Zanzibar ni nchi huru au ni sehemu ya Tanzania?

Zanzibar ni nchi huru au ni sehemu ya Tanzania?

Hahaaaa..hii hoja haiko sawa kabisa..cha msingi SMZ iuliwe haina mana uwepo wake..kama zote Tanganyika na Zanzi ziliamua kuuunda Tanzania why kuwepo serikali ya smz..ambayo kila uchwao inaonyesha dalili ya kujifanya taifa huru.?

Suala la ardhi hoja ya kuwa visiwa ni vidogo sidhani kama inamashiko mana hii ni nchi moja na katiba inaruhusu mtu yoyote kuishi mahali popote ndani ya JMT huoni zenj ni wabinafsi.

Sambamba na hilo..hivi SMZ inachangia kiasi gani kwenye pato la the so called JMT.?

#MaendeleoHayanaChama
Zanzibar haichangii hata ndururu kwenye Muungano.
P
 
Zenji ni Nchi yenye bahati ya kuvuna kwenye shamba la bibi!! 2021-2025 ni kipindi cha mavuno. Kikiongezeka hadi 2030 watavuna kiasi ambacho hawatahitaji tena shamba la bibi! Watakuja na mkwara wa kujitenga!!!!! Itakuwa imeshakuwa Dubai ya Africa!!
Kwasasahiv ni mkoa wa Tz.
 
Ongea yote lakini Karume aliingizwa mkenge na Nyerere mtoto wa mjini akagawa nchi kupitia Hati Idhini ya Muungano (Articles of the Union). Zanzibar siyo nchi bali dola, nchi Tanzania. Hutaki unaacha, lakini ukweli ndiyo huo.

Kuhusu Zanzibari kujitoa kwenye Muungano: Binafsi nasema hata leo usiku wakitaka watoke tu.
Usiwadanganye eti wakitaka watoke!. It's very unfortunately zile artcles of Union sio contract ni aggreement, tumeungana for life, hakuna kipengele cha kuvunja Muungano, hivyo huu muungano wetu adhimu, tutaulinda kwa gharama yoyote!.

Mkuu Pascal unamaanisha unachoongea, au unaongea ili watu fulani waone msimamo wako?
 
Uchina ya kikomunisti (Peoples Republic of China) haikuwa na kiti Umoja wa Mataifa na haikutambuliwa na mataifa ya magharibi hadi mwaka 1979. Unataka kuniambia kwamba Uchina haikuwa dola ???

Kuhusu kusimamia usalama wake: Nchi kama Vatican na Andorra zinasimamiaje Usalama wake ilhali hazina hata majeshi ???

Kuilinganisha nchi ya Zanzibar na Taifa la Vatican (Holly Sea/ Holly Chair)ni sawa na kulinganisha mlima na kichuguu.

Ni hivi, ili kitu (entity) iwe dola (state) inapaswa kuwa ni vigezo vinne.

1. Watu.
2. Serikali.
3.Eneo(territory)
4. Sovereignty (Uhuru) both uhuru wa ndani ya mipaka na nje ya mipaka.

Vatican, ina Mkuu wa nchi, ambaye ni Pope, na huyu Pope anaongoza watu ambao ni Wakatoliki. Mfano, mimi ni Mkatoliki, kwa hiyo nipo chini ya sheria za Katoliki/Vatican. Kwa hiyo Vatican inafuzu kigezo cha kuwa na WATU.

Serikali: Vatican wana Serikali ambayo Mkuu wake ni Pope na chini yake kuna Makadinali, Maaskofu, Maaskofu Wakuu, Maparoko, Mapadre, Mashemasi, Frateri, na Baraza la Waleyi.

Eneo: Vatican ina eneo la kiutawala.

Uhuru ( Sovereignty). Vatican ina uhuru wake wa ndani na ina sheria zake ambazo ndiyo Canon Law. Vatican ina Mahakama zake ambazo ni Canon Courts. Kuna walinzi wa usalama na wengineo.

Kuhusu uhuru wa nje; Vatican ina mabalozi zaidi ya 180+ duniani kote, ikiwemo hapa Tanzania. Vatican ina Kiti Umoja wa Mataifa, inaweza kusaini Mikataba na nchi nyingine duniani.

Kwa hiyo, utaona utofauti wa Vatican na Zanzibar kwamba Vatican ina Sovereignty both internal and external ila Zanzibar haina.

Zanzibar is not sovereign, but Vatican Holly Sea/ Holly Chair is.
 
Mbona Zanzibar ina Rais na serikali huku Tanganyika ikikosa vyote hivyo?......huku si kuwanyima haki raia wa Tanganyika?
Hakuna raia wa Tanganyika.

Uraia wa Tanganyika uliisha tangu April 26, 1964, ambapo Taifa la Tanganyika na Zanzibar yaliungana, na kuzaliwa Tanzania.

Tanganyika na Zanzibar zilipoteza uhuru wao na kuzaliwa Dola huru Tanzania.

Hao raia wa Tanganyika wako wapi na wanaishi sehemu gani?
 
Mtabwabwaja sana mwaka hii. Walipokua wanataka kujitenga mlikua mnawabania sasa ona povu livyowatoka.

Na kwa taarifa yenu mkataba hauvunjiki, wazinzibari ndo washafika. Chapeni kazi tujenge nchi. Tuacheni kujihisisha Na vitu vilivyo nje ya uwezo wetu.
 
Zanzibar kwanza ni taifa, a nation (a large group of people who inhabit a specific territory and are connected by history, culture, or another commonality). Wanzanzibari wana historia, wana utamaduni. Wazanzibari popote walipo duniani wanajitambua kama Wazanzibari na wanatambulika kama Wazanzibari. Asili ya Wazanzibari haipotei. Zanzibar ilivamiwa na Nyerere na jeshi lake ikapoteza uhuru. Siyo kupungua, ilipoteza kabisa. Lakini kutokana kuwa Zanzibar ni taifa, lazima kuna siku uhuru utarudi.

Tanganyika haikuwa taifa, ilikuwa ni mkusanyiko wa makabila uliowekwa pamoja na serikali ya Uingereza wakaita Tanganyika. Tanganyika ilikuwa haina historia, haina utamaduni wake. Ni nchi bandia (artificial country). Nyerere alilijua hili na ndiyo maana kwake ilikuwa rahisi kuiua Tanganyika, kuvamia Zanzibar na kuunda nchi mpya aliyoita Tanzania ambayo nayo ni batili (artificial country). Nchi ya kweli ambayo ilipoteza uhuru wake ni Zanzibar pekee kwa sababu Zanzibar ni taifa kwanza.

Zanzibar kwanza ni taifa, a nation (a large group of people who inhabit a specific territory and are connected by history, culture, or another commonality). Wanzanzibari wana historia, wana utamaduni. Wazanzibari popote walipo duniani wanajitambua kama Wazanzibari na wanatambulika kama Wazanzibari.
,.........................

Unàfahamu tofauti ya 'taifa', 'nchi' na 'dola'?
...............

Asili ya Wazanzibari haipotei. Zanzibar ilivamiwa na Nyerere na jeshi lake ikapoteza uhuru.
..................
Nyerere 'alivamia' Taifa la Zanzibar au Nchi ya Zanzibar?

Siyo kupungua, ilipoteza kabisa. Lakini kutokana kuwa Zanzibar ni taifa, lazima kuna siku uhuru utarudi.
......................

Taifa ni watu, kwani Wazanzibari hawapo huru? Unachanganya kati ya nation, state, na country

Tanganyika haikuwa taifa, ilikuwa ni mkusanyiko wa makabila uliowekwa pamoja na serikali ya Uingereza wakaita Tanganyika. Tanganyika ilikuwa haina historia, haina utamaduni wake. Ni nchi bandia (artificial country).
................

Unaona. Umeanza kusema Tanganyika ilikuwa Taifa, halafu ukasema tena Tanganyika ilikuwa nchi ......Kuna tofauti. Unachanganya.

Nyerere alilijua hili na ndiyo maana kwake ilikuwa rahisi kuiua Tanganyika, kuvamia Zanzibar na kuunda nchi mpya aliyoita Tanzania ambayo nayo ni batili (artificial country).
...................
Haya

Nchi ya kweli ambayo ilipoteza uhuru wake ni Zanzibar pekee kwa sababu Zanzibar ni taifa kwanza.
..........'
 
Hakuna raia wa Tanganyika.

Uraia wa Tanganyika uliisha tangu April 26, 1964, ambapo Taifa la Tanganyika na Zanzibar yaliungana, na kuzaliwa Tanzania.

Tanganyika na Zanzibar zilipoteza uhuru wao na kuzaliwa Dola huru Tanzania.

Hao raia wa Tanganyika wako wapi na wanaishi sehemu gani?
Kwanini utambulisho wa Tanganyika ufe na wa Zanzibar uwepo?....hii sio sawa.
 
No sio kuwanyima haki, bali ni Tanganyika ndio tumefaidika zaidi, kabla ya Muungano, Tanganyika ilikuwa ni eneo la Tanganyika tuu, baada ya Muungano, Tanganyika ikabadili jina kuwa Tanzania na sasa eneo lote la JMT ni letu Zanzibar inclusive!. Serikali ya JMT ndani yake ndio kuna serikali ya Tanzania Bara kwa mambo ambayo sio ya Muungano.
P
Faida ni kuongeza eneo la utawala tu.....ila gharama zingine kama madeni tunabeba Tanganyika japo mikopo wote tulifaidi....hii sio sawa.

Haturuhusiwi hata kumiliki ardhi kule ila huku ni sawa wao kumiliki.
 
Zanzibar kwanza ni taifa, a nation (a large group of people who inhabit a specific territory and are connected by history, culture, or another commonality). Wanzanzibari wana historia, wana utamaduni. Wazanzibari popote walipo duniani wanajitambua kama Wazanzibari na wanatambulika kama Wazanzibari. Asili ya Wazanzibari haipotei. Zanzibar ilivamiwa na Nyerere na jeshi lake ikapoteza uhuru. Siyo kupungua, ilipoteza kabisa. Lakini kutokana kuwa Zanzibar ni taifa, lazima kuna siku uhuru utarudi.

Tanganyika haikuwa taifa, ilikuwa ni mkusanyiko wa makabila uliowekwa pamoja na serikali ya Uingereza wakaita Tanganyika. Tanganyika ilikuwa haina historia, haina utamaduni wake. Ni nchi bandia (artificial country). Nyerere alilijua hili na ndiyo maana kwake ilikuwa rahisi kuiua Tanganyika, kuvamia Zanzibar na kuunda nchi mpya aliyoita Tanzania ambayo nayo ni batili (artificial country). Nchi ya kweli ambayo ilipoteza uhuru wake ni Zanzibar pekee kwa sababu Zanzibar ni taifa kwanza.
Wewe ni muongo tena. Muongo mkubwa. Zanzibar iwe na history halafu Tanganyika ikose history ?! Mbona umeikuza mno zanzibar na kuidunisha Tanganyika. Kwa lipi hasa ?!.

Muungano hata mimi siukubali achilia mbali kuupenda. Lakini si kwa kuidunisha Tanganyika. Zanzibar haina kitu Tanganyika ikikaa pembeni. Zaidi zaidi kutegemea misaada .
 
Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar, zote mbili zilikufa ile April 26, 1964 kwa kupoteta sovereignty zake, na kuzikabidhi kwa Taifa jipya la Tanzania. Tanganyika ikalifuta hadi jina na kugeuka Tanzania Bara. Zanzibar ili maintain jina lake.
P
Why P. ?!
 
Ukinambia ni sehemu ya Tanzania nitakuuliza maswali yafuatayo:

1. Kwanini Watanganyika hawaruhusiwi kumiliki ardhi Zanzibar?

2. Kwanini ni ngumu ajira za Zanzibar kuhusisha Watanganyika?

3. Kwanini wana rais wao na bendera yao?

4. Kwanini wana taasisi zao zinazojitegemea kama mahakama, bunge, tume ya uchaguzi nk?

5. Kwanini timu za Zanzibar zinaiwakilisha Zanzibar kama nchi kwenye mashindano mbalimbali ya CAF kwa ngazi ya vilabu?

6. Kwanini taasisi zao zinaendeshwa tofauti kabisa na Tanzania, mfano kule watu wanatibiwa bure kwa hospitali za serikali, gharama za umeme ni nafuu sana nk?

Ukinambia Zanzibar ni nchi huru nitakuuliza maswali yafuatayo:

1. Kwanini haina amiri jeshi mkuu kwa maana ya kwamba haina jeshi linalojitegemea?

2. Kwanini Tanzania ikikopa Zanzibar wanapata fungu lao tena kwa uwiano usio sawa (Zanzibar inapata ratio kubwa) huku ikiwa mlipaji wa mkopo akiwa Tanzania bara pekee.

3. Kwanini haina sarafu yake yenyewe?

Mtazamo wangu: Muungano una mapungufu mengi.

Huwezi kuwa na Nchi ambayo kuna wakati inakuwa nchi kamili na kuna wakati inakuwa sehemu ya nchi nyingine.

Nadhani ni muda sahihi Zanzibar kuwa mkoa wa Tanzania, ama tuwaachie nchi yao wajitegemee.

Inavyoonekana ni kuwa Nyerere alitaka kuwalaghai Wazanzibari mwisho wa siku akajikuta anatengeneza muungano usioeleweka na sasa madhara yake yapo dhahiri.

Hoja ya usalama kwangu haina mashiko! Kama tumeweza kuilinda mipaka yetu yote dhidi ya nchi korofi zinazotuzunguka tutashindwaje kujilinda dhidi ya Zanzibar?
Zanzibar ni ki mkoa kimojawapo nchini Tanzania, asilimia 70 ya wakazi weusi wa Zbr wametoka bara.

Nipo Kizi Mkazi, njooni tule Kitimoto
 
Kuilinganisha nchi ya Zanzibar na Taifa la Vatican (Holly Sea/ Holly Chair)ni sawa na kulinganisha mlima na kichuguu.
Umeona ulivyo unazungumza vitu kwa kukaririshwa: The Vatican City na The Holly See ni viti viwili tofauti. Tena ukizungumza hivi mbele ya watu wasomi utadharaurika sana. The Vatican City na The Holy See ni kitu kimoja tokea lini ???

Haya sikiliza sasa: The Vatican ni nchi na dola ambayo ni makao makuu ya kanisa takatifu la mitume la Katoliki, huku The Holly See ni serikali inayoongoza kanisa takatifu la mitume la kikatoliki. The Vatican City na The Holly See kisheria tunasema vyote ni watu (They both have legal personality).

Sasa iko hivi, kabla ya kuzaliwa The Vatican City mwaka 1929 kupitia The Lateran Pacts, The Holly See ilikuwepo na ndiyo imeendesha kanisa la Katoliki tangu kuanguka kwa dola la kipapa kipindi cha Mfalme Napoleon Bonaparte mwaka 1809. Vatican kama nchi na dola imezaliwa mwaka 1929.

The Vatican IS NOT The Holly See, let this sink within depths of your cranium. Nakushauri mkuu, uandike hoja baada ya kufanya tafiti za kina.

Ni hivi, ili kitu (entity) iwe dola (state) inapaswa kuwa ni vigezo vinne.

1. Watu.
2. Serikali.
3.Eneo(territory)
4. Sovereignty (Uhuru) both uhuru wa ndani ya mipaka na nje ya mipaka.
Umejichanganya sana. Wewe siyo raia wa Vatican wewe ni raia wa Tanzania, ambaye yuko chini ya sheria za nchi ya Tanzania: Sheria za Vatican ambazo zinakuongoza wewe ni zile kidini (Canon and Ecclesiastical Laws), tena kwenye mambo machache kama ndoa, talaka na ubatizo wa watoto. Ukienda Vatican ndiyo utabanwa na sheria za huko.

Sasa hivyo vigezo vya dola ambavyo umeniwekea hapa, navyo umevichanganya sana. Vimetolewa na mkataba wa monte-video (The Monte-Video Convention of 1933) ambao ulitoa vigezo vya taifa au dola ambavyo ni: Permanent Population, Government, Defined Territory and Sovereignty.

Sasa The Vatican haina idadi ya watu ya kudumu (Permanent Population) watu wa pale huja na kuondoka baada ya kumaliza utumishi wao na kurudi nchini kwao. Ndiyo maana nakwambia hivi, kukosekana kwa kigezo kimoja haimaanishi kwamba dola siyo huru.

Kama kigezo ni SOVEREIGNTY, kuna nchi kama The Sovereign Military Order of Malta (SMOM) ambayo haina Political Sovereignty lakini bado inatambulika kama nchi na ina ushawishi mkubwa sana kimataifa. Haya mambo inabidi yafanyiwe tafiti sana kabla ya kukimbilia kuwasikiliza wanasiasa kama Tundu Lissu.
 
Usiwadanganye eti wakitaka watoke!. It's very unfortunately zile artcles of Union sio contract ni aggreement, tumeungana for life, hakuna kipengele cha kuvunja Muungano, hivyo huu muungano wetu adhimu, tutaulinda kwa gharama yoyote!.
P
Kwenye sheria ya Marekani kuna kitu kinaitwa THE FEDERAL COMPACT, (Ndiyo nadharia unayiongea hapa)kinachodai kwamba yale madola yaliingia kwenye mkataba wa maisha, hivyo sehemu ya uhuru wao ikafa na sasa wanadhaminiwa na serikali ya shirikisho.

Lakini hii ni nadharia tu, kwasababu uhalisia wenyewe hauko hivyo. Pamoja na THE FEDERAL COMPACT (Mkataba wa kudumu) wanaume miaka ya 1860 walashika mtutu, na kutengeneza nchi yao (The Dixie Land), hapo ikafahamika kwamba mkataba ulikuwa ni wa kudumu au lah.

Walitoka wakina Kossovo kule Serbia sembuse Zanzibar. Siku wakubwa wa dunia hii waliochangia kuzaliwa kwa huu muungano wakiamua Zanzibar iwe huru, itakuwa huru tu ndani ya usiku mmoja, na siku hiyo mtatambua kwamba mkataba huo ni wa kuduma au lah.

Binafsi nachukia mno Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar......
 
Back
Top Bottom