Zanzibar ni nchi huru au ni sehemu ya Tanzania?

Hatuna tatizo lolote na Early Migrations, wenyeji asili wa Azania ni bantustans, lakini Nilotics wamehamia, Semi Nilotics, wamehamia, tuna Cushites, tuna Afroasiatic, ila kitendo cha watu kutoka Bara jingine kuhamia Africa, kulowea, kujifanya ndio kwao, wao ndio wao, kuwadharau wenyeji na hivi ndivyo wageni hawa walivyowafanya wenyeji
Kisha wenyeji wakafanya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, wakaungana na jirani zao, jee kuna mwenyeji yoyote atataka Muungano ufe?.
P
 

 

Very well said mkuu....nimekuelewa sana sanaaa
 
Na Zanzibar mstari ulichorwa na nani?
 
Zanzibar ina uwezo wa kusaini mikataba ya kimataifa: Kama makoloni yasiyo na Sovereign yaliweza kusaini mikataba ambayo iko mpaka leo, sembuse Zanzibar! Huwa napenda kuwaambia wanasheria wa Tanzania someni sana PUBLIC INTERNATIONAL LAW ili kuelewa haya mambo, CONSTITUTIONAL AND ADMINISTRATIVE LAW hazitoshi. Sasa umeandika mambo mengi, lakini ukweli ni kwamba Zanzibar ina uwezo wa kusaini mikataba ya kimataifa.

Mkuu hutaki unaacha,....
 
The Vatican is not The Holly See, nashukuru umekubali. Lakini pia wewe kubanwa na sheria za Vatican siyo jambo la ajabu kabisa. Mimi binafsi nabwanwa na sheria za Rotary Club International chombo ambacho siyo nchi wala dola. Lakini ili sheria za Rotary Club ziweze kunibana ni lazima kwanza ziruhusiwe na sheria za dola la Tanzania. Leo hii The JALA kama isingeruhusu Sheria za dini zitambulike, sidhani kama zingetambulika.

Pili, mkataba baina ya The Vatican City na Tanzania nao unachangia hayo kuwezekana. Dola la Tanzania likiamua leo lisitambue sheria za dini yako, linaweza fanya hivyo mara moja tu na zisitambulike. Huu ndiyo utaratibu ulivyo. Hutaki unaacha.

Kuhusu PERMANENT POPULATION: Narudia tena, kinachowaumiza wanasheria wa Tanzania ni kutokuwa na ufahamu wa PUBLIC INTERNATIONAL LAW. Tafasiri ya dola na vigezo vyake imetolewa na mikataba miwili mikubwa duniani. Mkataba wa kwanza Kabisa ni The Treaty of Westphalia 1648, mkataba wa pili ni The Monte-Video Conventio 1933 ambao unasema taifa lazima liwe na PERMANENT POPULATION. Mbona haya ni marahisi tu, na ulitakiwa uwe umeyasoma mwaka wa pili Chuo.

Sasa kuhusu SOMS, kuna kitu kinachoitwa THE SUI-GENERIS STATES ambacho kama walau ungekuwa ulisoma vizuri chuo mwaka wa pili ungekuwa unakifahamu vizuri na sidhani kama tungekuwa tunabishana hapa.
 
Nikitumia mantiki yako, on CIVILIZATIONAL TERMS kila taifa ni Artificial, maana hakuna jamii iliyowahi kuzaliwa na kuwa taifa tu. Mataifa yote hapo mwanzo yalianza kama Fiefdoms under Feudal Lords: Makabila machache yalitawaliwa na mtu mmoja mwenye ukwasi na ardhi. Dhana ya taifa la kisasa (The Modern State) imeanza kutumika mara ya kwanza karne ya 17.
 
Kisheria Zanzibar ina uwezo wa kujiunga na mashirika ya kimataifa na kuingia mikataba ya kimataifa. Hayo ya kukataliwa kujiunga na Organisatio of Islamic Cooperation (OIC) ni siasa uchwara za kitanzania ambazo mimi mtaalamu sitajihusisha nazo kabisa. Sasa niseme tu kitu rahisi ambacho kama utapenda kufuatilia, utafuatilia. Usipokubaliana na mimi, ACHA.

Union of Soviets Socialists Republics (USSR) iliundwa na nchi 15. Lakini mbali na taifa lile kuwa na kiti kwenye umoja wa mataifa kama taifa, nchi wanachama kama Ukraine na Belarus nao walikuwa na viti vyao vya kudumu kule Umoja wa Mataifa. Niende mbali zaidi, wewe Hong-Kong mbali na kuwa sehemu ya Uchina, ni mwanachama wa World Trade Organisation (WTO).

Hawana External Sovereignty lakini wameweza kusaini mkataba wa WTO na kuwa wanachama. Sembuse Zanzibar ??? Nchi kama Tanganyika ingekutana na watu wasomi wenye uelewa kama wenzetu wa huko Ulaya na Marekani, basi hizi porojo za OIC au Nyerere zisingekuwepo. Nyerere kukataa Zanzibar kujiunga na OIC hakuondoi ukweli kwamba Zanzibar inaweza kujiunga na OIC.
 
Rabda utufafanulie mwenyeji ni yupi?
kama jamii ina miaka 300 bado hajawa mwenyeji?
Kama wenyeji ni waafrika weusi basi ndio 80% ya wazanzibari kama sio zaidi,kuna hofu gani kuitisha kura ya maoni wakaamua hatma ya Nchi yao.

Je Jumbe alitaka serikali 3 ni muarabu wa Qatar 🇶🇦 ,Oman au Yemen 🇾🇪 ?

Tena cha ajabu huu ubaguzi unachochewa Zanzibar tu unapojadiliwa muungano ila bara kuna wahidi hata kiswahili ni chakubabaisha na wapo katikati kwenye siasa za nchi.
 
Kwa sababu hizo ulizotoa na mifano uliyotoa ukubali kuwa huu siyo muungano, ni vamizi. Nyerere alipinga Zanzibar kujiunga na OIC kwa kusema itaenda kinyume cha katiba ya JMT na nchi kutokuwa na dini (secular state). Tunashukuru kwa ulivyoonyesha wazi kuwa huo mnaouita muungano siyo muungano wa kawaida.
 

Inaonekana upo level ya uanafunzi wakati mimi nipo level ya kitaalam.

Siyo kweli kwamba Tanzania inazitambua Sheria za Vatican (Katoliki). Kwa sheria ipi?

Halafu ni hivi, matumizi ya jina 'Vatican' au 'Holy Sea' hutumika kumaanisha 'Mamlaka Kuu ya Kanisa Katoliki' kwa hiyo sidhani kama ni kitu cha kibishania, that's how it is.

JALA hairuhusu sheria za kidini, bali inaruhusu na kutambua matumizi ya sheria za kimila, miongoni mwa mengine.
 
Za ndani kabisa siku tukivunja muungano Zanzibar anachukua km 16 kutoka usawa wa bahari piga kutoka feri na kama ubungo
 
Hujaelewa bado maana ya taifa? Ngoja nirudie tena

A nation is a large group of people who inhabit a specific territory and are connected by history, culture, or another commonality.

Mataifa yapo mengi. WaIrish ni taifa, WaBritish ni taifa, WaJapan ni taifa, WaIran ni taifa n.k. Zanzibar ni taifa ukisoma vizuri hiyo maana ya taifa, ukijua historia ya Zanzibar utaona Zanzibar ni taifa. Tanganyika ilivyokuwepo haikuwa taifa. Ilikuwa ni nchi bandia.
 
Watu wa bara walivukaje bahari mpaka Zanzibar? Ukisema walikuwepo wakati visiwa vinamegeka siyo kweli. Modern human hakuwepo enzi hizo.
 
Miaka yote mmeshindwa kutatua kero kwa nini tuamini mnaweza? Miaka karibu 58 mmeshindwa kuondoa kero. Zanzibar umaskini umeongezeka, haki za binadamu zinaminywa, damu za Wazanzibari mnazimwaga kama damu za kuku. Mikopo mnapiga kelele. Mgao wa kipato cha taifa mnapiga kelele. Sasa mambo gani haya? Acheni tuu Zanzibar ipate uhuru tubaki tuu kama nchi jirani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…