Anapatikana mtaa wa Tandamti na Congo Kariakoo location namba nitafute.
Januari 2000
Wazanzibari waambiwa:
Jihadharini na Pengo
WAZANZIBAR wametakiwa wachukue hadhari dhidi ya majaribio ya kutaka kuwaingiza katika balaa sambamba wakiitafakari kwa makini kauli ya Kardinali Pengo.
Aidha wametakiwa kuelewa historia ya kanisa Katoliki kuwa halijakuwa na rekodi nzuri hasa katika ukanda wa maziwa makuu pale linapojitumbukiza katika siasa.
Hayo yameelezwa na Wananchi kadhaa walioongea na gazeti hili mjini Zanzibar kufuatia kauli ya Kardinali huyo juu ya siasa za Zanzibar.
"Huko Rwanda Maaskofu wamelaumiwa kushiriki katika mauaji ya halaiki ya Wanyarwanda, huko Burundi pia wanalaumiwa, tunapowasikia leo wakizungumzia siasa zetu lazima tuhofu balaa zao, alisema bwana Hassan Mazrui.
Kama ni kuitakia mema Zanzibar, haiwezi kuwa nia ya askofu alisema bw. Mazrui
Alieleza kuwa chama tawala CCM kimejiwekea tabia ya kusimamia mabadiliko ambapo moja ya mabadiliko makubwa yaliyofanywa ni kuingilia makubaliano ya Muungano. Mabadiliko ambayo yalimuondoa Rais wa Zanzibar kuwa makamu wa Rais.
"Kanisa katoliki lilikuwa wapi kukemea mabadiliko hayo yaliyovunja makubaliano ya muungano", alihoji bwana huyo.
Aidha amesema Nyerere alikaa zaidi ya miaka 20 akibadili mambo apendavyo mara kofia mbili mtu mmoja mara kofia moja tena kofia mbili, "Mbona hakuna askofu aliyehoji na kumwambia kakaa sana. Hiyo Demokrasia wameijua lini? Alihoji
"Katika kikao kile wakatoliki hawakuwepo? Pengo leo anazungumza kwa niaba ya nani, Kanisa katoliki au yeye binafsi? Alihoji bw. Ameir.
"Kama anaona mabadiliko yataathiri Kanisa Katoliki basi Masheikh watatembea nyumba kwa nyumba kuyaunga mkono aliongeza na kama yatalinufaisha kanisa pia watafanya hivyo kuwaepusha Wazanzibar na balaa hilo, alisema bw. Ameir.
Mama mmoja Safia Shaame aliyedai ni mwana CCM alisema Pengo na kanisa lake hawezi kudai anawatakia mema Wazanzibar.
Alisema muungano 1964 ulikuwa wa Mambo11 Serikali za Tanganyika na Zanzibar zilibaki na wizara zao na mambo mengine ila 11 tu ndiyo wakakubaliana yawe ya Muungano.
Ina maana kama ni Wizara 11 ndio zingekuwa za Muungano. Lakini wizara zote na watumishi wote wa serikali ya Tanganyika wakapandishwa daraja na kuwa wa Serikali ya Muungano ya Tanzania.
Matokeo yake anasema Wizara ya Maendeleo ya Jamii wanawake na watoto Tanzania ni ya muungano wakati ya Zanzibar sio ya muungano na misaada ikija inaishia kwa Marry Nagu. Hali ni hiyo hiyo kwa Wizara za kilimo, Elimu na nyinginezo.
"Je Maaskofu hata wale waliomtangulia Pengo hilo hawakuliona"? Alihoji
Alisema kwa upande mwingine imekuwa ikidaiwa kuwa Mwalimu Nyerere alipigania kudumu kwa muungano amani na utulivu.
Hata hivyo akahoji mbona Mwalimu hakufika Zanzibar toka 1995. Alidai kuwa Mwalimu alikuwa hodari wa kuwasimanga Wazanzibar kwamba wanabaguana Waunguja na Wapemba.
" Kama aliwatakia mema mbona hakuwapatanisha bali akawafanya kama somo katika mikutano yake ya hadhara, alisema Bi Safia na kuongeza kuwa "kama ni umoja na amani Zanzibar italetwa na Wazanzibar wenyewe.
Aidha alisema haya yanayotokea sasa ni mipango ya makusudi iliyopangwa nje ya Zanzibar kupitia chama tawala ili kuwapambanisha wazanzibar.