Mkuu
Bepari2020, naomba nikurejeshe kwenye historia kwa kifupi
1. Naanza na Physical Geography da Formation ya Visiwa vyote vya bahari ya Hindi vilikuwa sehemu ya nchi kavu, vikamegeka, vikazungukwa na maji. Hivyo Zanzibar, Pemba Mafia ilikuwa ni sehemu ya Bara. Uthibitisho wa hoja hii ni mchoro huu
View attachment 2125554
2. Visiwa vya Zanzibar vilikuwa ni sehemu ya bara miaka milioni nyuma!, vikamegeka na eneo la kati likasombwa na mmomonyoko!,
3. Baada ya miaka mingi watu wa bara ndio wakaazi asili wa visiwa vya Zanzibar na Pemba, simulizi za kale za Fumo Liongo Karne 8 na Ibin Batuta karne ya 12 zilieleza. Kiongozi wao aliitwa Mwinyi Mkuu.
4. Karne ya 15, Mreno Vasco Da Gama alipopita ndipo akapeleka Ureno sifa ya visiwa vya Zanzibar na Pemba.
5. Karne ya 16, Ureno ikaivamia Zanzibar, ndipo mtawala wa asili wa Zanzibar, MwinyiMkuu kuwaomba Waarabu wa Oman wamsaidie kuwatimua Wareno.
6. Baada ya kazi ya kuwatimua Wareno kukamimika, Karne ya 17, hakuna anayekijua kilichomkuta Mwinyimkuu maana hakijaandikwa popote, ila mara ghafla mwaka 1734, Sultan Sayyed Said, akaihamisha Sultanet yake kutoka Oman na kuihamishia Zanzibar kwa
kuvivamia visiwa hivyo na kuvitwaa as if havina wenyewe, wakakulia, wakazaliana, wakalowea na sasa baadhi yao wameanza kujisahau kwa kudhania visiwa hivyo ni mali yao ilhali wao ni watu wa kuja tuu!.
7. Mkutano wa Berlin wa mwaka 1884, ukamtambua rasmi Sultan wa Zanzibar kama mtawala na mmiliki halali wa visiwa vya Zanzibar na akapewa a 10 miles za costal stip ya Bara ilikuwa chini ya himaya ya Sultan wa Zanzibar.
8. Tanganyika ilikuwa koloni la Ujerumani, Kenya ilikuwa Koloni la Uingereza, nchi hizi zote mbili hazikuwa na access ya bahari kwasababu a 10 miles ya costal stipe ya pwani yote ya Africa Mashariki ilikuwa chini ya himaya ya Sultan, ila Zanzibar ilikuwa chini ya uangalizi wa Uingereza, ndipo mwaka 1890, Waingereza na Wajerumani
wakaingia mkataba, wa Hellingoland, (The Zanzibar Treaty) Sultan wa Zanzibar aziachie zile 10 miles kwa matumizi ya German East Africa.
9. Tarehe 10 Desemba, 1963, Uingereza ikatoa uhuru wa bandia kwa Zanzibar kuendelea kuwa chini Sultan na serikali kibaraka wa Sultan.
10. Ndipo tarehe 12 January 1964 wanaume wakaingia kazini wakafanya yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya 1964, vilirudisha heshima ya visiwa hiyo iliyoporwa na madhalimu wale na muungano ukavirudisha visiwa hivyo kwa wenyewe halisi.
Mapinduzi Daima!
Muungano Udumishwe!
Mungu ibariki Tanzania.
P.