Zanzibar ni nchi huru au ni sehemu ya Tanzania?

Zanzibar ni nchi huru au ni sehemu ya Tanzania?

Hiyo Katiba ianze kufuatwa na hao walioiandika . Chaguzi zote zinafanywa kwa kuzivunja katiba na kanuni Za uchaguzi. Tuanzie hapo kwanza
Kwa hiyo mnataka Rais wa Zanzibar asiye kibaraka awe wa namna gani atakayeivunja Katiba?.
 
Mimi siongei na watoto , maswali hayo kawaulize watoto wenzako
Kumbe huwezi kumruhusu mtu mwingine alale na mkeo vivyo hivyo serikali ya ccm haiwezi kumuweka mtu mwenye fikra na mtazamo kama wako lazima wamuweke mtu wao.
 
Kumbe huwezi kumruhusu mtu mwingine alale na mkeo vivyo hivyo serikali ya ccm haiwezi kumuweka mtu mwenye fikra na mtazamo kama wako lazima wamuweke mtu wao.
Sawaaa, saasaaaaa kalale
 
Sawaaa, saasaaaaa kalale
Kama una uwezo fanya wewe ambavyo unataka kiongozi wa Zanzinzibar asiyeburuzwa na ndiyo maana nimekwambia hivi hata angetawala Malaika Zanzinzibar lazima angetii Katiba maana Zanzinzibar ni sehemu ya muungano kinyume na hapo ukubali kupotezwa wewe jambo ambalo ni vigumu kulikubali.
 
Sawa vizuri kalale
 
Ndugu yangu angalia usije kufa kwa ugonjwa wa moyo, huu Muungano hakuna wa kuuvunja hayupo hajazaliwa na hatozaliwa wee umia vumilia mpaka mwisho wa dahari.
 
Zanzibar siyo nchi (Country), bali ni dola(State) inayounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu muungano uliwekwa kimkataba na hati idhini (Union Charter/Articles of the Union). Hivyo Zanzibar ilipunguza sehemu ya uhuru wake kujitawala (State Sovereignty) kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pili, suala la ajira lina pembe mbili. Kuna pembe ya Muungano na pembe ya Zanzibari. Watanganyika wapo Zanzibari na wanafanya kazi, lakini ni katika zile sehemu za mambo yanayohusu Muungano tu. Jambo kama hili liko hata kule Hong-Kong Uchina, na maisha yanaenda kama kawaida.

Tatu, suala la bendera siyo shida, maana bendera ni utambulisho tu (Emblem of Identity). Hata wewe ukiamua kuwa na bendera yako unaweza kuitengeneza na kuisajili kupitia HAKI-MILIKI (Intellectual Property). Nchini Marekani kila jimbo lina bendera yake na maisha yanaenda vizuri tu. Tena wanaenda mbali kabisa na kutumia bendera (The Confederate Flag) ya madola ya kusini (Dixie-Land) ambayo yaliasi muungano.

Nne, nadhani jina Raisi ni cheyo tu, hivyo unaweza leo ukamua kumuita Raisi wa Zanzibari wa Zanzibar Waziri Mkuu wa visiwani, Gavana,Sultani au Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Lakini muhimu kujiuliza ni hili: Je, madaraka yake ya Uraisi yanaishia wapi na ukimlinganisha na Raisi mwenzake ??? Utakuja kufahamu ni kwamba Uraisi wa Zanzibari hauvuki maji ya Pemba na Unguja, lakini Raisi wa Tanganyika madaraka yake yanavuka maji na kufika Pemba hadi Unguja, katika ngazi ya kitaifa hadi kichama.

Tano, mashirikisho mengi huwa na mihimili na taasisi zinazojitegemea kama mahakama, bunge na serikali zao. Wengine kama Ethiopia walienda mbali zaidi kuwa hata vikosi vyao binafsi vya ulinzi. Nchini Marekani kuna baadhi ya majimbo yana nguvu sana hadi kumuwezesha Gavana kutoa adhabu ya kifo. Hivyo hili la Zanzibar lisikutatize kabisa mkuu.

Sita, kuhusu uwakilishi wa Zanzibari kwenye siasa za kimataifa hilo ni jambo la kawaida sana maana sheria za kimataifa hazikatazi. Tokea mwaka 1945 hadi 1991 Umoja wa Kisovieti ulikuwa una viti vitatu kule Umoja wa Mataifa ambavyo ni vya USSR, Ukraine na Belarus ilhali wote wanatoka kwenye nchi moja iitwayo The Union of Soviets Socialist Republics (USSR). Hivyo hapa napo binafsi sioni tatizo kabisa.

Saba, kuhusu taasisi kujiendesha kwa utofauti hilo linatokana na uwepo wa madaraka ya ndani ya kujiendesha (Internal Sovereignty/Semi-Autonomy). Hata nchini Uchina, Hong-Kong inajiendesha kitofauti kabisa, nchini Marekani jimbo kama California ambalo huwa linajiendesha kitofauti kabisa na sera zake za kiliberi. Ambacho wengi kinatukera ni kwamba Tanganyika kutoweza kujiamulia mambo yake binafsi. Tunalitaka taifa letu.

Nane, hili la mikopo nakubaliana na wewe kabisa. Zanzibari haitakiwi ipate fungu lolote lile kwenye masuala yasiyo ya muungano (Non-Union Matters) ambayo yanaihusu Tanganyika. Mbaya zaidi hili la kukopa kupitia mngongo wa Tanganyika, ilhali sheria za kimataifa zinaruhusu Zanzibar iweze kukopa yenyewe binafsi. Katiba ya Ujerumani inaruhusu Ujerumani Mashariki na Ujerumani Magharibi kuingia katika mikataba binafsi ya kimataifa na nchi nyingine. Hivyo Ujerumani Mashariki inaruhusiwa hadi kukopa nje, ili mradi tu itoe taarifa kwa serikali ya Muungano.

Tunataka Zanzibar nao wakope kwa jina lao, maana inaruhusiwa kabisa. Huu ujanja wa kutaka kuiumiza Tanganyika, umenza kututia kinyaa watu wengi na kutukera sana. Hasahasa unapofanywa na Raisi Mzanzibari ambaye kiuhalisia hakutakuwa kabisa kugusa mambo ya Tanganyika.

Tisa, kuhusu ardhi. Wazanzibari ni watu wenye midomo sana na wanapenda kuongea siasa zao ambazo zimejaa ubaguzi wa rangi na dini. Lakini ukweli mchungu ni kwamba kuna mambo ambayo Tanganyika ikitutumua misuli, lazima wataumia sana. Mwaka 2014 ilifanyika tafiti na kufahamika kwamba kule Zanzibar (1 Square Kilometer inakaliwa na watu 200) wakati huku Tanganyika (1 Square Kilometer inaliwa na watu 20-30).

Tukisema tuanze kuwakazia, nadhani watu kama Raisi Hussein Mwinyi, Raisi Samia, Bakhresa na wapemba wengine ambao wako Dar es Salaam kisheria inabidi wamiliki ardhi kama wawekezaji kupitia kitu kiitwacho The Derivetive Right. Lakini jambo jingine kubwa utafiti wa mafuta ya Zanzibar ulifanywa kipindi cha Raisi Magufuli na kutambulika kwamba baadhi ya miamba yenye mafuta ambayo Zanzibari ingechimba imefika hadi Tanganyika, tena sehemu kubwa iko Tanganyika.

Kiukweli mimi natamani Tanganyika irudi, ikiwezekana kabisa tuvunje huu muungano.

Halafu nyie Moderators mliopo ONLINE (Boqin , Wand , BlackBold , YinYang , Active , Mhariri ) tafadhali tuheshimiane sana. Hili la mimi kuweka nukta .... ili kuwahi nafasi ya kuandika muda nitakaotaka mimi binafsi haliwahusu kabisa. Sasa kujifanya mko kichwani mwangu na kutabiri kwamba navuruga mijadala ni upigaji ramli na uchawi. Nimewavumilia sana kuna siku mkanipa BAN, leo mmefuta nilichoandika. Tafadhali sana heshimuni uhuru wangu na tusipangiane cha kuandika.
Mkuu sijui mm nilikuwa wapi sijaona bandiko lako huwa nikiona koment yako mahali popote Happ jf nafurahi mno na Kisha natulia kukufatiliza wew unasemaje au unamuelekeo gani hvyo nakuaminigi Sana chochote usemacho ,wee Ni member mmoja wapo nakukubali Sana Sana na sijui kwanin ??nitatatafuta siku moja nikione live live mnk navutiwa Sana na wew. Hapa ktk jamvi

Embu ona elimu uliyoshusha Happ jamvini kwa koment yako mmoja tu na nzito na kumfunika Hadi mleta mada

We w nadhani ccm ccm wakutumie vzr kwenye ishu hi ya muungano Kuna kitu ,vitu unavijuwa kwa uelewa mpana Sana

Happ awali nilidhani muungano ni muhimu kwetu cc kumbee unatunyonya cc watanganyika Ni kheri kubakia na jina bovu la tanganyika kuliko upuuzi huu wa Sasa HV

Ubarikiwe Sana mkuu kwa elimu ya bure uliyo nipa

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Anapatikana mtaa wa Tandamti na Congo Kariakoo location namba nitafute.
 
Wanzanzibar pamoja na uchache wao wanajitambua kuliko sisi Watangsnyika. Kwa kiasi kikubwa wametuonyesha njia ya kuboresha Muungano wetu kupitia Mabadiliko ya kumi ya Katiba ya Zanzibar yaliyofanyika mwaka 2010. Kwa sasa Katiba hiyo inatambua kuwa Zanzibar ni Nchi, Rais wa Wanzibar ana madaraka ya kugawa Mikoa na Wilaya, inatambua uwepo wa Mnzanzibar, nk.

Ibara ya 80 ya Katiba hiyo inazuia chombo chochote kujadili au kurekebisha sehemu ya kwanza ya sura ya kwanza ya Katiba hiyo, ambayo ndio iliyobeba niliyoyaandika hapo juu, hadi kufanyike kura ya maoni itakayowahusisha Wanzanzibar wote wenye haki ya kushiriki
 
Na sasa hivi wameanza kufukuzwa watanganyika taratiibu kwa kisingizio cha umalaya na omba omba
Kwani wewe hulioni SASA hivi nijambo la kawaida kukuta majiani mapaka Wenda wazimu toka Tanganyika wanazurura katika Mitaa na viunga vya miji ya Zanzibar mpka washangaa kabisa hao omba omba ndio USISEME hao Malaya ndio Mtihani wauza njugu balaa hivi Tanganyika hakuna sehemu za kuuza njugu? Au korosho mpaka mujazane kwetu??
 
Ndugu yangu angalia usije kufa kwa ugonjwa wa moyo, huu Muungano hakuna wa kuuvunja hayupo hajazaliwa na hatozaliwa wee umia vumilia mpaka mwisho wa dahari.
Hakuna aliyefikiria Karume kuondoka kiulaini au Magufuli na hata Baba yenu Nyerere aliyedai kuishi miaka mingi.
Ilivunjika Soviet union yenye Nuclear itakuwa Uvamizi huu uliobaki wa akina Makamba na genge lake ??
 
Ukinambia ni sehemu ya Tanzania nitakuuliza maswali yafuatayo:

1. Kwanini Watanganyika hawaruhusiwi kumiliki ardhi Zanzibar?

2. Kwanini ni ngumu ajira za Zanzibar kuhusisha Watanganyika?

3. Kwanini wana rais wao na bendera yao?

4. Kwanini wana taasisi zao zinazojitegemea kama mahakama, bunge, tume ya uchaguzi nk?

5. Kwanini timu za Zanzibar zinaiwakilisha Zanzibar kama nchi kwenye mashindano mbalimbali ya CAF kwa ngazi ya vilabu?

6. Kwanini taasisi zao zinaendeshwa tofauti kabisa na Tanzania, mfano kule watu wanatibiwa bure kwa hospitali za serikali, gharama za umeme ni nafuu sana nk?

Ukinambia Zanzibar ni nchi huru nitakuuliza maswali yafuatayo:

1. Kwanini haina amiri jeshi mkuu kwa maana ya kwamba haina jeshi linalojitegemea?

2. Kwanini Tanzania ikikopa Zanzibar wanapata fungu lao tena kwa uwiano usio sawa (Zanzibar inapata ratio kubwa) huku ikiwa mlipaji wa mkopo akiwa Tanzania bara pekee.

3. Kwanini haina sarafu yake yenyewe?

Mtazamo wangu: Muungano una mapungufu mengi.

Huwezi kuwa na Nchi ambayo kuna wakati inakuwa nchi kamili na kuna wakati inakuwa sehemu ya nchi nyingine.

Nadhani ni muda sahihi Zanzibar kuwa mkoa wa Tanzania, ama tuwaachie nchi yao wajitegemee.

Inavyoonekana ni kuwa Nyerere alitaka kuwalaghai Wazanzibari mwisho wa siku akajikuta anatengeneza muungano usioeleweka na sasa madhara yake yapo dhahiri.

Hoja ya usalama kwangu haina mashiko! Kama tumeweza kuilinda mipaka yetu yote dhidi ya nchi korofi zinazotuzunguka tutashindwaje kujilinda dhidi ya Zanzibar?
Kwenye ..kuwa mkoa.. naomba ushikirie hapo!
 
Back
Top Bottom