Zanzibar ni nchi huru au ni sehemu ya Tanzania?

Zanzibar ni nchi huru au ni sehemu ya Tanzania?

Tanganyika ina
Zanzibar haichangii hata ndururu kwenye Muungano.
P

1.Tanganyika inachangia kiasi gani ?
Nielimishe kwa ushahidi
2.nini maana ya neno TanZania?
3. TRA ni nini?
4.Tanganyika bado ipo?
Naomba kujuzwa
 
Usiwadanganye eti wakitaka watoke!. It's very unfortunately zile artcles of Union sio contract ni aggreement, tumeungana for life, hakuna kipengele cha kuvunja Muungano, hivyo huu muungano wetu adhimu, tutaulinda kwa gharama yoyote!.
P
Sio sahihi
Bunge likipata 2/3 ya bara na Zanzibar muungano unavunjika Tizama vizuri katiba ya sasa.
Hata kura ya maoni ya wazanzibar inaweza vunja muungano tizama katiba ya Zanzibar.
46819BA3-9ADA-4779-959B-F165FEDE05B5.jpg

Kama mtaulinda kwa gharama yoyote hata kwa kumwaga damu huo si Muungano ni ukoloni are u proud to be colonial power ?mnapenda historia iwaandike hivyo nyinyi waafika kuwa mlitawala kimabavu nchi nyengine ya kiafrika.
 
Kwenye Muungano wetu, kuna mmoja ni the majority, Tanganyika, ana eneo kubwa, na mwingine ni minority, Zanzibar ana eneo kiduchu, hivyo ardhi ya JMT ndio ardhi ya wote, lakini ardhi ya Zanzibar sio ardhi ya Muungano, ni kwa ajili ya Wazanzibari only. Ingekuwa free wabara kumiliki ardhi Zanzibar, visiwa vile vingezama!.
P

Wasiwasi wako tu wala visingezama. Ingesaidia zaidi kuunganisha na kuwa na Muungano wa kweli.

Nothern Ireland ina watu1.8M, Wales 3M, Scotland 5M, England 55M.

Muungano wao unaendelee na hizi nchi zenye ardhi ndogo wala hazilalamiki kuhusu ardhi. Infact they encourage people to move to these countries.

Hawana ubaguzi kwenye ajira, elimu, dini zingine, ndoa etc.
 
Umeona ulivyo unazungumza vitu kwa kukaririshwa: The Vatican City na The Holly See ni viti viwili tofauti. Tena ukizungumza hivi mbele ya watu wasomi utadharaurika sana. The Vatican City na The Holy See ni kitu kimoja tokea lini ???

Haya sikiliza sasa: The Vatican ni nchi na dola ambayo ni makao makuu ya kanisa takatifu la mitume la Katoliki, huku The Holly See ni serikali inayoongoza kanisa takatifu la mitume la kikatoliki. The Vatican City na The Holly See kisheria tunasema vyote ni watu (The both have legal personality).

Sasa iko hivi, kabla ya kuzaliwa The Vatican City mwaka 1929 kupitia The Lateran Pacts, The Holly See ilikuwepo na ndiyo imeendesha kanisa la Katoliki tangu kuanguka kwa dola la kipapa kipindi cha Mfalme Napoleon Bonaparte mwaka 1809. Vatican kama nchi na dola imezaliwa mwaka 1929.

The Vatican IS NOT The Holly See, let this sink within depths of your cranium. Nakushauri mkuu, uandike hoja baada ya kufanya tafiti za kina.

Umejichanganya sana. Wewe siyo raia wa Vatican wewe ni raia wa Tanzania, ambaye yuko chini ya sheria za nchi ya Tanzania: Sheria za Vatican ambazo zinakuongoza wewe ni zile kidini (Canon and Ecclesiastical Laws), tena kwenye mambo machache kama ndoa, talaka na ubatizo wa watoto. Ukienda Vatican ndiyo utabanwa na sheria za huko.

Sasa hivyo vigezo vya dola ambavyo umeniwekea hapa, navyo umevichanganya sana. Vimetolewa na mkataba wa monte-video (The Monte-Video Convention of 1933) ambao ulitoa vigezo vya taifa au dola ambavyo ni: Permanent Population, Government, Defined Territory and Sovereignty.

Sasa The Vatican haina idadi ya watu ya kudumu (Permanent Population) watu wa pale huja na kuondoka baada ya kumaliza utumishi wao na kurudi nchini kwao. Ndiyo maana nakwambia hivi, kukosekana kwa kigezo kimoja haimaanishi kwamba dola siyo huru.

Kama kigezo ni SOVEREIGNTY, kuna nchi kama The Sovereign Military Order of Malta (SMOM) ambayo haina Sovereignty lakini bado inatambulika kama nchi na ina ushawishi mkubwa sana kimataifa. Haya mambo inabidi yafanyiwe tafiti sana kabla ya kukimbilia kuwasikiliza wanasiasa kama Tundu Lissu.

Sheria za Vatican ambazo zinakuongoza wewe ni zile kidini (Canon and Ecclesiastical Laws), tena kwenye mambo machache kama ndoa, talaka na ubatizo wa watoto. Ukienda Vatican ndiyo utabanwa na sheria za huko.
.,....................

Hapa umekubaliana na mimi kwamba sheria za Vatican zinaniongoza.

Sasa hivyo vigezo vya dola ambavyo umeniwekea hapa, navyo umevichanganya sana. Vimetolewa na mkataba wa monte-video (The Monte-Video Convention of 1933) ambao ulitoa vigezo vya taifa au dola ambavyo ni: Permanent Population, Government, Defined Territory and Sovereignty.
..,...........
Sijajua hapa unapinga nini zaidi naona umetoa reference ya nilichosema

Sasa The Vatican haina idadi ya watu ya kudumu (Permanent Population) watu wa pale huja na kuondoka baada ya kumaliza utumishi wao na kurudi nchini kwao. Ndiyo maana nakwambia hivi, kukosekana kwa kigezo kimoja haimaanishi kwamba dola siyo huru.

.,.....,.....

Rejea case ya Machano na Wenzake iliyoamuliwa na Mahakama ya Rufaa. Vigezo vyote vinne ni sharti vitimie. Na Zanzibar ilikosa kimoja, sovereignty, na hivyo kuamuliwa siyo dola na hivyo basi Serikali ya Zanzibar haiwezi kufanyiwa uhaini.

Holly Chair/Vatican ina watu. Hakuna sheria inasema watu wawe permanent. Ni hivi, popote alipo Mkatoliki basi utawala wa Pope upo. Yaani, utawala wa Papa hauna territory maalum. Na hiyo ni exception kwenye general rule ya defined territory.

Kama kigezo ni SOVEREIGNTY, kuna nchi kama The Sovereign Military Order of Malta (SMOM) ambayo haina Sovereignty lakini bado inatambulika kama nchi na ina ushawishi mkubwa sana kimataifa.

..........😀

Sasa unasemaje Malta haina sovereignty huku unasema inatambulika kama huru?

Kutambulika kama huru ndiyo sovereignty yenyeweee
 
Ongea yote lakini Karume aliingizwa mkenge na Nyerere mtoto wa mjini akagawa nchi kupitia Hati Idhini ya Muungano (Articles of the Union). Zanzibar siyo nchi bali dola, nchi Tanzania. Hutaki unaacha, lakini ukweli ndiyo huo. Nchi kama Scotland na Ireland zilivamiwa na Uingereza na mpaka leo hii, zimebakia kuwa madola yanayounda Umoja wa Nchi za Kifalme (The United Kingdom), sembuse Zanzibar ??

Hata Waskoti na Waairishi wakienda duniani hujitambulisha kama Waskoti na Waairishi, lakini ukweli mchungu ni kwamba nchi ni Umoja wa Nchi za Kifalme (The United Kingdom). Wako na tamaduni zao za kuvaa magauni, lakini ukweli ni kwamba Scotland na Northern Ireland siyo nchi bali ni madola yanayounda The United Kingdom. Huu ndiyo ukweli, kama hutaki unaacha.

Halafu unavyozungumzia Tanganyika, yenye wabantu asilimia 80% ambao wamefanana kivinasaba, kilugha na kitamaduni kama Artificial State ukidhani ni hoja ya msingi, napata shida sana na uelewa wako. Duniani mataifa Artificial yako mangapi lakini bado maisha yanaenda ??? Marekani ni Artificial State, lakini sidhani kama kuna kitu ambacho ninyi Wazanzibari mmewapita, kama kipo niambie hapa.

Kuhusu Zanzibari kujitoa kwenye Muungano: Binafsi nasema hata leo usiku wakitaka watoke tu. Mbali na Zanzibar kuwa A Maritime-Security Buffer Zone (A Mere Appendage) to Tanganyika's Territory, sioni umuhimu mwingine. Kama upo nitajie. Ilivyokuwa Zanzibar kwa Tanganyika kipindi chote cha vita baridi, ni sawa na ilivyokuwa Poland kwa Urusi kipindi chote cha vita baridi: A Mere Appendage.
Northern Ireland imechanganyika, kuna wenye asili ya Britain na kuna wenye asili ya Ireland. Northern Ireland siyo taifa hilo. Taifa ni Ireland na taifa ni Britain. Scotland ni taifa na sitoshangaa kama ikipata uhuru siku zijazo. Walipiga kura ya maoni 2014 matokeo yakawa 55.3% walipinga, 44.7% walitaka.

Tanzania hata kuuzungumzia huo mnaouita muungano unaonekana kama adui sembuse kupiga kura ya maoni kuuliza je bado pande zote mbili wanautaka? Usilinganishe muungano wa UK na hili vamizi la Zanzibar alilofanya Nyerere.

Tanganyika ni artificial state huwezi kupinga. Kwa mfano Mmasai wa Tanzania na Mmasai wa Kenya ni watu wale wale ila Uingereza ilichora mstari kwenye ramani ikawatenganisha. Huwezi kusema Mmasai wa Kenya na Mmasai wa Tanzania wana tofauti lakini Mmasai wa Tanzania na Msukuma wana utamaduni mmoja.

Artificial states huwa ni rahisi kusambaratika. Angalia nchi kama Syria, angalia Iraq, hata Marekani ilikuwa karibu kusambaratika, walishapigana vita ya wenyewe kwa wenyewe wakauwana watu zaidi ya milioni 1

Wewe binafsi uko tayari Zanzibar ijitoe kwenye huo unaouita muungano lakini CCM haikubali na wapo tayari kuulinda kwa gharama yoyote. Wako tayari kumwaga damu, kufunga watu, kufilisika ili kuulinda huo unaouita muungano. Sera hiyo haiwezi kuendelea siku zote.
 
Wewe ni muongo tena. Muongo mkubwa. Zanzibar iwe na history halafu Tanganyika ikose history ?! Mbona umeikuza mno zanzibar na kuidunisha Tanganyika. Kwa lipi hasa ?!.

Muungano hata mimi siukubali achilia mbali kuupenda. Lakini si kwa kuidunisha Tanganyika. Zanzibar haina kitu Tanganyika ikikaa pembeni. Zaidi zaidi kutegemea misaada .
Historia ya Tanganyika ni kuanza kuwa koloni la Uingereza 1922, kupata uhuru 1961, na kuuliwa na mwaka 1964. Nje ya hapo hakuna Tanganyika wala haina historia. Ni sehemu tuu Mwingereza alichora mstari kwenye ramani akapaita Tanganyika. Siyo taifa hilo.
 
Zanzibar kwanza ni taifa, a nation (a large group of people who inhabit a specific territory and are connected by history, culture, or another commonality). Wanzanzibari wana historia, wana utamaduni. Wazanzibari popote walipo duniani wanajitambua kama Wazanzibari na wanatambulika kama Wazanzibari.
,.........................

Unàfahamu tofauti ya 'taifa', 'nchi' na 'dola'?
...............

Asili ya Wazanzibari haipotei. Zanzibar ilivamiwa na Nyerere na jeshi lake ikapoteza uhuru.
..................
Nyerere 'alivamia' Taifa la Zanzibar au Nchi ya Zanzibar?

Siyo kupungua, ilipoteza kabisa. Lakini kutokana kuwa Zanzibar ni taifa, lazima kuna siku uhuru utarudi.
......................

Taifa ni watu, kwani Wazanzibari hawapo huru? Unachanganya kati ya nation, state, na country

Tanganyika haikuwa taifa, ilikuwa ni mkusanyiko wa makabila uliowekwa pamoja na serikali ya Uingereza wakaita Tanganyika. Tanganyika ilikuwa haina historia, haina utamaduni wake. Ni nchi bandia (artificial country).
................

Unaona. Umeanza kusema Tanganyika ilikuwa Taifa, halafu ukasema tena Tanganyika ilikuwa nchi ......Kuna tofauti. Unachanganya.

Nyerere alilijua hili na ndiyo maana kwake ilikuwa rahisi kuiua Tanganyika, kuvamia Zanzibar na kuunda nchi mpya aliyoita Tanzania ambayo nayo ni batili (artificial country).
...................
Haya

Nchi ya kweli ambayo ilipoteza uhuru wake ni Zanzibar pekee kwa sababu Zanzibar ni taifa kwanza.
..........'

Nimesema Zanzibar ni taifa. Zanzibar is a nation. Sijachanganya chochote na maana ya taifa/nation nimeshaiweka. Zanzibar ilipovamiwa na Nyerere ilipoteza sovereignity, ilipoteza uhuru ila haijapoteza utaifa.

Tanganyika huwezi kuita taifa. Haikuwa na hadhi hiyo ukifuata maana ya utaifa. Ilikuwa ni nchi bandia (artificial state) iliyoundwa na Uingereza na ikavunjwa au kuuliwa na Nyerere. Huwezi kulinganisha Zanzibar na Tanganyika hata siku moja.
 
Niende mbali zaidi na kusema kwamba, Zanzibar ina External Sovereignty kwasababu ina uwezo wa kuingia makubaliano ya kimataifa (Treaties, Pacts, Covenants and Concessions) peke yake bila kuingiliwa au kuathiriwa na Serikali ya Muungano na Tanganyika. Hapa utasemaje Zanzibar haina Sovereignty wewe ???
Hii siyo kweli. Zanzibar haiwezi kwenda kinyume na katiba ya JMT. Mfano mzuri ni Nyerere kupinga Zanzibar kujiunga na
Organisation of Islamic Cooperation (OIC). Haya ni makubaliano ya kimataifa ambayo Wazanzibari walitegemea yatasaidia kuinua uchumi. Sasa sovereignity gani hiyo?
 
Tanzania hata kuuzungumzia huo mnaouita muungano unaonekana kama adui sembuse kupiga kura ya maoni kuuliza je bado pande zote mbili wanautaka? Usilinganishe muungano wa UK na hili vamizi la Zanzibar alilofanya Nyerere.

Wewe binafsi uko tayari Zanzibar ijitoe kwenye huo unaouita muungano lakini CCM haikubali na wapo tayari kuulinda kwa gharama yoyote. Wako tayari kumwaga damu, kufunga watu, kufilisika ili kuulinda huo unaouita muungano. Sera hiyo haiwezi kuendelea siku zote.
Mkuu Bepari2020, kwenye mijadala ya kuhusu maslahi ya Taifa kama hoja hii, ni vema tuwe wakweli toka ndani ya nafsi zetu kwa kwanza kuukubali ukweli uliopo hata kama hatukubaliani nao .
Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar uliounda Tanzania, ni kitu ambacho kipo na kina exist, hivyo huwezi kuita "huo mnaouita Muungano" as if ni kitu ambacho hakipo ila kinaitwa tuu!. Hakuna huo mnaouita Muungano, hatuuiti Muungano, bali Muungano upo una exist.

Pili waasisi wa Muungano, Nyerere na Karume, waheshimiwe, usianze kumyooshea kidole mmoja na kumuita kwa majina mabaya kama "hili vamizi la Zanzibar alilofanya Nyerere".

Muungano wetu adhimu sio vamizi!. The Initiator wa Muungano ni Karume ndio alikuja bara kumuomba Nyerere ulinzi wa kuyalinda Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, dhidi ya manowari za Uingereza zilizokuwa zimetia nanga Mombasa tayari kwa kuja kuivamia Zanzibar, kuigomboa na kumrejesha Sultan aliyepinduliwa.

Ndipo Nyerere akapendekeza tuungane, Karume akakubali pale pale "tuungane, wewe rais, mimi Makamo". Usimtwishe Nyerere uzushi wa uvamizi!. Zile story za Kipumbwi ni hadithi tuu za uongo na ukweli.

Tuujadili Muungano in good faith kuwa una kero ambazo zimeendelea kutatuliwa na mwisho wa siku kero zote zitaondoshwa, tutakuwa na Muungano shwari bila kero ila pia kama ilivyo kwenye penzi, mahasidi hawakosekani hivyo tunaiendeleza nadhiri zote mbili, kwa Zanzibar "Naapa na naahidi, Mbele ya Mungu, Mapinduzi nitakulinda mpaka kifo". Na kwa JMT, "Muungano tutaulinda kwa gharama yoyote".
P
 
Nimesema Zanzibar ni taifa. Zanzibar is a nation. Sijachanganya chochote na maana ya taifa/nation nimeshaiweka. Zanzibar ilipovamiwa na Nyerere ilipoteza sovereignity, ilipoteza uhuru ila haijapoteza utaifa.

Tanganyika huwezi kuita taifa. Haikuwa na hadhi hiyo ukifuata maana ya utaifa. Ilikuwa ni nchi bandia (artificial state) iliyoundwa na Uingereza na ikavunjwa au kuuliwa na Nyerere. Huwezi kulinganisha Zanzibar na Tanganyika hata siku moja.
Kwani kilichoungana na Tanganyika ni 'dola la Zanzibar', 'nchi ya Zanzibar' , 'serikali ya Zanzibar' au 'taifa la Zanzibar'?
 
Hoja ya kutokuwa na kiti UN au kutotambulika ni hoja mufilisi kabisa na zimekaa kisiasa.
Vigezo vikuu vya dola ni hivi ambavyo Zanzibar imekidhi:
1. Government
2. Population
3. Territory
4. Sovereignty (Both Internal and External Sovereignty)

Ambacho Advocate Tundu Lissu amewapotosha watanzania wengi ni lile la kusema kwamba Zanzibar haina External Sovereignty. Hili siyo kweli, Zanzibar ina External Sovereignty kwasababu imewahi kuwa nchi huru hapo awali, lakini External Sovereignty yake inaendeshwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano ambayo Zanzibar ni nchi mshirika.

Niende mbali zaidi na kusema kwamba, Zanzibar ina External Sovereignty kwasababu ina uwezo wa kuingia makubaliano ya kimataifa (Treaties, Pacts, Covenants and Concessions) peke yake bila kuingiliwa au kuathiriwa na Serikali ya Muungano na Tanganyika. Hapa utasemaje Zanzibar haina Sovereignty wewe ???
😀 Nimeshangazwa na aya👆 yako ya mwisho.

Naona unaandika unachotaka kusikia na siyo kilichopo.

Katika Muunguno, Jamhuri ya Muunguno wa Tanzania ndiyo the only sovereign State (dola huru) linalosaini mikataba ya Kimataifa.

Zanzibar siyo sovereign State since 1964. Haina sovereignty.

NB:Ninasisitiza google na usome Kesi ya Mahakama ya Rufaa ya Tanzania baina ya Machano Hamis and Others v. Republic, ambapo Wahe. Majaji walifanya utafiti wa kina kirefu, na kuelezea kwa undani kuhusu dhana nzima ya uraia, dola huru na uhaini.

Hivi vitu vipo kisheria, na ukitoa hoja bila rejea ya sheria na principles ni kosa. You're actually not with me(us).
 
1.Tanganyika inachangia kiasi gani ?
Nielimishe kwa ushahidi
2.nini maana ya neno TanZania?
3. TRA ni nini?
4.Tanganyika bado ipo?
Naomba kujuzwa
Bandiko lililotangulia nimesisitiza hili jambo tulijadili kwa kuwa wakweli na kutanguliza mbele maslahi ya Taifa.
1. Kwanza Tanganyika haipo, kilichopo ni Tanzania Bara na Tanzania Visiwani. Mpaka sasa gharama zote za kuendesha Muungano zinagharimiwa na upande mmoja tuu wa Muungano, na hii ni kero inayoendelea kushughulikiwa, Tume ya pamoja ya fedha imeishaundwa, kinachoendelea ni Establishment ya gharama za Muungano, zikiisha patikana , Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar zinachangia kwa uwiano ule ule, wa 95.5%/4.5%.
maswali No. 2, 3 siyajibu. Swali la 4, nimeisha lijibu.
P
 
Historia ya Tanganyika ni kuanza kuwa koloni la Uingereza 1922, kupata uhuru 1961, na kuuliwa na mwaka 1964. Nje ya hapo hakuna Tanganyika wala haina historia. Ni sehemu tuu Mwingereza alichora mstari kwenye ramani akapaita Tanganyika. Siyo taifa hilo.
Kwani Zanzibar inayo history ipi zaidi ya ukoloni huo wa mwarabu ? Mataifa yetu haya ya Africa kwa sehemu kubwa , waliishi jamii za watu waliokuepo kipindi hicho wakizungumza lugha zao na tamaduni zao, Zanzibarikiwemo .

Ramani zao, na serikali zao zimechorwa na wakoloni. Zanzibar ni visiwa pembezoni mwa Tanganyika huwezi kwepa hilo. Kikubwa mna haki ya kujiendeshea mambo yenu kama ilivyo Comoros, Seashells, Madagascar nk. Hili la muungano wa kinyonyaji hapana. Tanganyika iacheni na uwema wake wa kimshumaa
 
Nimesema Zanzibar ni taifa. Zanzibar is a nation. Sijachanganya chochote na maana ya taifa/nation nimeshaiweka. Zanzibar ilipovamiwa na Nyerere ilipoteza sovereignity, ilipoteza uhuru ila haijapoteza utaifa.

Tanganyika huwezi kuita taifa. Haikuwa na hadhi hiyo ukifuata maana ya utaifa. Ilikuwa ni nchi bandia (artificial state) iliyoundwa na Uingereza na ikavunjwa au kuuliwa na Nyerere. Huwezi kulinganisha Zanzibar na Tanganyika hata siku moja.
Unajikweza mno na Zanzibar yako. Ambayo hata asili ya jina lake ni wakoloni wenu wa ki Arabs . Huu utaifa unayoipa zanzibar kuinyima Tanganyika umeitoa wapi ?!. Bila Tanganyika, Zanzibar is nothing. Bahati mbaya kwa Tanganyika na nzuri Zanzibar ni kukuta viongozi wa Tanganyika wasiojielewa . Wenye mapenzi na jina Tanzania kuliko nchi yao
 
Zanzibar kwanza ni taifa, a nation (a large group of people who inhabit a specific territory and are connected by history, culture, or another commonality). Wanzanzibari wana historia, wana utamaduni. Wazanzibari popote walipo duniani wanajitambua kama Wazanzibari na wanatambulika kama Wazanzibari. Asili ya Wazanzibari haipotei. Zanzibar ilivamiwa na Nyerere na jeshi lake ikapoteza uhuru. Siyo kupungua, ilipoteza kabisa. Lakini kutokana kuwa Zanzibar ni taifa, lazima kuna siku uhuru utarudi.

Tanganyika haikuwa taifa, ilikuwa ni mkusanyiko wa makabila uliowekwa pamoja na serikali ya Uingereza wakaita Tanganyika. Tanganyika ilikuwa haina historia, haina utamaduni wake. Ni nchi bandia (artificial country). Nyerere alilijua hili na ndiyo maana kwake ilikuwa rahisi kuiua Tanganyika, kuvamia Zanzibar na kuunda nchi mpya aliyoita Tanzania ambayo nayo ni batili (artificial country). Nchi ya kweli ambayo ilipoteza uhuru wake ni Zanzibar pekee kwa sababu Zanzibar ni taifa kwanza.
Mkuu Bepari2020, naomba nikurejeshe kwenye historia kwa kifupi
1. Naanza na Physical Geography da Formation ya Visiwa vyote vya bahari ya Hindi vilikuwa sehemu ya nchi kavu, vikamegeka, vikazungukwa na maji. Hivyo Zanzibar, Pemba Mafia ilikuwa ni sehemu ya Bara. Uthibitisho wa hoja hii ni mchoro huu
main-qimg-5cbc19ebebd337281fd47d1270670a81-c.jpg

2. Visiwa vya Zanzibar vilikuwa ni sehemu ya bara miaka milioni nyuma!, vikamegeka na eneo la kati likasombwa na mmomonyoko!,
3. Baada ya miaka mingi watu wa bara ndio wakaazi asili wa visiwa vya Zanzibar na Pemba, simulizi za kale za Fumo Liongo Karne 8 na Ibin Batuta karne ya 12 zilieleza. Kiongozi wao aliitwa Mwinyi Mkuu.
4. Karne ya 15, Mreno Vasco Da Gama alipopita ndipo akapeleka Ureno sifa ya visiwa vya Zanzibar na Pemba.
5. Karne ya 16, Ureno ikaivamia Zanzibar, ndipo mtawala wa asili wa Zanzibar, MwinyiMkuu kuwaomba Waarabu wa Oman wamsaidie kuwatimua Wareno.
6. Baada ya kazi ya kuwatimua Wareno kukamimika, Karne ya 17, hakuna anayekijua kilichomkuta Mwinyimkuu maana hakijaandikwa popote, ila mara ghafla mwaka 1734, Sultan Sayyed Said, akaihamisha Sultanet yake kutoka Oman na kuihamishia Zanzibar kwa
kuvivamia visiwa hivyo na kuvitwaa as if havina wenyewe, wakakulia, wakazaliana, wakalowea na sasa baadhi yao wameanza kujisahau kwa kudhania visiwa hivyo ni mali yao ilhali wao ni watu wa kuja tuu!.
7. Mkutano wa Berlin wa mwaka 1884, ukamtambua rasmi Sultan wa Zanzibar kama mtawala na mmiliki halali wa visiwa vya Zanzibar na akapewa a 10 miles za costal stip ya Bara ilikuwa chini ya himaya ya Sultan wa Zanzibar.
8. Tanganyika ilikuwa koloni la Ujerumani, Kenya ilikuwa Koloni la Uingereza, nchi hizi zote mbili hazikuwa na access ya bahari kwasababu a 10 miles ya costal stipe ya pwani yote ya Africa Mashariki ilikuwa chini ya himaya ya Sultan, ila Zanzibar ilikuwa chini ya uangalizi wa Uingereza, ndipo mwaka 1890, Waingereza na Wajerumani
wakaingia mkataba, wa Hellingoland, (The Zanzibar Treaty) Sultan wa Zanzibar aziachie zile 10 miles kwa matumizi ya German East Africa.
9. Tarehe 10 Desemba, 1963, Uingereza ikatoa uhuru wa bandia kwa Zanzibar kuendelea kuwa chini Sultan na serikali kibaraka wa Sultan.
10. Ndipo tarehe 12 January 1964 wanaume wakaingia kazini wakafanya yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya 1964, vilirudisha heshima ya visiwa hiyo iliyoporwa na madhalimu wale na muungano ukavirudisha visiwa hivyo kwa wenyewe halisi.

Mapinduzi Daima!
Muungano Udumishwe!
Mungu ibariki Tanzania.

P.
 
Mkuu Bepari2020, naomba nikurejeshe kwenye historia kwa kifupi
1. Naanza na Physical Geography da Formation ya Visiwa vyote vya bahari ya Hindi vilikuwa sehemu ya nchi kavu, vikamegeka, vikazungukwa na maji. Hivyo Zanzibar, Pemba Mafia ilikuwa ni sehemu ya Bara. Uthibitisho wa hoja hii ni mchoro huu View attachment 2125554

Watu waliofika Zanzibar 1734 kwa maneno yako Unawaita watu wa kuja tu Yaani ilipofika 1964 waliokua na miaka 230.
.tukiaza hivyo hata wewe usikute ni Mrundi au Mnubi wa central Africa
Kwa taarifa tu sultan Jamshid mama yake ni Mmanyema.
Alie kuwa waziri mkuu aliepinduliwa ni Mpemba wa asili.
Mgeni ni Okello alizaliwa kukulia Uganda 🇺🇬 na kuja zanzibar kuuwa wenyeji na kurudi kwao.
 
Back
Top Bottom