Zanzibar ni nchi huru au ni sehemu ya Tanzania?

Zanzibar ni nchi huru au ni sehemu ya Tanzania?

Ndani ya Tanzania Zanzibar ni nchi huru kwa kuwa wanauhuru wa kujifanyia chochote wanachokitaka na Rais anayeitwa Rais wa Muungano hana mamlaka yoyote ya kuwaamlia wazanzibar hata mkuu wa wilaya hawezi akawateulia,nje Tanzania Zanzibar siyo nchi huru kwa kuwa haina ubavu wa kujifanyia jambo lolote la kimataifa.
 
Sasa nijibu ujinga?

Mngekuwa mmeuwawa muda huu ungekuwa Online JF?
Kwani ungalikuwa hujapewa ile Huduma, ungaliandika haya ?usiwafanyie uchoyo vijana Na tungaliuwawa usingaliipata kitu yako uipendayo
 
Concern yangu hapa ni kuwa bado Watanganyika tunabanwa sana kwenye hili la ajira, while sisi tunaruhusiwa kufanya kazi kule kwenye mambo yanayohusu muungano tu wao wanaruhusiwa kwenye kila kona na siku hizi naona kwenye kila ajira za bara wao wanapewa asilimia 21.

Sio kuwa napinga ulichoeleza
Muungano huu ni mzigo kwa watanganyika!
 
Zanzibar siyo dola huru kwa sababu:

Haina kiti UN na haitambuliki Kimataifa kama dola yaani state. Vigezo vingine vya kuwa dola vipo ila kimojawapo pekee cha uhuru wa Kimataifa yaani external sovereignty haina.
Hoja ya kutokuwa na kiti UN au kutotambulika ni hoja mufilisi kabisa na zimekaa kisiasa.
Vigezo vikuu vya dola ni hivi ambavyo Zanzibar imekidhi:
1. Government
2. Population
3. Territory
4. Sovereignty (Both Internal and External Sovereignty)

Ambacho Advocate Tundu Lissu amewapotosha watanzania wengi ni lile la kusema kwamba Zanzibar haina External Sovereignty. Hili siyo kweli, Zanzibar ina External Sovereignty kwasababu imewahi kuwa nchi huru hapo awali, lakini External Sovereignty yake inaendeshwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano ambayo Zanzibar ni dola mshirika (Composite State)

Niende mbali zaidi na kusema kwamba, Zanzibar ina External Sovereignty kwasababu ina uwezo wa kuingia makubaliano ya kimataifa (Treaties, Pacts, Covenants and Concessions) peke yake bila kuingiliwa au kuathiriwa na Serikali ya Muungano na Tanganyika. Hapa utasemaje Zanzibar haina Sovereignty wewe ???
 
Kuna miungano ya aina mbili,
Union na Federation.
Union ni nchi mbili zinaungana na kuunda nchi moja mpya. Zile nchi zote mbili zinapoteza utaifa wake, soverenity, na kuukabidhi kwa nchi mpya. Hivyo Muungano wetu ni Union. Jamhuri ya Tanganyika na Peoples Republic of Zanzibar, ile April 1964 ziliungana kwa Union na kuunda taifa jipya la Tanzania. Tanganyika ikapoteza utaifa wake wote, ikaukabidhi kwa Tanzania. Zanzibar nayo ikapoteza utaifa wake wa Kimataifa na kuukabidhi Tanzania, hivyo kukawa hakuna tena nchi au Taifa la Tanganyika wala Zanzibar, kilichopo ni JMT.

Japo Muungano wetu Kimataifa ni Muungano wa Union nchi mbili kuungana na kugeuka nchi moja, ya JMT yenye rais mmoja, rais wa JMT, yenye serikali moja, serikali ya JMT inayotambulika kimataifa, ikiwemo UN. Lakini kitaifa, Muungano wetu ni Federation ya nchi mbili, zenye marais wawili, serikali mbili zinazojitegemea.

Hivyo Muungano wetu ni unique, ni Muungano wa Union kwa upande mmoja, at the same time ni Muungano wa Federation kwa upande mwingine.
P
Kwa kifupi ni muungano wa kipuuzi kuwahi kutokea duniani..yani haueleweki.

#MaendeleoHayanaChama
 
Ukinambia ni sehemu ya Tanzania nitakuuliza maswali yafuatayo:

1. Kwanini Watanganyika hawaruhusiwi kumiliki ardhi Zanzibar?

2. Kwanini ni ngumu ajira za Zanzibar kuhusisha Watanganyika?

3. Kwanini wana rais wao na bendera yao?

4. Kwanini wana taasisi zao zinazojitegemea kama mahakama, bunge, tume ya uchaguzi nk?

5. Kwanini timu za Zanzibar zinaiwakilisha Zanzibar kama nchi kwenye mashindano mbalimbali ya CAF kwa ngazi ya vilabu?

6. Kwanini taasisi zao zinaendeshwa tofauti kabisa na Tanzania, mfano kule watu wanatibiwa bure kwa hospitali za serikali, gharama za umeme ni nafuu sana nk?

Ukinambia Zanzibar ni nchi huru nitakuuliza maswali yafuatayo:

1. Kwanini haina amiri jeshi mkuu kwa maana ya kwamba haina jeshi linalojitegemea?

2. Kwanini Tanzania ikikopa Zanzibar wanapata fungu lao tena kwa uwiano usio sawa (Zanzibar inapata ratio kubwa) huku ikiwa mlipaji wa mkopo akiwa Tanzania bara pekee.

3. Kwanini haina sarafu yake yenyewe?

Mtazamo wangu: Muungano una mapungufu mengi.

Huwezi kuwa na Nchi ambayo kuna wakati inakuwa nchi kamili na kuna wakati inakuwa sehemu ya nchi nyingine.

Nadhani ni muda sahihi Zanzibar kuwa mkoa wa Tanzania, ama tuwaachie nchi yao wajitegemee.

Inavyoonekana ni kuwa Nyerere alitaka kuwalaghai Wazanzibari mwisho wa siku akajikuta anatengeneza muungano usioeleweka na sasa madhara yake yapo dhahiri.

Hoja ya usalama kwangu haina mashiko! Kama tumeweza kuilinda mipaka yetu yote dhidi ya nchi korofi zinazotuzunguka tutashindwaje kujilinda dhidi ya Zanzibar?
Griii!!! 😖😖, kwani kuna editing nyingine zimefanyika😫? Nachojua tulishamaliza na Mizengo!!!! Samahani kwa kuwapigia kelele!!😏
 
Zanzibar siyo nchi (Country), bali ni dola(State) inayounda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Huu muungano uliwekwa kimkataba na hati idhini (Union Charter/Articles of the Union). Hivyo Zanzibar ilipunguza sehemu ya uhuru wake kujiwala (National Sovereignty) kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pili, suala la ajira lina pembe mbili. Kuna pembe ya Muungano na pembe ya Zanzibari. Watanganyika wapo Zanzibari na wanafanya kazi, lakini ni katika zile sehemu za mambo yanayohusu Muungano tu. Jambo kama hili liko hata kule Hong-Kong Uchina, na maisha yanaenda kama kawaida.

Tatu, suala la bendera siyo shida, maana bendera ni utambulisho tu (Emblem of Identity). Hata wewe ukiamua kuwa na bendera yako unaweza kuitengeneza na kuisajili kupitia HAKI-MILIKI (Intellectual Property). Nchini Marekani kila jimbo lina bendera yake na maisha yanaenda vizuri tu. Tena wananda mbali kabisa na kutumia bendera (The Confederate Flag) ya madola ya kusini (Dixie-Land) ambayo yaliasi muungano.

Nne, nadhani jina Raisi ni cheyo tu, hivyo unaweza leo ukamua kumuita Raisi wa Zanzibari wa Zanzibar Waziri Mkuu wa visiwani, Gavana,Sultani au Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Lakini muhimu kujiuliza ni hili: Je, madaraka yake ya Uraisi yanaishia wapi na ukimlinganisha na Raisi mwenzake ??? Utakuja kufahamu ni kwamba Raisi wa Zanzibari hauvuki maji ya Pemba na Unguja, lakini Raisi wa Tanganyika madaraka yake yanavuka maji na kufika Pemba hadi Unguja, katika ngazi ya kitaifa hadi kichama.

Tano, mashirikisho mengi huwa na mihimili na taasisi zinazojitegemea kama mahakama, bunge na serikali zao. Wengine kama Ethiopia walienda mbali zaidi kuwa hata vikosi vyao binafsi vya ulinzi. Nchini Marekani kuna baadhi ya majimbo yana nguvu sana hadi kumuwezesha Gavana kutoa adhabu ya kifo. Hivyo hili la Zanzibar lisikutatize kabisa mkuu.

Sita, kuhusu uwakilishi wa Zanzibari kwenye siasa za kimataifa hilo ni jambo la kawaida sana maana sheria za kimataifa hazikatazi. Tokea mwaka 1945 hadi 1991 Umoja wa Kisovieti ulikuwa una viti vitatu kule Umoja wa Mataifa ambavyo ni vya Urusi, Ukraine na Belarus ilhali wote wanatoka kwenye nchi moja iitwayo The Union of Soviets Socialist Republics (USSR). Hivyo hapa napo binafsi sioni tatizo kabisa.

Saba, kuhusu taasisi kujiendesha kwa utofauti hilo linatokana na uwepo wa madara ya ndani ya kujiendesha (Internal Sovereignty). Hata nchini Uchina, Hong-Kong inajiendesha kitofauti kabisa, nchini Marekani jimbo kama California ambalo huwa linajiendesha kitofauti kabisa na sera zake za kiliberi. Ambacho wengi kinatukera ni kwamba Tanganyika kutoweza kujiamulia mambo yake binafsi. Tunalitaka taifa letu.

Nane, hili la mikopo nakubaliana na wewe kabisa. Zanzibari haitakiwi ipate fungu lolote lile kwenye masuala yasiyo ya muungano (Non-Union Matters) ambayo yanaihusu Tanganyika. Mbaya zaidi hili la kukopa kupitia mngongo wa Tanganyika, ilhali sheria za kimataifa zinaruhusu Zanzibar iweze kukopa yenyewe binafsi. Katiba ya Ujerumani inaruhusu Ujerumani Mashariki na Ujerumani Magharibi kuingia katika mikataba binafsi ya kimataifa na nchi nyingine. Hivyo Ujerumani Mashariki inaruhusiwa hadi kukopa nje, ili mradi tu itoe taarifa kwa serikali ya Muungano.

Tunataka Zanzibar nao wakope kwa jina lao, maana inaruhusiwa kabisa. Huu ujanja wa kutaka kuimiza Tanganyika, umenza kututia kinyaa watu wengi na kutukera sana. Hasahasa unapofanywa na Raisi Mzanzibari ambaye kiuhalisia hakutakuwa kabisa kugusa mambo ya Tanganyika.

Tisa, kuhusu ardhi. Wazanzibari ni watu wenye midomo sana na wanapenda kuongea siasa zao ambazo zimejaa ubaguzi wa rangi na dini. Lakini ukweli mchungu ni kwamba kuna mambo ambayo Tanganyika ikitutumua misuli, lazima wataumia sana. Mwaka 2014 ilifanyika tafiti na kufahamika kwamba kule Zanzibar (1 Square Kilometer inakaliwa na watu 200) wakati huku Tanganyika (1 Square Kilometer inaliwa na watu 20-30).

Tukisema tuanze kuwakazia, nadhani watu kama Raisi Hussein Mwinyi, Raisi Samia, Bakhresa na wapemba wengine ambao wako Dar es Salaam kisheria inabidi wamiliki ardhi kama wawekezaji kupitia kitu kiitwacho The Derivetive Right. Lakini jambo jingine kubwa utafiti wa mafuta ya Zanzibar ulifanywa kipindi cha Raisi Magufuli na kutambulika kwamba baadhi ya miamba yenye mafuta ambayo Zanzibari ingechimba imefika hadi Tanganyika, tena sehemu kubwa iko Tanganyika.

Kiukweli mimi natamani Tanganyika irudi, ikiwezekana kabisa tuvunje huu muungano.

Halafu nyie Moderators mliopo ONLINE (Boqin , Wand , BlackBold , YinYang , Active , Mhariri ) tafadhali tuheshimiane sana. Hili la mimi kuweka nukta .... ili kuwahi nafasi ya kuandika muda nitakaotaka mimi binafsi haliwahusu kabisa. Sasa kujifanya mko kichwani mwangu na kutabiri kwamba navuruga mijadala ni upigaji ramli na uchawi. Nimewavumilia sana kuna siku mkanipa BAN, leo mmefuta nilichoandika. Tafadhali sana heshimuni uhuru wangu na tusipangiane cha kuandika.
Safi kabisa!
 
Hoja ya kutokuwa na kiti UN au kutotambulika ni hoja mufilisi kabisa na zimekaa kisiasa.
Vigezo vikuu vya dola ni hivi ambavyo Zanzibar imekidhi:
1. Government
2. Population
3. Territory
4. Sovereignty (Both Internal and External Sovereignty)

Ambacho Advocate Tundu Lissu amewapotosha watanzania wengi ni lile la kusema kwamba Zanzibar haina External Sovereignty. Hili siyo kweli, Zanzibar ina External Sovereignty kwasababu imewahi kuwa nchi huru hapo awali, lakini External Sovereignty yake inaendeshwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano ambayo Zanzibar ni nchi mshirika.

Niende mbali zaidi na kusema kwamba, Zanzibar ina External Sovereignty kwasababu ina uwezo wa kuingia makubaliano ya kimataifa (Treaties, Pacts, Covenants and Concessions) peke yake bila kuingiliwa au kuathiriwa na Serikali ya Muungano na Tanganyika. Hapa utasemaje Zanzibar haina Sovereignty wewe ???
Internal sovereignty ipo nusu maana Zanzibar inaweza kusimamia sheria zake ila kwa upande mwingine haiwezi kusimamia usalama wake.

External sovereignty haina kwa sababu haiwezi kujihusisha naa masuala ya Kimataifa na pia haitambuliki kama dola na Taifa huru
 
ni wakati sasa wa kuanza huu mjadala kwa mapana zaidi lakini sihuoni muungano miaka 20 ijayo,
ila wazanzibar wajiandae kisaikolojia
Ewaaa!

Binafsi hiki kitendo cha Zanzibar kukopa kwa kutumia Jamhuri ya Muungano kinanikera sana. Wakati uwezo wa wao kukopa wanao. Huu mzigo unamuangukia JMT ambaye ni Tanganyika. Hili suala linaonekana ni la makusudi kabisa!
 
Walisemaaaa weeeeeee,
Leo munasemaaaaa weeeeee,
Mwisho wa siku kwenye pande zote mbili kuna wanaotaka uwepo na wanaotaka uvunjike
 
Kisa mnapata gawio la bure...hamchangii hata senti kwenye bajeti ya the so called muungano.

#MaendeleoHayanaChama
Mukiuvunja mutakaohasirika ni nyie,
Sie hatutaki kuuvunja
Ila mukilazimisha na uvunjike tu
Hasara nyingi kukiko faida
 
Ukinambia ni sehemu ya Tanzania nitakuuliza maswali yafuatayo:

1. Kwanini Watanganyika hawaruhusiwi kumiliki ardhi Zanzibar?

2. Kwanini ni ngumu ajira za Zanzibar kuhusisha Watanganyika?

3. Kwanini wana rais wao na bendera yao?

4. Kwanini wana taasisi zao zinazojitegemea kama mahakama, bunge, tume ya uchaguzi nk?

5. Kwanini timu za Zanzibar zinaiwakilisha Zanzibar kama nchi kwenye mashindano mbalimbali ya CAF kwa ngazi ya vilabu?

6. Kwanini taasisi zao zinaendeshwa tofauti kabisa na Tanzania, mfano kule watu wanatibiwa bure kwa hospitali za serikali, gharama za umeme ni nafuu sana nk?

Ukinambia Zanzibar ni nchi huru nitakuuliza maswali yafuatayo:

1. Kwanini haina amiri jeshi mkuu kwa maana ya kwamba haina jeshi linalojitegemea?

2. Kwanini Tanzania ikikopa Zanzibar wanapata fungu lao tena kwa uwiano usio sawa (Zanzibar inapata ratio kubwa) huku ikiwa mlipaji wa mkopo akiwa Tanzania bara pekee.

3. Kwanini haina sarafu yake yenyewe?

Mtazamo wangu: Muungano una mapungufu mengi.

Huwezi kuwa na Nchi ambayo kuna wakati inakuwa nchi kamili na kuna wakati inakuwa sehemu ya nchi nyingine.

Nadhani ni muda sahihi Zanzibar kuwa mkoa wa Tanzania, ama tuwaachie nchi yao wajitegemee.

Inavyoonekana ni kuwa Nyerere alitaka kuwalaghai Wazanzibari mwisho wa siku akajikuta anatengeneza muungano usioeleweka na sasa madhara yake yapo dhahiri.

Hoja ya usalama kwangu haina mashiko! Kama tumeweza kuilinda mipaka yetu yote dhidi ya nchi korofi zinazotuzunguka tutashindwaje kujilinda dhidi ya Zanzibar?
Ni mkoa maalum wa Tanzania
 
Back
Top Bottom