Zanzibar ni nchi huru au ni sehemu ya Tanzania?

Ukinambia ni sehemu ya Tanzania nitakuuliza maswali yafuatayo:

1. Kwanini Watanganyika hawaruhusiwi kumiliki ardhi Zanzibar?

2. Kwanini ni ngumu ajira za Zanzibar kuhusisha Watanganyika?

3. Kwanini wana rais wao na bendera yao?

4. Kwanini wana taasisi zao zinazojitegemea kama mahakama, bunge, tume ya uchaguzi nk?

5. Kwanini timu za Zanzibar zinaiwakilisha Zanzibar kama nchi kwenye mashindano mbalimbali ya CAF kwa ngazi ya vilabu?

6. Kwanini taasisi zao zinaendeshwa tofauti kabisa na Tanzania, mfano kule watu wanatibiwa bure kwa hospitali za serikali, gharama za umeme ni nafuu sana nk?

Ukinambia Zanzibar ni nchi huru nitakuuliza maswali yafuatayo:

1. Kwanini haina amiri jeshi mkuu kwa maana ya kwamba haina jeshi linalojitegemea?

2. Kwanini Tanzania ikikopa Zanzibar wanapata fungu lao tena kwa uwiano usio sawa (Zanzibar inapata ratio kubwa) huku ikiwa mlipaji wa mkopo akiwa Tanzania bara pekee.

3. Kwanini haina sarafu yake yenyewe?

Mtazamo wangu: Muungano una mapungufu mengi.

Huwezi kuwa na Nchi ambayo kuna wakati inakuwa nchi kamili na kuna wakati inakuwa sehemu ya nchi nyingine.

Nadhani ni muda sahihi Zanzibar kuwa mkoa wa Tanzania, ama tuwaachie nchi yao wajitegemee.

Inavyoonekana ni kuwa Nyerere alitaka kuwalaghai Wazanzibari mwisho wa siku akajikuta anatengeneza muungano usioeleweka na sasa madhara yake yapo dhahiri.

Hoja ya usalama kwangu haina mashiko! Kama tumeweza kuilinda mipaka yetu yote dhidi ya nchi korofi zinazotuzunguka tutashindwaje kujilinda dhidi ya Zanzibar?
Ni sehemu ya Tanzania Bali ni autonomy region
 
Mkuu unashangaa nini, mbona kuna madola duniani hayana majeshi !!!
-The Vatican.
-The Sovereign Order of Malta
-The Principality of Andorra

Sawa.

Nadhani umesoma kwa kujibu, hujasoma ili kuelewa. Nimezungumza kwamba kwenye Union Matters watanganyika wanafanya kazi Zanzibar. Lakini huu mfumo uko hata kule Marekani. Kuna ofisi za jimbo na shirikisho. Hapa gumu kuelewa ni lipi ???

Concern yangu hapa ni kuwa bado Watanganyika tunabanwa sana kwenye hili la ajira, while sisi tunaruhusiwa kufanya kazi kule kwenye mambo yanayohusu muungano tu wao wanaruhusiwa kwenye kila kona na siku hizi naona kwenye kila ajira za bara wao wanapewa asilimia 21.

Sio kuwa napinga ulichoeleza
 
Mkuu umetoa somo murua kabisa
Zanzibar siyo nchi (Country), bali ni dola(State) inayounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu muungano uliwekwa kimkataba na hati idhini (Union Charter/Articles of the Union). Hivyo Zanzibar ilipunguza sehemu ya uhuru wake kujiwala (National Sovereignty) kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pili, suala la ajira lina pembe mbili. Kuna pembe ya Muungano na pembe ya Zanzibari. Watanganyika wapo Zanzibari na wanafanya kazi, lakini ni katika zile sehemu za mambo yanayohusu Muungano tu. Jambo kama hili liko hata kule Hong-Kong Uchina, na maisha yanaenda kama kawaida.

Tatu, suala la bendera siyo shida, maana bendera ni utambulisho tu (Emblem of Identity). Hata wewe ukiamua kuwa na bendera yako unaweza kuitengeneza na kuisajili kupitia HAKI-MILIKI (Intellectual Property). Nchini Marekani kila jimbo lina bendera yake na maisha yanaenda vizuri tu. Tena wananda mbali kabisa na kutumia bendera (The Confederate Flag) ya madola ya kusini (Dixie-Land) ambayo yaliasi muungano.

Nne, nadhani jina Raisi ni cheyo tu, hivyo unaweza leo ukamua kumuita Raisi wa Zanzibari wa Zanzibar Waziri Mkuu wa visiwani, Gavana,Sultani au Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Lakini muhimu kujiuliza ni hili: Je, madaraka yake ya Uraisi yanaishia wapi na ukimlinganisha na Raisi mwenzake ??? Utakuja kufahamu ni kwamba Raisi wa Zanzibari hauvuki maji ya Pemba na Unguja, lakini Raisi wa Tanganyika madaraka yake yanavuka maji na kufika Pemba hadi Unguja, katika ngazi ya kitaifa hadi kichama.

Tano, mashirikisho mengi huwa na mihimili na taasisi zinazojitegemea kama mahakama, bunge na serikali zao. Wengine kama Ethiopia walienda mbali zaidi kuwa hata vikosi vyao binafsi vya ulinzi. Nchini Marekani kuna baadhi ya majimbo yana nguvu sana hadi kumuwezesha Gavana kutoa adhabu ya kifo. Hivyo hili la Zanzibar lisikutatize kabisa mkuu.

Sita, kuhusu uwakilishi wa Zanzibari kwenye siasa za kimataifa hilo ni jambo la kawaida sana maana sheria za kimataifa hazikatazi. Tokea mwaka 1945 hadi 1991 Umoja wa Kisovieti ulikuwa una viti vitatu kule Umoja wa Mataifa ambavyo ni vya Urusi, Ukraine na Belarus ilhali wote wanatoka kwenye nchi moja iitwayo The Union of Soviets Socialist Republics (USSR). Hivyo hapa napo binafsi sioni tatizo kabisa.

Saba, kuhusu taasisi kujiendesha kwa utofauti hilo linatokana na uwepo wa madara ya ndani ya kujiendesha (Internal Sovereignty). Hata nchini Uchina, Hong-Kong inajiendesha kitofauti kabisa, nchini Marekani jimbo kama California ambalo huwa linajiendesha kitofauti kabisa na sera zake za kiliberi. Ambacho wengi kinatukera ni kwamba Tanganyika kutoweza kujiamulia mambo yake binafsi. Tunalitaka taifa letu.

Nane, hili la mikopo nakubaliana na wewe kabisa. Zanzibari haitakiwi ipate fungu lolote lile kwenye masuala yasiyo ya muungano (Non-Union Matters) ambayo yanaihusu Tanganyika. Mbaya zaidi hili la kukopa kupitia mngongo wa Tanganyika, ilhali sheria za kimataifa zinaruhusu Zanzibar iweze kukopa yenyewe binafsi. Katiba ya Ujerumani inaruhusu Ujerumani Mashariki na Ujerumani Magharibi kuingia katika mikataba binafsi ya kimataifa na nchi nyingine. Hivyo Ujerumani Mashariki inaruhusiwa hadi kukopa nje, ili mradi tu itoe taarifa kwa serikali ya Muungano.

Tunataka Zanzibar nao wakope kwa jina lao, maana inaruhusiwa kabisa. Huu ujanja wa kutaka kuimiza Tanganyika, umenza kututia kinyaa watu wengi na kutukera sana. Hasahasa unapofanywa na Raisi Mzanzibari ambaye kiuhalisia hakutakuwa kabisa kugusa mambo ya Tanganyika.

Tisa, kuhusu ardhi. Wazanzibari ni watu wenye midomo sana na wanapenda kuongea siasa zao ambazo zimejaa ubaguzi wa rangi na dini. Lakini ukweli mchungu ni kwamba kuna mambo ambayo Tanganyika ikitutumua misuli, lazima wataumia sana. Mwaka 2014 ilifanyika tafiti na kufahamika kwamba kule Zanzibar (1 Square Kilometer inakaliwa na watu 200) wakati huku Tanganyika (1 Square Kilometer inaliwa na watu 20-30).

Tukisema tuanze kuwakazia, nadhani watu kama Raisi Hussein Mwinyi, Raisi Samia, Bakhresa na wapemba wengine ambao wako Dar es Salaam kisheria inabidi wamiliki ardhi kama wawekezaji kupitia kitu kiitwacho The Derivetive Right. Lakini jambo jingine kubwa utafiti wa mafuta ya Zanzibar ulifanywa kipindi cha Raisi Magufuli na kutambulika kwamba baadhi ya miamba yenye mafuta ambayo Zanzibari ingechimba imefika hadi Tanganyika, tena sehemu kubwa iko Tanganyika.

Kiukweli mimi natamani Tanganyika irudi, ikiwezekana kabisa tuvunje huu muungano.

Halafu nyie Moderators mliopo ONLINE (Boqin , Wand , BlackBold , YinYang , Active , Mhariri ) tafadhali tuheshimiane sana. Hili la mimi kuweka nukta .... ili kuwahi nafasi ya kuandika muda nitakaotaka mimi binafsi haliwahusu kabisa. Sasa kujifanya mko kichwani mwangu na kutabiri kwamba navuruga mijadala ni upigaji ramli na uchwani. Nimewavumilia sana kuna siku mkanipa BAN, leo mmefuta nilichoandika. Tafadhali sana heshimuni uhuru wangu na tusipangiane cha kuandika.
 
Muungano una nchi moja tu, ambayo ni Zanzibar.

Watanganyika hawaitaki nchi yao!

Kinachofanyika sasa ni nchi isiyotambulika kuikalia kimabavu na kuidumaza Zanzibar!!
Zanzibar imedumazwa katika eneo lipi?
 
Ukinambia ni sehemu ya Tanzania nitakuuliza maswali yafuatayo:

1. Kwanini Watanganyika hawaruhusiwi kumiliki ardhi Zanzibar?

2. Kwanini ni ngumu ajira za Zanzibar kuhusisha Watanganyika?

3. Kwanini wana rais wao na bendera yao?

4. Kwanini wana taasisi zao zinazojitegemea kama mahakama, bunge, tume ya uchaguzi nk?

5. Kwanini timu za Zanzibar zinaiwakilisha Zanzibar kama nchi kwenye mashindano mbalimbali ya CAF kwa ngazi ya vilabu?

6. Kwanini taasisi zao zinaendeshwa tofauti kabisa na Tanzania, mfano kule watu wanatibiwa bure kwa hospitali za serikali, gharama za umeme ni nafuu sana nk?

Ukinambia Zanzibar ni nchi huru nitakuuliza maswali yafuatayo:

1. Kwanini haina amiri jeshi mkuu kwa maana ya kwamba haina jeshi linalojitegemea?

2. Kwanini Tanzania ikikopa Zanzibar wanapata fungu lao tena kwa uwiano usio sawa (Zanzibar inapata ratio kubwa) huku ikiwa mlipaji wa mkopo akiwa Tanzania bara pekee.

3. Kwanini haina sarafu yake yenyewe?

Mtazamo wangu: Muungano una mapungufu mengi.

Huwezi kuwa na Nchi ambayo kuna wakati inakuwa nchi kamili na kuna wakati inakuwa sehemu ya nchi nyingine.

Nadhani ni muda sahihi Zanzibar kuwa mkoa wa Tanzania, ama tuwaachie nchi yao wajitegemee.

Inavyoonekana ni kuwa Nyerere alitaka kuwalaghai Wazanzibari mwisho wa siku akajikuta anatengeneza muungano usioeleweka na sasa madhara yake yapo dhahiri.

Hoja ya usalama kwangu haina mashiko! Kama tumeweza kuilinda mipaka yetu yote dhidi ya nchi korofi zinazotuzunguka tutashindwaje kujilinda dhidi ya Zanzibar?
Kuwa na bendera sio ishu maana hata Jimbo la Texas marekani inabendera yake but yet bendera ya USA ni yake pia. ......mtazamo tu
 
Zanzibar siyo nchi (Country), bali ni dola(State) inayounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu muungano uliwekwa kimkataba na hati idhini (Union Charter/Articles of the Union). Hivyo Zanzibar ilipunguza sehemu ya uhuru wake kujiwala (National Sovereignty) kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pili, suala la ajira lina pembe mbili. Kuna pembe ya Muungano na pembe ya Zanzibari. Watanganyika wapo Zanzibari na wanafanya kazi, lakini ni katika zile sehemu za mambo yanayohusu Muungano tu. Jambo kama hili liko hata kule Hong-Kong Uchina, na maisha yanaenda kama kawaida.

Tatu, suala la bendera siyo shida, maana bendera ni utambulisho tu (Emblem of Identity). Hata wewe ukiamua kuwa na bendera yako unaweza kuitengeneza na kuisajili kupitia HAKI-MILIKI (Intellectual Property). Nchini Marekani kila jimbo lina bendera yake na maisha yanaenda vizuri tu. Tena wananda mbali kabisa na kutumia bendera (The Confederate Flag) ya madola ya kusini (Dixie-Land) ambayo yaliasi muungano.

Nne, nadhani jina Raisi ni cheyo tu, hivyo unaweza leo ukamua kumuita Raisi wa Zanzibari wa Zanzibar Waziri Mkuu wa visiwani, Gavana,Sultani au Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Lakini muhimu kujiuliza ni hili: Je, madaraka yake ya Uraisi yanaishia wapi na ukimlinganisha na Raisi mwenzake ??? Utakuja kufahamu ni kwamba Raisi wa Zanzibari hauvuki maji ya Pemba na Unguja, lakini Raisi wa Tanganyika madaraka yake yanavuka maji na kufika Pemba hadi Unguja, katika ngazi ya kitaifa hadi kichama.

Tano, mashirikisho mengi huwa na mihimili na taasisi zinazojitegemea kama mahakama, bunge na serikali zao. Wengine kama Ethiopia walienda mbali zaidi kuwa hata vikosi vyao binafsi vya ulinzi. Nchini Marekani kuna baadhi ya majimbo yana nguvu sana hadi kumuwezesha Gavana kutoa adhabu ya kifo. Hivyo hili la Zanzibar lisikutatize kabisa mkuu.

Sita, kuhusu uwakilishi wa Zanzibari kwenye siasa za kimataifa hilo ni jambo la kawaida sana maana sheria za kimataifa hazikatazi. Tokea mwaka 1945 hadi 1991 Umoja wa Kisovieti ulikuwa una viti vitatu kule Umoja wa Mataifa ambavyo ni vya Urusi, Ukraine na Belarus ilhali wote wanatoka kwenye nchi moja iitwayo The Union of Soviets Socialist Republics (USSR). Hivyo hapa napo binafsi sioni tatizo kabisa.

Saba, kuhusu taasisi kujiendesha kwa utofauti hilo linatokana na uwepo wa madara ya ndani ya kujiendesha (Internal Sovereignty). Hata nchini Uchina, Hong-Kong inajiendesha kitofauti kabisa, nchini Marekani jimbo kama California ambalo huwa linajiendesha kitofauti kabisa na sera zake za kiliberi. Ambacho wengi kinatukera ni kwamba Tanganyika kutoweza kujiamulia mambo yake binafsi. Tunalitaka taifa letu.

Nane, hili la mikopo nakubaliana na wewe kabisa. Zanzibari haitakiwi ipate fungu lolote lile kwenye masuala yasiyo ya muungano (Non-Union Matters) ambayo yanaihusu Tanganyika. Mbaya zaidi hili la kukopa kupitia mngongo wa Tanganyika, ilhali sheria za kimataifa zinaruhusu Zanzibar iweze kukopa yenyewe binafsi. Katiba ya Ujerumani inaruhusu Ujerumani Mashariki na Ujerumani Magharibi kuingia katika mikataba binafsi ya kimataifa na nchi nyingine. Hivyo Ujerumani Mashariki inaruhusiwa hadi kukopa nje, ili mradi tu itoe taarifa kwa serikali ya Muungano.

Tunataka Zanzibar nao wakope kwa jina lao, maana inaruhusiwa kabisa. Huu ujanja wa kutaka kuimiza Tanganyika, umenza kututia kinyaa watu wengi na kutukera sana. Hasahasa unapofanywa na Raisi Mzanzibari ambaye kiuhalisia hakutakuwa kabisa kugusa mambo ya Tanganyika.

Tisa, kuhusu ardhi. Wazanzibari ni watu wenye midomo sana na wanapenda kuongea siasa zao ambazo zimejaa ubaguzi wa rangi na dini. Lakini ukweli mchungu ni kwamba kuna mambo ambayo Tanganyika ikitutumua misuli, lazima wataumia sana. Mwaka 2014 ilifanyika tafiti na kufahamika kwamba kule Zanzibar (1 Square Kilometer inakaliwa na watu 200) wakati huku Tanganyika (1 Square Kilometer inaliwa na watu 20-30).

Tukisema tuanze kuwakazia, nadhani watu kama Raisi Hussein Mwinyi, Raisi Samia, Bakhresa na wapemba wengine ambao wako Dar es Salaam kisheria inabidi wamiliki ardhi kama wawekezaji kupitia kitu kiitwacho The Derivetive Right. Lakini jambo jingine kubwa utafiti wa mafuta ya Zanzibar ulifanywa kipindi cha Raisi Magufuli na kutambulika kwamba baadhi ya miamba yenye mafuta ambayo Zanzibari ingechimba imefika hadi Tanganyika, tena sehemu kubwa iko Tanganyika.

Kiukweli mimi natamani Tanganyika irudi, ikiwezekana kabisa tuvunje huu muungano.

Halafu nyie Moderators mliopo ONLINE (Boqin , Wand , BlackBold , YinYang , Active , Mhariri ) tafadhali tuheshimiane sana. Hili la mimi kuweka nukta .... ili kuwahi nafasi ya kuandika muda nitakaotaka mimi binafsi haliwahusu kabisa. Sasa kujifanya mko kichwani mwangu na kutabiri kwamba navuruga mijadala ni upigaji ramli na uchwani. Nimewavumilia sana kuna siku mkanipa BAN, leo mmefuta nilichoandika. Tafadhali sana heshimuni uhuru wangu na tusipangiane cha kuandika.
Nimekuelewa sana mkuuu maana umetoa ufafanuzi wa hali ya juuu.
 
Concern yangu hapa ni kuwa bado Watanganyika tunabanwa sana kwenye hili la ajira, while sisi tunaruhusiwa kufanya kazi kule kwenye mambo yanayohusu muungano tu wao wanaruhusiwa kwenye kila kona na siku hizi naona kwenye kila ajira za bara wao wanapewa asilimia 21.

Sio kuwa napinga ulichoeleza

Tatizo nchi yenu mmeiyeyusha hamuitaki mnaukumbatia u Tanzania ambao mna share Na Zanzibar . Mnapokuja Zanzibar mnakuja kwenye nchi ambayo nyinyi Kama wa Tanzania haiwahusu. Isipokuwa mambo ya muungano ya kitanzania

Zanzibar siyo nchi (Country), bali ni dola(State) inayounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu muungano uliwekwa kimkataba na hati idhini (Union Charter/Articles of the Union). Hivyo Zanzibar ilipunguza sehemu ya uhuru wake kujiwala (National Sovereignty) kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pili, suala la ajira lina pembe mbili. Kuna pembe ya Muungano na pembe ya Zanzibari. Watanganyika wapo Zanzibari na wanafanya kazi, lakini ni katika zile sehemu za mambo yanayohusu Muungano tu. Jambo kama hili liko hata kule Hong-Kong Uchina, na maisha yanaenda kama kawaida.

Tatu, suala la bendera siyo shida, maana bendera ni utambulisho tu (Emblem of Identity). Hata wewe ukiamua kuwa na bendera yako unaweza kuitengeneza na kuisajili kupitia HAKI-MILIKI (Intellectual Property). Nchini Marekani kila jimbo lina bendera yake na maisha yanaenda vizuri tu. Tena wananda mbali kabisa na kutumia bendera (The Confederate Flag) ya madola ya kusini (Dixie-Land) ambayo yaliasi muungano.

Nne, nadhani jina Raisi ni cheyo tu, hivyo unaweza leo ukamua kumuita Raisi wa Zanzibari wa Zanzibar Waziri Mkuu wa visiwani, Gavana,Sultani au Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Lakini muhimu kujiuliza ni hili: Je, madaraka yake ya Uraisi yanaishia wapi na ukimlinganisha na Raisi mwenzake ??? Utakuja kufahamu ni kwamba Raisi wa Zanzibari hauvuki maji ya Pemba na Unguja, lakini Raisi wa Tanganyika madaraka yake yanavuka maji na kufika Pemba hadi Unguja, katika ngazi ya kitaifa hadi kichama.

Tano, mashirikisho mengi huwa na mihimili na taasisi zinazojitegemea kama mahakama, bunge na serikali zao. Wengine kama Ethiopia walienda mbali zaidi kuwa hata vikosi vyao binafsi vya ulinzi. Nchini Marekani kuna baadhi ya majimbo yana nguvu sana hadi kumuwezesha Gavana kutoa adhabu ya kifo. Hivyo hili la Zanzibar lisikutatize kabisa mkuu.

Sita, kuhusu uwakilishi wa Zanzibari kwenye siasa za kimataifa hilo ni jambo la kawaida sana maana sheria za kimataifa hazikatazi. Tokea mwaka 1945 hadi 1991 Umoja wa Kisovieti ulikuwa una viti vitatu kule Umoja wa Mataifa ambavyo ni vya Urusi, Ukraine na Belarus ilhali wote wanatoka kwenye nchi moja iitwayo The Union of Soviets Socialist Republics (USSR). Hivyo hapa napo binafsi sioni tatizo kabisa.

Saba, kuhusu taasisi kujiendesha kwa utofauti hilo linatokana na uwepo wa madara ya ndani ya kujiendesha (Internal Sovereignty). Hata nchini Uchina, Hong-Kong inajiendesha kitofauti kabisa, nchini Marekani jimbo kama California ambalo huwa linajiendesha kitofauti kabisa na sera zake za kiliberi. Ambacho wengi kinatukera ni kwamba Tanganyika kutoweza kujiamulia mambo yake binafsi. Tunalitaka taifa letu.

Nane, hili la mikopo nakubaliana na wewe kabisa. Zanzibari haitakiwi ipate fungu lolote lile kwenye masuala yasiyo ya muungano (Non-Union Matters) ambayo yanaihusu Tanganyika. Mbaya zaidi hili la kukopa kupitia mngongo wa Tanganyika, ilhali sheria za kimataifa zinaruhusu Zanzibar iweze kukopa yenyewe binafsi. Katiba ya Ujerumani inaruhusu Ujerumani Mashariki na Ujerumani Magharibi kuingia katika mikataba binafsi ya kimataifa na nchi nyingine. Hivyo Ujerumani Mashariki inaruhusiwa hadi kukopa nje, ili mradi tu itoe taarifa kwa serikali ya Muungano.

Tunataka Zanzibar nao wakope kwa jina lao, maana inaruhusiwa kabisa. Huu ujanja wa kutaka kuimiza Tanganyika, umenza kututia kinyaa watu wengi na kutukera sana. Hasahasa unapofanywa na Raisi Mzanzibari ambaye kiuhalisia hakutakuwa kabisa kugusa mambo ya Tanganyika.

Tisa, kuhusu ardhi. Wazanzibari ni watu wenye midomo sana na wanapenda kuongea siasa zao ambazo zimejaa ubaguzi wa rangi na dini. Lakini ukweli mchungu ni kwamba kuna mambo ambayo Tanganyika ikitutumua misuli, lazima wataumia sana. Mwaka 2014 ilifanyika tafiti na kufahamika kwamba kule Zanzibar (1 Square Kilometer inakaliwa na watu 200) wakati huku Tanganyika (1 Square Kilometer inaliwa na watu 20-30).

Tukisema tuanze kuwakazia, nadhani watu kama Raisi Hussein Mwinyi, Raisi Samia, Bakhresa na wapemba wengine ambao wako Dar es Salaam kisheria inabidi wamiliki ardhi kama wawekezaji kupitia kitu kiitwacho The Derivetive Right. Lakini jambo jingine kubwa utafiti wa mafuta ya Zanzibar ulifanywa kipindi cha Raisi Magufuli na kutambulika kwamba baadhi ya miamba yenye mafuta ambayo Zanzibari ingechimba imefika hadi Tanganyika, tena sehemu kubwa iko Tanganyika.

Kiukweli mimi natamani Tanganyika irudi, ikiwezekana kabisa tuvunje huu muungano.

Halafu nyie Moderators mliopo ONLINE (Boqin , Wand , BlackBold , YinYang , Active , Mhariri ) tafadhali tuheshimiane sana. Hili la mimi kuweka nukta .... ili kuwahi nafasi ya kuandika muda nitakaotaka mimi binafsi haliwahusu kabisa. Sasa kujifanya mko kichwani mwangu na kutabiri kwamba navuruga mijadala ni upigaji ramli na uchwani. Nimewavumilia sana kuna siku mkanipa BAN, leo mmefuta nilichoandika. Tafadhali sana heshimuni uhuru wangu na tusipangiane cha kuandika.
Zanzibar siyo dola huru kwa sababu:

Haina kiti UN na haitambuliki Kimataifa kama dola yaani state. Vigezo vingine vya kuwa dola vipo ila kimojawapo pekee cha uhuru wa Kimataifa yaani external sovereignty haina.
 
Wakati mwingine huwa unachemka sana Pascal Mayalla .
Muungano wa Union ndiyo nini ?!.

Muungano wetu ni utapeli wa wanasiasa hasa walioko madarakani . Nothing more
Kuna miungano ya aina mbili,
Union na Federation.
Union ni nchi mbili zinaungana na kuunda nchi moja mpya. Zile nchi zote mbili zinapoteza utaifa wake, soverenity, na kuukabidhi kwa nchi mpya. Hivyo Muungano wetu ni Union. Jamhuri ya Tanganyika na Peoples Republic of Zanzibar, ile April 1964 ziliungana kwa Union na kuunda taifa jipya la Tanzania. Tanganyika ikapoteza utaifa wake wote, ikaukabidhi kwa Tanzania. Zanzibar nayo ikapoteza utaifa wake wa Kimataifa na kuukabidhi Tanzania, hivyo kukawa hakuna tena nchi au Taifa la Tanganyika wala Zanzibar, kilichopo ni JMT.

Japo Muungano wetu Kimataifa ni Muungano wa Union nchi mbili kuungana na kugeuka nchi moja, ya JMT yenye rais mmoja, rais wa JMT, yenye serikali moja, serikali ya JMT inayotambulika kimataifa, ikiwemo UN. Lakini kitaifa, Muungano wetu ni Federation ya nchi mbili, zenye marais wawili, serikali mbili zinazojitegemea.

Hivyo Muungano wetu ni unique, ni Muungano wa Union kwa upande mmoja, at the same time ni Muungano wa Federation kwa upande mwingine.
P
 
Nyinyi mnaouwa watu mnaupa sida Uislamu ?
Hapa Duniani kuna watu wanauana wenyewe kwa wenyewe kama waislamu?

Yemen, Iraq, Libya, Sudan, Taliban, Syria nk wote hao ni mashehk, sasa mkiongeza na hayo mambo yenu itakuwaje?
 
Mbona hujibu swali ?

Mnapotuuwa mnaupa sifa Uislamu ?
 
Duh...!.
huku ni kuuchokoa Muungano!.
Ndani ya Muungano, Zanzibar sio nchi, ni sehemu ya JMT inayojitegemea kwa mambo yake ya ndani. JMT ndio nchi. Ni nchi moja yenye rais mmoja wa JMT na Amir Jeshi Mkuu.

Nje ya Muungano, Zanzibar ni nchi, ni moja ya nchi mbili zinazounda JMT.

Muungano wetu ni Muungano unique duniani.
Kwa upande mmoja ni Muungano wa Union, yaani Tanzania ni nchi moja ya JMT, yenye sehemu mbili, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani.

Kwa upande wa pili Muungano wetu ni federation yenye nchi mbili, katiba mbili, serikali mbili na marais wawili, ila kati ya hizo nchi mbili, moja ni dola na nyingine sio dola.
P
Baada ya nchi ya Zanzibar ambayo inajulikana na kila mtu kwa kuwa ina serekali yake inayoongozwa na Rais wake ndugu HUSSEIN MWINYI nchi ya pili ni nchi gani na Rais wake ni nani?.
 
Back
Top Bottom