitwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania. Na ndo maana wanajeshi wa JWTZ wako kote Zanzibar na bara.

Na HAKUNA sarafu mbili, kama Mshana alivyotaka kutudanganya danganya hapa kama watoto.

WEWE PASKALI NA MSHANA of all the people msijue kwamba Zanzibar hawana hela yao na jeshi lao na mahakama ???? Au mnaleta mizaha mizaha na uongo wa makusudi ambao kizungu wanauita bull crap ????

Sasa umekuja na ki rubbish kipya eti nchi moja ndio yenye sovereignty. Nchi gani ndio ina sovereignty, Tanganyika au Zanzibar ?
 
Back
Top Bottom