Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Mkuu MALCOM LUMUMBA , kwanza asante for this.Hoja ya kutokuwa na kiti UN au kutotambulika ni hoja mufilisi kabisa na zimekaa kisiasa.
Vigezo vikuu vya dola ni hivi ambavyo Zanzibar imekidhi:
1. Government
2. Population
3. Territory
4. Sovereignty (Both Internal and External Sovereignty)
Sifa za nchi ni hizi
1. People- Watu wanaotambulika Kimataifa. Japo Zanzibar inao watu waitwao Wazanzibari, watu hawa hawatambuliki Kimataifa, Kimataifa hakuna mtu anayeitwa Mzanzibari, aliyepo ni Mtanzania tuu, Wazanzibari hawana passport hivyo hawana utambulisho wa Kimataifa.
2. Land. A defined area with international recognized boundaries. Zanzibar ina land, teritory, lakini haina international boundaries. Mipaka ya Kimataifa ni ya Tanzania tuu.
3. Government. A institution that works on creating and enforcing laws using state organs. Zanzibar ins serikali yake, SMZ, lakini haina vyombo vya dola, Jeshi, polisi, na Usalama, hivyo Zanzibar ni nchi kwa maana ya eneo lakini sio dola kwasababu haina vyombo vya dola!. Vyombo vya dola viko chini ya Amir Jeshi Mkuu ambaye ni mmoja tuu, rais wa JMT. Katiba ya JMT inaitambua Tanzania kama ni nchi moja ya JMT na Zanzibar ni sehemu ya JMT. Lakini katika kujifariji kwa kujidanganya, marekebisho ya katiba ya Zanzibar ya 2010 yaliyoanzisha GNU, yakaitambulisha Zanzibar kama ni nchi, ni moja ya nchi mbili zinazounda JMT. Ikaitaja mipaka ya nchi ya Zanzibar. Ikamtaja rais wa Zanzibar kama Amir Jeshi wa JKU, KMKM na vikosi vya SMZ. Kwenye set up ya Muungano, JKU, KMKM na Vikosi vya SMZ sio vyombo vya dola, hivi ni para military, yaani Jeshi Usu, ni migambo tuu kama Auxlary Police, askari wa Tanapa, Ultmate securiy au Group 4. Hivyo Zanzibar haina vyombo vya dola, ila ina mahakama yake inayohudumiwa na polisi wa JMT.
4. Sovereignty. The right to rule give by other nations, Zanzibar haina sovereignty. Sovereignty ni moja tuu, ila leo ndio na mimi nimejifunza humu kumbe kuna sovereignty 2, yaani internal na external sovereignty. Ni kweli Zanzibar ina mamlaka yake ya ndani, lakini sovereignty tunamaanisha sovereignty ya kimataifa. Kwa taarifa tuu, hata hoja ya sovereignty ya ndani, Zanzibar haina!. Mnakikumbuka kisa cha Abdu Jumbe?. Baadhi ya maamuzi muhimu ya mustakabali wa Zanzibar yanafanyika Dodoma. The intenal sovereignty ya Zanzibar mwisho Chumbe. Unaweza usiamini hata mabadiliko ya katiba ya Zanzibar, hayatambuliki na Katiba ya JMT!.
5.International recognition- Zanzibar haina international recognition, haitambuliki UN, ila kwenye baadhi ya nchi za Kiislamu na Kiarabu, Zanzibar inatambulika, na kwavile 98% ya Wanzibari ni Muslims, Zanzibar ilijiunga na OIC kama Zanzibar, lakini kwa vile Kimataifa hakuna Zanzibar, zilipigwa kelele hadi Zanzibar kulazimishwa kujitoa OIC kwa kudanganyiwa pipi, kuwa ijitoe halafu Tanzania itajiunga OIC, na baada ya Zanzibar kujitoa, hadithi ikaishia hapo!. Mpaka leo, mpaka kesho, Zanzibar haiwezi kukopa na kuingia mikataba ya Kimataifa bila udhamini wa JMT!.
6. Sarafu: Zanzibar haina sarafu yake, sarafu ni ya JMT.
Hivyo Zanzibar ni nchi jina tuu but in reality, Zanzibar sio nchi, bali ni sehemu ya JMT. Nchi ni Tanzania.
P